NASAHA
Na. 062 Jumatano  Agosti 23 - 29, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
LISHE 

Unakula au unaliwa? 

MARA nyingi watu hupenda kupata ua kufanya mambo fulani fulani kwa kukusudia kupata kitu fulani inaweza kukugharimu pesa na muda mwingi. Bila kujua, unafika mwisho hakupata alichotarajia. Wengi wetu tunaweza kugundua kuwa hatukupata lakini kwa upeo finyu watu wengi hushindwa kujua wamepata au wamekosa. Haya yaweza kutokea kwenye biashara, masomo n.k. Hapo ndipo yanapokuja maswali unakula au unaliwa ndugu wewe?!

Kwa upande wa lishe haya yanaweza kutokea kabisa. Hasa haya yanapatikana katika mtindo wa kununua na kula.Unatafuta fedha kwa nguvu zote, kisha unapanga matumizi yako kwa bajeti finyu. Je unachonunua kwa ajili ya kula kinakunufaisha vile ulivyokusudia au unatupa pesa zako bure? 

Kuna baadhi ya vyakula ambavyo havina virutubisho vya kutosha kulingana na bei yake. Vinywaji baridi ni mfano wa karibu kabisa. Haiyumkini kila mmoja wetu anapata soda katika mwezi mzima.Soda inauzwa sh.200 lakini kilichomo humo ni maji, sukari, rangi na kemikali zisizounufaisha mwili. Ni bora ukanywa maziwa kikombe kidogo kimoja cha shs.100 na kipande cha keki cha sh.100. Tofauti ya thamani mwilini kati ya soda na maziwa na keki, hata mtoto mdogo anaweza kukwambia. Hivyo basi badala ya kuliwa na soda wewe kula maziwa na keki inayokupatia nguvu vitamini, madini, na protini ndani yake. Kamani suala la kinywaji baridi hata maziwa pia yapo ya baridi. 

Mbali ya soda vinywaji vinavyowekwa kwenye chupa kama black currant na squshi, juice mbali mbali za kwenye mifuko pia ni hatari kwa afya na ni upotevu wa fedha bila kujua. Unaweza kukuta mgonjwa ananunuliwa juisi ya rangi nyekundu eti ili aongeze damu! Masikini kumbe humo ni rangi tu na wala si damu inayofikiriwa. Au hata maji ya zabibu kwenye chupa au ya matunda, vyote hivi ni kiini macho tu. Hakuna cha matunda ndani yake wala uhalisia wowote bali ni wizi wa kutumia akili. Unatoa wewe mwenyewe pesa mkononi na kununua hujaitwa wala kulazimishwa. 

Kama hili huliamini soma kwenye paketi au chupa za vinywaji mbalimbali kilichomo kimetengenezwa na nini. Utaambulia "Artificial flavour" ladha ya kutengeneza, rangi,sukari na dawaza kuzuia isiharibike. Hivyo wajijaza dawa mwilini mwako bila kujua ambazo zaweza kukuzuru hata wewe.Tunakushauri ujizoeshe na kuamini kuwa vyakaula halisi ndio bora zaidi kuliko vyakula vya viwandani. Chungwa moja la sh.10/- linathamani kuliko juisi au soda ya 200/=. Sasa hapo ni kula au kuliwa? 

Vinywaji hivi pia huwa na sukari nyingi ambazo ni hatari kwa afya, hasa kwa meno na wenye matatizo ya kisukari. Usiozeshe meno ya mwanao au kumjaza madawa mwanao au wewe mwenyewe bila sababu ya msingi. Tengeneza maji ya matunda wewe mwenyewe kwa njia nyepesi tu za kukamua au kupondaponda na kuchuja katika hali ya usafi. Usimpe mtoto pesa aende nazo shule akanunulie soda bali mtayarishie mwanao kinywaji toka kwenye matunda halisi. 

Vyakula vinapokuwa vimeharibika hutoa dalili mbalimbali za kuonesha kuwa havifai tena.Vyaweza kutoa harufu tofauti na ile ya awali (mbaya) kubadilika rangi n.k. Pamoja na hayo, watu hupuuza na kula vivyo hivyo vilivyo. Matokeo yake hupelekea kuumwa tumbo na kuharisha na kupoteza maji na virutubisho vingine. Gharama inarudi kwenye dawa na malipo ya kumwona daktari. Umekula au umeliwa? 

Waweza kuona chakula kina uvundo hafifu 'mouldy' , hasa kwa vilivyolala na kuwekwa kwenye joto. Vinyoa hivyo huwa na sumu ambayo hudhuru bila kuonesha haraka madhara yake. Kuwa mwangalifu kuchagua mikate au af-keki (half cake)inayokaa muda mrefu, kwani vijidudu 'fungus' wanaweza kujificha ndani yake. 

Epuka kula vyakula vilivyoachwa vya moto kwa muda mrefu kwani joto ni hali inayopendwa na vijimelea aina ya bakteria kuzaliana. 

Usinywe maji ovyo au juisi za mitaani zisizochemshwa ili mradi tu ni rahisi kwa bei lakini ni ghali kifaya. Barafu na aina zake vyote havina thamani sana mwilini kulingana na bei yake. 

Unapotoa pesa zako, jiulize unakula au unaliwa pesa zako? 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Kama hamtaki demokrasia, mnataka nini basi?

Prof. Lipumba ana uwezo wa kuongoza nchi - CCM

Kampeni za uchaguzi 2000, CCM yamalizia muda wake na kusema:
Imefanya kazi ya ‘kuipendeza’ Marekani

Vita dhidi ya rushwa ianzie kwa vigogo -Lipumba

Wakati umefika wanawake kushiriki siasa - Mugissa

TLP yadaiwa kuukejeri Uislamu

CUF Kigamboni kuzindua kampeni leo

USHAURI NASAHA
Nimechoka kuwa mtangazaji wa redio

MAKALA
Mungu na mataifa ya dunia

MAELEZO BINAFSI
Mjue mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Lipumba

MIPASHO NASAHA
Krosi matiplikesheni!

MAKALA
Wananchi kajiandikisheni kupiga kura ili kuleta mabadiliko ya serikali kwa njia ya amani

KALAMU YA MWANDISHI
Mkijirekebisha mtakaribishwa

Habari za Kimataifa

LISHE
Unakula au unaliwa?

MASHAIRI

MICHEZO

  • Yanga, Mtibwa nani bingwa leo?
  • Ugomvi mkubwa baina ya Simba na Yanga waibuka 
  • Arsenal yaitandika Liverpool
  • Ngorongoro Heroes yaenda Msumbiji

  •  


    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita