NASAHA
Na. 062 Jumatano  Agosti 23 - 29, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
HABARI 
 
 

Wakati umefika wanawake kushiriki siasa - Mugissa 

Na Tinker A. Mdimu 

KARNE ya ishirini na moja imemzindua mwanamke wa Kitanzania katika siasa kuona wakati umefika wa kupima na kuamua jambo ambalo linaweza kuleta manufaa kwa kulinganisha na maisha ambayo wanaishi hivi sasa.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa wanawake na watoto Taifa wa chama cha CUF, Bibi Rossalia Nabina Mugissa alipokuwa akifungua matawi 26 ya chama cha CUF katika kata ya Vingunguti jimbo la Ukonga wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Bibi Mugissa alisema, amefurahishwa kuona wanawake wa tawi la Sarafina lililopo kata ya Vingunguti jimbo la Ukonga wilaya ya Ilala wamepata uongozi wao wenyewe bila ya kushirikiana na wanaume kuanzia Mwenyekiti hadi wajumbe wote wa tawi. 

Mama Mugissa aliendelea kusema, hayo ni maendeleo makubwa katika chama chake kufikia hatua hiyo ambapo ni wakati muafaka hivi sasa dunia nzima inapiga kelele juu ya wanawake kushika nafasi mbalimbali za uongozi iwe ni katika chama, serikali, mashirika ya umma au katika taasisi. 

Aliendelea kusema: " Hakuna kitu ambacho hatuwezi kukifanya cha kuleta maendeleo yetu, ni kiasi cha bibi au mabibi kupanga na kutiana moyo na lengo litafikiwa". 

Akishirikiana na Naibu Mkurugenzi wa Fedha, Bibi Ghania Chaurembo katika ufunguzi huo, walishusha bendera za UDP na kupandisha za CUF na kurudishiwa kadi 60 za chama cha UDP. 

Matawi yaliyofunguliwa ni Desmond Tutu, Curl Peters, Galatasary, Tetea Amani, Faru 'B', Nyota Njema, Mbele kwa Mbele, Mtambani 'B' ambalo lilikukuwa tawi la UDP. 

Mengine ni tawi la Mchongomani, Mwembe karata, pia lililokuwa tawi la UDP Mtambani 'A' kwa Simba Sokoni UDP kwa Simba, Martin Luther King na tawi la Wahutu. 

Mengine ni tawi la wapendanao, tawi la Kubali yaishe, Tawi la Sarafina, tawi la mji mpya, tawi la Ukombozi, tawi la Vijana Taifa la leo, tawi la Mashujaa halilii bunduki, kwa Tekero na Viagra. Jumla matawi yalikuwa 26. 

Walioshiriki katika ufunguzi huo walikuwepo mgombea Ubunge wa jimbo la Ukonga kupitia Chama cha CUF Bw. Msina, Udiwani Bw. Said Kimburu, Mkurugenzi wa Wanawake Bibi Rossalia N. Mugissa, Bibi Zainab Khalfan kaimu Mkurugenzi wanawake wilaya ya Ilala, Bibi Jamile Ally mjumbe mkutano mkuu taifa. 


TLP yadaiwa kuukejeri Uislamu

Na Mwandishi Wetu 

JUMUIYA wanafunzi Waislamu wa mkoa wa Kilimanjaro wamedai kwamba chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kinachoongozwa na Augustine Lyatonga Mrema kimeukejeli, kuudhalilisha Uislamu na Waislamu hapa Tanzania.

Kwa mujibu wa tamko lao la Agosti mwaka huu, uliyosainiwa na Musa Ramadhani ambaye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa jumuiya hiyo, imedaiwa kwamba mgombea mwenza wa Bwana Mrema anayetambulishwa kama Sheikh alisema Waislamu ni watu wanaotumiwa na kufuata mkumbo. 

".....kwenye Uwanja wa Mashujaa katika Manispaa ya Moshi mjini ..... Sheikh Ali alitoa maneno ya kuwashutumu na kuwakejeli Waislamu kwa kuwaita ni watu wenye kufuata mkumbo tu, ni watu wa kutumiwa na Misikiti yao ni vituo vya watu wanaotaka uongozi katika nchi...." Ilisomeka sehemu ya tamko la wanafunzi hao. 

Hivi karibuni baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani walidai kwamba chama cha TLP ni chama cha Kanisa Katoliki na hawako tayari kushirikiana nacho. 


CUF Kigamboni kuzindua kampeni leo

Na Mandishi Wetu 

CHAMA Cha Wananchi (CUF) katika Jimbo la Kigamboni ambalo ni moja kati ya majimbo mawili ya uchaguzi ya Wiya ya Tgemeke kinatarajia kufungua rasmi mikutano yake ya kampeni leo katika viwanja vya Zakhem.

Mwinyekiti wa jimbo hilo Bwa.Msamaha A. Msamaha akiongea na mwandishi wa habari hizi alisema kuwa mkutano huo wa kuwanadi mgombea ubunge na madiwani wa chama chake katika Jimgo hilo utahudhuriwa pia na viongozi wa wilaya, akiwemo mwenyekiti wake Mhe.Tambwe Hiza. Pia ameleza Bw. Msamaha kuwa Mchungaji Christopher Mtikila naye atapata muda wa kuongea na wananchi. 

Mgombea ubunge wa CUF katika Jimbo hilo ni Bw.Frank Magoba, ambaye Bw. Msamaha amemwelezea kuwa ni mtu anayekubalika na kwamba ni chagua la wananchi wa Kigamboni. Hivyo amedai kuwa ushindi dhidi ya chama chake uko wazi hasa ikizingatiwa kuwa hata wanachama wa kambi ya CCM wamechoswa na rushwa ilichokigubika chama cha CCM wakati wa kura za maoni jimboni humo. 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Kama hamtaki demokrasia, mnataka nini basi?

Prof. Lipumba ana uwezo wa kuongoza nchi - CCM

Kampeni za uchaguzi 2000, CCM yamalizia muda wake na kusema:
Imefanya kazi ya ‘kuipendeza’ Marekani

Vita dhidi ya rushwa ianzie kwa vigogo -Lipumba

Wakati umefika wanawake kushiriki siasa - Mugissa

TLP yadaiwa kuukejeri Uislamu

CUF Kigamboni kuzindua kampeni leo

USHAURI NASAHA
Nimechoka kuwa mtangazaji wa redio

MAKALA
Mungu na mataifa ya dunia

MAELEZO BINAFSI
Mjue mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Lipumba

MIPASHO NASAHA
Krosi matiplikesheni!

MAKALA
Wananchi kajiandikisheni kupiga kura ili kuleta mabadiliko ya serikali kwa njia ya amani

KALAMU YA MWANDISHI
Mkijirekebisha mtakaribishwa

Habari za Kimataifa

LISHE
Unakula au unaliwa?

MASHAIRI

MICHEZO

  • Yanga, Mtibwa nani bingwa leo?
  • Ugomvi mkubwa baina ya Simba na Yanga waibuka 
  • Arsenal yaitandika Liverpool
  • Ngorongoro Heroes yaenda Msumbiji

  •  


    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita