|
Na. 060 Jumatano Agosti 9 - 15, 2000 |
|
|
|
|
|
Kumsaidia mtoto aweze kujitegemea KUJITEGEMEA hapa tunachukulia kuwa ni uwezo wa mtoto kutenda na kukidhi haja zake bila kutegemea msaada wa wakubwa. Ieleweke wazi kuwa,kujitegemea huku hakujumuishi kujitafutia malazi, chakula,mavazi, elimu au usalama .Hapa tunaangalia uwezo wa mtoto kusema shida zake bila kusemewa na mtu mzima, kuvaa nguo mwenyewe, kupiga mswaki, kula n.k. Hata hivyo kulingana na tabia ya makuzi, uwezo wa kuieleza ndio unaotangulia kwani mtoto anamudu kutumia lugha kabla hajaweza kuoga au kupiga mswaki. Makala yetu ya leo basi itaangalia jinsi ya kumsaidia mtoto kutumia lugha kueleza hisia na mahitaji yake. Mzazi au mlezi anawajibu mkubwa wa kumsaidia mtoto anayemlea kutumia lugha ili kubainisha mahitaji yake apate kutekelezewa,kubainisha pia hisia zake ili wale anaoishi nao waelewe anavyojisikia juu ya jambo fulani kama analipenda ua halipendi, kama anapenda chakula fulani au la, kama ameudhika na jambo fulani au la. Iwapo kuna jambo au kitu fulani ambacho mtoto anakuhitaji, afundishwe ajieleze vipi ili kuwafahamisha anaoishi nao kuwa anahitaji, kwa mfano, machungwa na si miwa aliyopewa. Mzazi pia amfundishe mtoto namna nzuri ya kujieleza. Kwa mfano, aombe kwa adabu na si kulazimisha anapohitaji kitu. Katika kumfundisha hivi, itasaidika kuondoa hali ya mtoto kulia au kuharibu vitu pale anapohitaji kitu fulani. Itarahisisha mawasiliano baina yake na wale anaoishi nao, kwani ikumbukwe kuwa si kila mtu anao uwezo wa kuelezwa kwa nini mtoto analia sana au anakuwa mnyonge wakati fulani. Vilevile, mtoto anaweza kusaidiwa kwa sisi wenyewe wazazi au walezi kuonesha mfano kama vile mtoto anapokosea, tusikimbilie kumchapa bali tutumie lugha kwanza kumuonesha kuwa alichokifanya hakikubaliki katika jamii na familia na, hivyo asirudie tena. Tunapotumia lugha katika hali kama hii tunamfundisha mtoto kuwa anapochukizwa na kitu aseme kwamba amechukia au kwamba hapendi jambo fulani asilie bali aseme kwamba hapendi. Wakati mtoto anaposhindwa kusema kuwa nataka kujisaidia na akakaa kimya mpaka akajichafua, inaweza kutia hasira kwa mazazi au mlezi, au unaweza kukosa mtu wa kukubali kubaki na mwanao unapokuwa na shughuli nje ya nyumbani. Ili kuzuia hali kama hii, hatuna budi basi kumsaidia mtoto aweze kusema anapohitaji kujisaidia na kumsaidia kumuonesha choo au msalani ulipo ili hali ya kumtegemea mtu mzima amfanyie kila kitu ipungue au kuondoka kabisa, kwani mtoto akielewa hivi licha ya kusema anahitaji kujisaidia, mtoto huyu atakwenda mwenyewe chooni bila kusindikizwa. Hata hivyo, katika kufanya hivyo mzazi au mlezi azingatie umri wa mtoto na usalama wake kwanza (vyoo vingine vinamatundu ambayo mtoto anaweza kutumbukia iwapo atakwenda bila mtu mzima, usafi wa choo pia unaweza kuhatarisha afya ya mtoto). Mtoto mwingine anaweza kukosa ujuzi wa kujieleza pale ambapo anasikia njaa badala yake akaamua kulia, kulala n.k. Mzazi yeyote anayemuelewa mtoto wake anafahamu vyema kuwa mtoto huyo akisikia njaa anakuwaje. Katika hali kama hii mtoto hutegemea uwezo wa mzazi wake kutafsiri kilio au hasira zake. Lakini je, mtoto huyu atakuwa na mama yake wakati wote na mahali popote? Jibu ni hapana. Hivyo ni vyema kwa nmzazi huyu kumfundisha mtoto wake aweze kujieleza kuwa anasikia njaa naanahitaji chakula na si kulia. Amueleweshe pia kuwa kujieleza ni njia rahisi ya kuweza kueleweka, na mara moja shida yake inaweza kuanza kushughulikiwa. Wakati mwingine mtoto anaweza kuumia au kupata homa, katika hali kama hii anahitaji msaada wa haraka ili kumpunguzia maumivu aliyonayo. Mtoto ambaye hawezi kujieleza anaweza kukaa kimya na akaendelea na michezo yake ingawa badala ya kusimama, ataonekana amekaa au kulala. Hii inaweza kusababisha athari kubwa zaidi. Mtoto anapokuwa na homa, na homa ikiendelea kuwa kali anaweza kupata degedege na hali hiyo ikiendelea mtoto huyo baadaye ataonekana kama vile ana kifafa au taahira ya akili. Mtoto aliyejichoma na msurmari, chupa, au kujikata na bati anawezakupata tetenus asiposhughulikiwa mapema. Katika hali kama hizi ni lazima tumfundishe mtoto kujieleza kwani inawezakana kuwa hakuna mtu mkubwa aliyemwona. Kujitegemea kwake katika kujieleza kutasaidia kupatiwa msaada wa haraka. Kwa ujumla tumsaidie mtoto aweze kujitegemea kulingana na umri wake, na kwa kuangalia yale anayoyaweza. Tumfundishe kupiga simu polisi, kuita gari la wagonjwa (ambulance), kutoa taarifa kikosi cha zimamoto (fire brigade) n.k. iwapo uwezo wake wakujieleza umekomaa kuweza kufanya hivyo. Tupunguze hali ya kutegemea wakubwa hata pale ambapo wanaweza kutenda bila msaada wao. |
YALIYOMO
KAULI
YA WAISLAMU
Karume adaiwa ‘kutafuta ujiko’ kwa kutofautiana na Mkapa Mkapa akiuka sera yake-Chuo Kikuu Uandikishaji wapiga kura waanza CUF yataja wagombea wake Temeke CCM yamtuhumu Mwenyekiti wake pandikizi Propaganda ya Udini itaisambaratisha nchi - CHADEMA USHAURI NASAHA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
Je, unajua haki yako unapokamatwa na polisi? LISHE
|
|
|
|
|