NASAHA
Na. 062 Jumatano  Agosti 23 - 29, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Ushauri Nasaha 
 
 

Nimechoka kuwa mtangazaji wa redio

Na Khadija M. Idd 

Ni kweli hasa wala si utani, wala uongo kwamba nimechoka kufanyakazi ya utangazaji wa redio hususani zile za kizamani (Redio za siku hizi zina simu).Labda msomaji utashangaa imekuwaje leo mshauri NASAHA amekasirika na kukata tamaa namna hii? Unajua, habari yenyewe iko hivi, mtangazaji akiwa studio anaendelea na kazi yake kama kawaida huku wakati mwingine 'akicheka na' wasikilizaji, akiuliza na kujijibu maswali mbalim, bali kama afanyavyo anti Iki wa TVZ katika kipindi cha maoni ya watoto kwa picha, au akitoa tabasamu la mwaka na 'ahsante' nyingi kwa wasikilizaji kama wafanyavyo watangazaji wa CNN. Hivi mtangazaji huyu anajua kuwa hao wasikilizaji wenyewe wapo?!

Basi huko kuchoka kwangu kunatokana na halihiyo ya kufanyakazi huku akidhani kwamba kuna watuwaliowasha redio au televisheni. Kumbe maskini ya Mungu, pengine hakuna anayesikiliza au kuangalia stesheni yako! 

Hata hivyo mimi simtaganzaji bali nachukuwa mfano huo kuwafahamisha wasomaji wangu kuwa sipendi na si suala la kupenda tu bali taaluma yangu ya saikolojia na ushauri NASAHA hairuhusu NASAHA kushughulikia tatizo la mteja yeyote bila yeye mwenyewe kuwa tayari. Nafikiri nimekuwa nikifanyakazi bila ya ridhaa ya wasomaji wangu; kutafuta cha kuandika nakudhani kwamba walengwa wamepata ujumbe na wameufurahia au wameukubali. Kumbe nililoandika si tatizo kwao, au hata kama ni tatizo si kubwa kama nilivyolionesha. Mambo yamekuwa kiuvyogo uvyogo! 

Sasa ndugu msomaji unaponikasirikia kuwa sijaandika juu ya tatizo linalokusibu wewe na utu uzima huo na yule mwanao tototundu mimi nitajuaje. Au nyinyi wasomaji wa kule Jang'ombe Zanzibar,kule Kiparang'anda, huko Mkuti, Masasi, Same, Chamwino, Kyela niambieni basi nitajuaje basi kwamba hili nililoliandika hapa linahitajika sana kwenu au haliwafai. Sasa wakati tunafikiria la kufanya ili mshauri NASAHA asiendelee kuwa mtangazaji wa redio,labda tuangalie kisa hiki. 

Siku moja wakati nimepumzika nyumbani mtu mmoja wa karibu yangu alinisuta tena mbele ya wageni. Kwamba wewe unaandika habari za watu tu kila siku au za watoto. Kwa kweli nilishikwa na butwaa na hata hivyo nilimjibu kadri nilivyoweza. Hata hivyo msuto huo ulinipa mwanga na kunirudisha nyuma enzi za shule, nikang'amua kwamba, alaa kumbe kuna wanaokereka na baadhi ya makala! Lakini huyu mtu yu karibu nami akitaka kuniambia lolote kuhusu makala atanitafuta na kunieleza. Sasa vipi yule aliyeko Mahuta, Newala, au yule wa Sakina, Arusha. Na yule wa Mufindi akikereka anafanya nini? 

Wapendwa wasomaji haya yalikuwa ni maelezo baada ya habari, la kuzingatia hapa ni kuwa zana za uwazi na ukweli zinaturuhusu kusoma na kusikika. Karne ya demokrasia inatutaka tuhoji kabla ya kukubali, basi kwa vigezo hiyo mshauri NASAHA anakueleza, badala ya kunung'unika na kususa kusoma gazeti lako la NASAHA mwandikie na ueleze kero iliyokusibu, tatizo linalokusumbua na msaada unaouhitaji. Maoni na mapendekezo yako yanaweza kuwa ni amri kwa mshauri NASAHA na yanaweza kuondoa mtivyogo wa mambo! 

Anuani yetu ni ile ile: Mshauri NASAHA, S.L.P 75042, DSM

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Kama hamtaki demokrasia, mnataka nini basi?

Prof. Lipumba ana uwezo wa kuongoza nchi - CCM

Kampeni za uchaguzi 2000, CCM yamalizia muda wake na kusema:
Imefanya kazi ya ‘kuipendeza’ Marekani

Vita dhidi ya rushwa ianzie kwa vigogo -Lipumba

Wakati umefika wanawake kushiriki siasa - Mugissa

TLP yadaiwa kuukejeri Uislamu

CUF Kigamboni kuzindua kampeni leo

USHAURI NASAHA
Nimechoka kuwa mtangazaji wa redio

MAKALA
Mungu na mataifa ya dunia

MAELEZO BINAFSI
Mjue mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Lipumba

MIPASHO NASAHA
Krosi matiplikesheni!

MAKALA
Wananchi kajiandikisheni kupiga kura ili kuleta mabadiliko ya serikali kwa njia ya amani

KALAMU YA MWANDISHI
Mkijirekebisha mtakaribishwa

Habari za Kimataifa

LISHE
Unakula au unaliwa?

MASHAIRI

MICHEZO

  • Yanga, Mtibwa nani bingwa leo?
  • Ugomvi mkubwa baina ya Simba na Yanga waibuka 
  • Arsenal yaitandika Liverpool
  • Ngorongoro Heroes yaenda Msumbiji

  •  


    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita