|
Na. 062 Jumatano Agosti 23 - 29, 2000 |
|
|
|
|
|
Krosi matiplikesheni! Na Abu Halima Sa Changwa WIKI hii nilikuwa biiize, kwa hiyo sikuweza kupitapita mitaani kuangalia mambo mambo huku na kule. Lakini nilikuwa nikifuatilia kwa makini mambo yanaenda vipi duniani kwa ujumla. Nimekutana na msamiati pale nilipokuwa nikisikia na kusoma kuhusu nyambizi ya Urusi iliyozama. Neno nyambizi ni geni kwangu, sijui ni jipya au vipi, lakini ndio hivyo, nyambizi imezama na wapiganaji mia na ushee wa Urusi ya mbabe Putini wameangamia. Kwa vile nimepata msamiati, naweza sasa kuutumia. Vyama vya siasa ni nyambizi, sijui ni ipi itazama kama ya mbabe Putini, maana naona mvutano ni mkubwa kweli, wala hautabiriki. Nasema hivi kwa sababu ni jana tu nilikuwa na lundo la magazeti mapya. Mara katika gazeti moja wapo nikakutana na kichwa cha habari MREMA AUBAINI UZEMBE WA WAKRISTO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA. ATAWANYA WARAKA KWA MAASKOFU KUMI, YUMO PENGO, MUSHEMBA NA KAKOBE. Nikashangaa, Ama! Huyu si ndiye yule aliyesikika hapa juzi tu akivishutumu vyama fulani kwamba vina udini. Sasa imekuwaje? Maaskofu na uchaguzi mkuu wapi na wapi! Haya! Jingine lililonishangaza zaidi, kwenye gazeti jingine maarufu, kulikuwa na habari yenye kichwa cha habari: MAKANISA KUTOA ELIMU YA UCHAGUZI. Nikaona Mh! Mambo hayo. Tena leo makanisa na uchaguzi, wakati tumewasikia viongozi wa serikali na wengine wa Kanisa wakikemea kuchanganya dini na siasa. Sasa habari hii ilimuelezea askofu Kyaruzi akisema: "Ni makosa makubwa na ni dhambi mbele za Mungu kwa Mkristo kutojiandikisha hali akijua kuwa ni agizo la Mungu kwa Taifa lolote kuwa na viongozi ambao pia wanashiriki kulisaidia kanisa kuabudu kwa uhuru na amani". Kinyume cha mambo ni kwamba, kule Tanga, kuna shehe wa Answar Sunna anawaambia Waislamu kwamba ni haramu kujiandikisha, ni haramu kupiga kura kuchagua viongozi wa kikafiri. Hoja yake anasema, inakuwaje Waislamu wajihusishe na vyama au serikali inayojitangaza yenyewe kwamba haina dini? Lakini mara twasikia taasisi yake imetoa pesa kujenga ofisi ya CCM. Sasa huku kama sio kuwakoroga, na kuwakomfyuzi na kuwachanganya watu, ni nini? Halafu kiongozi wa dini akichanganya watu anawachanganya kweli kweli! Hapa Dar kuna mashehe ngangari, wao wanawaambia Waislamu, kura ni WAAJIB. Na aya wanazo. Hawa nawaita ngangari kwa sababu misemo yao imewatia sekeseke la nguvu, tofauti na maaskofu. Mashehe hawa wamekurupushwa kwa kile kinachoitwa kuchanganya dini na siasa, lakini hawakomi. Wamo tu. Habari za akina Kyaruzi kuhimiza waumini wao, sio kuchanganya. Lakini akisema Mbukuzi, Loh! Alijisemea Marehemu Kighoma Malima, ndege wote walie, lakini akilia bundi, uchuro! Haya! Jingine nililolipata kwenye magazeti hayo ya jana ni la hao hao wanadini kujihusisha na siasa. Nasikia huko Jangwani alikuwapo Al-Ma'ruuf, Qaasim ibn Mtopea. Sasa hivi yuko CCM. Nasikia kakung'uta aya mpaka ambazo bado hazijashuka: INNALLAAHA LAA YUGHAYYIRU NI'MATIHII Kwa kweli, kusoma kwangu kooooooote, sijawahi kubahatika kukumbana na aya hii. Lakini Jangwani huwa kuna mambo. Pale wanakwenda watu wengi kutoa neno. Ni kiwanja cha dini mbali mbali kuchemka. Nyingine za kupunga mashetani, nyingine za kufungisha ndoa. Sasa pengine Asshaikhun Kabiir, Ibn Mtopea alishushiwa Wahyi. Hiyo labda haitakuwa ajabu, maana manabii wengi walishushiwa aya zao wakiwa jangwani. Nabii Musa (as) alikuwa jangwani, Nabii Muhammad (saw) alikuwa jangwani. Naye Mtopea alikuwa Jangwani. Mambo hayo! Huku kwingine nako, kwenye Qaaf (CUF) yupo Reverendi Cristopha. Naye ametoka jela juzi na moto wake, na anasema hakomi, kwa mujibu wa gazeti moja. SAA YA UKOMBOZI NI SASA! Twaambiwa atakuwa na Profesa Ngangari katika ziara zote za kampeni mikoani. Hapo nyuma tulisikia shutuma, CCM wakisema kwamba CUF ni chama cha Waislamu. Mimi nilikuwa nasubiri tu ukweli wa mambo, kama nilivyosema wiki iliyopita, Satyameva Jayate van ri tam. [Ukweli huwa juu ya uongo]. Hii imeanza kuonekana kampeni zilipoanza tu. Sisi yetu macho na masikio. Shutuma za Uislamu wa CUF zitaingia wapi? Huku CCM kuna sheikh MTOPEA, tayari kuwapaka MATOPE wapinzani. Na huku kuna mchungaji MTIKILA, tayari KUWATIKISA watawala. Hapa ndipo unapopata krosi matiplikesheni. Nyambizi ipi itazama, tutajua oktoba. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Prof. Lipumba ana uwezo wa kuongoza nchi - CCM Kampeni
za uchaguzi 2000, CCM yamalizia muda wake na kusema:
Vita dhidi ya rushwa ianzie kwa vigogo -Lipumba Wakati umefika wanawake kushiriki siasa - Mugissa CUF Kigamboni kuzindua kampeni leo USHAURI NASAHA
MAKALA
MAELEZO BINAFSI
MIPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
LISHE
|
|
|
|
|