NASAHA
Na. 060 Jumatano  Agosti 9 - 15, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
HABARI ZA KIMATAIFA
 
 

Waislamu Kashmir mezani na India

Kashmir

KIKUNDI cha wapiganaji wa Kiislamu cha huko Kashmir Hizbu-Mujahidin wiki hii wameanza mazungumzo ya ana kwa ana na India ili kutatua mgogoro wa pande hizo mbili.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa India Bwana Kamar Pande amekutana na makamanda wanne wa Hizbu Mujahidin na kuunda kamati maalum.

Kamati hiyo itashughulikia suala la kusitisha mapigano na kuelekea mazungumzo ya amani.

Wiki iliyopita kikundi hicho cha Kiislamu kilitangaza kusimamisha mapigano kati yake na India kwa muda wa miezi mitatu ili kufanya majadiliano ya mezani.

Hata hivyo kuna vikundi vingine vya Kiislamu vimepinga hatua hiyo ya kusimamisha mapigano.

Vikundi hivyo vimetaka mapigano yaendelee hadi India isalimu amri.

Hizbu wametoa sharti la mazungumzo kuwa lazima Pakistan ishirikishwe, jambo ambalo India imelikataa.

Kiongozi mkuu wa Hizbu - Mujahidin aliyepo Pakistan amesema kuwa atafikiria wiki ijayo kuvunja mazungumzo hayo endapo India itashikilia msimamo wake huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Koffi Annan amezitaka India na Kashmir zijizuie na mapigano na badala yake zimfanye mazungumzo kufikia amani ya kudumu.

Naye balozi wa Marekani nchini India amezitaka pande hizo zifanye moyo wa kustahimilivu na kuendelea na mazungumzo.

India na Kashmir zipo katika mapigano ambayo yamechukua zaidi ya miaka kumi na kugharimu maisha ya maelfu ya watu.

Kashmir ambayo ina Waislamu wengi kuliko dini nyingine inataka kujitenga na kuanzisha Jamhuri huru ya Kiislamu.

Nayo India ambayo inakalia kwa mabavu jimbo hilo inailaumu Pakistan kwa kusadia wapiganaji hao wa Kiislamu kwa hali na mali.

Hata hivyo India kwa kutumia helikopta za kijeshi inaendesha msako katika wilaya ya Dode huko Kashmir kuwasaka wapiganaji wa Kiislamu.

Waziri Mkuu wa India Bwana Bhehar Vajpayee amekwenda kutembelea familia zilizopitwa janga hilo.


Saddam Hussein awashutumu Waarabu

BAGHDAD, Iraq

RAIS wa Iraq ameyashutumu mataifa ya Ghuba na Kiarabu kwa kuendelea kuyaruhusu mataifa ya Marekani na Uingereza kuweka vituo vya kijeshi katika nchi zao.

Akiongea katika kuadhimisha miaka 12 tangu kusimamishwa kwa vita kati yake na Iran iliyodumu kwa miaka minane, Rais huyo amesema ni aibu kuona ndege za Marekani na Uingereza zikuruka katika nchi za ghuba, huku zikiangamiza maisha ya malaki ya wananchi wa Iraq.

Amesema kutokana na vita hiyo kuna mafunzo zaidiya 58, baadhi ya mafunzo hayo ni usimchokoze nyoka kabla hujajiandaa, usiwalinganishe marafiki na maadui zako.

Akiwa amevalia suti yake nyeusi, amesema, sasa atabadilisha mfumo wa hotuba zake, amewataka viongozi wa nchi hizo wasimuatamie adui zao.

Kwa miaka mingi sasa, Iraq imekuwa ikisifiwa kama ngome ya nchi za Kiarabu.


Taleban wamalizia ngwe

AFGHANISTAN

WANAMGAMBO wa Kiislamu wa Taleban huko Afghanistan wiki hii wamepambana na kuwasambaratisha wapinzani huko 'Ishkemesh' Takat.

Talaban ambao wanamiliki asilimia 90 ya Afghanistan wamebakiwa na kundi moja la upinzani likiongozwa na Bw. Shah Masudi.

Kikundi cha Bw. Masudi kinashirikiana na utawala ulioondolewa madarakani mnamo mwaka 1996 wakati Talaban ilipokamata mji wa Kabul.

Baada ya kuundoa madarakani utawala wa kisekula wana Talaban hao waliasisi utekelezaji wa sharia ya Kiislamu.

Wiki iliyopita walifanya shambulio huko 'Baghlan' dhidi ya wapinzani.

Tajikistan imelalamikiwa na Afghanistan kuwa inawasaidia wapinzani dhidi ya Talaban.

Juu
 

YALIYOMO
 

KAULI YA WAISLAMU
BAKWATA na Kanisa

Karume adaiwa ‘kutafuta ujiko’ kwa kutofautiana na Mkapa

Mkapa akiuka sera yake-Chuo Kikuu

Uandikishaji wapiga kura waanza

NLD, NRA, PONA vyamruka Mrema

CUF  yataja wagombea wake Temeke

CCM yamtuhumu Mwenyekiti wake pandikizi

Propaganda ya Udini itaisambaratisha nchi - CHADEMA

USHAURI NASAHA
Kumsaidia mtoto aweze kujitegemea

MAKALA
Lengo la propaganda

MIPASHO NASAHA
NJOZI! NJOZI!

MAKALA
Tujihadhari na risasi za sukari

KALAMU YA MWANDISHI
Popo Bawa la kisiasa

Je, unajua haki yako unapokamatwa na polisi?

Habari za Kimataifa

LISHE
Ulaji wa matunda

MASHAIRI

MICHEZO

  • Baada ya kuitumia kuigaragaza Simba: Shungu akiri ‘ngangari' ni kiboko
  • Manga azikwa Moro
  • •••Dewji ahusishwa na kifo cha mnyama Simba
  • Lunyamila, Kayoza waongoza kwa mabao

  •  


    Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita