|
Na. 060 Jumatano Agosti 9 - 15, 2000 |
|
|
|
|
|
Popo Bawa la kisiasa Na Maalim Bassaleh KATIKA miaka ya nyuma, hapa jijini Dares Salaam kulitokea uvumi kuwa kulikuwapo na shetani aliyekuwa akiitwa Pop Bawa. Kwa kukaririwa mara kwa mara, uvumi huo ukasambaa kwa kasi kama moto katika nyika. Mradi kikaingia kishindo kikubwa sana, mpaka wakaazi wengi wa mkoa huu wakaingiwa na woga wa kubakwa na Popo Bawa! Safari moja ikaja habari kuwa Pop Bawa ametiwa nguvuni, na ameshikiliwa katika kituo cha Polisi cha Buguruni. Watu wa kila rika wakamimimika katika kituo hicho kumwangalia kiumbe huyo wa ajabu. Kilichochangia zaidi kukubalika kwamba kweli alikuwapo Popo Bawa ni kuwa kila aliyerudi kutoka Buguruni alihakikisha kweli ameshuhudia tokeo la kukamatwa Popo Bawa! Ilikuwa ukipita mitaani utakuta makundi ya watu yakizungumzia juu ya kukamatwa kwa dude hilo. Mimi mwenyewe siku hiyo nilipokuwa nikipita karibu na soko kuu la Kariakoo, nilimwona kijana mmoja wa Kibaniani ambaye alikuwa ni jirani yangu na ni dereva wa teksi, amezungukwa na KUNDI KUBWA LA WATU, WAKIMSIKILIZA AKIWAELEZEA JUU YA TUKIO HILO LA BUGURUNI. Aliwahadithia kuwa yeye mwenyewe alikuwa akitokea huko Buguruni, na ameshuhudia jambo hilo. Baadhi ya wale waliokuwa wakimsikiliza wakasema, "wako wapi wale waliokuwa wakipinga habari za Popo Bawa, waje wamsikilize huyu dereva wa teksi. Yeye mwenyewe ametokea Buguruni na amemwona Popo Bawa!" Hata na mimi nilikuwa karibu nimsadiki. Lakini ikanipitikia akilini kwa nini kwanza simwulizi maswali ili kupata uhakika? Basi nikamwuliza, "wewe unatokea Buguruni hivi sasa?" Akanijibu, "Diyo!" Nikaendelea kumwuliza, "Wewe umemwona kwa macho yako huyo Popo Bawa?" Akasema, "Mimi hapana ona kwa macho. Lakini mimi ona watu mingi Polisi Buguruni. Yote wasema Popo Bawa kwisa kamata. Iko dani polisi!" Pale pale nikakumbuka maneno ya Gobbels, aliyekuwa Waziri wa Propaganda wa utawala wa Hitler, katika vita vikuu vya dunia. Gobbels alisema kuwa jambo lo lote, japokuwa la uongo, ukitaka litangae na likubalike upesi basi litangaze, kasha ulikariri mara kwa mara. Naam, japokuwa habari, za Popo Bawa zilikuwa ni uzushi, lakini kwa vile zilikuwa zikikaririwa mara kwa mara watu wakazisadiki. Baadhi ya watu, tena wengi tu, wakaingiwa na hofu, kwa jambo lisilokuwapo kabisa! Basi na juzi, Jumapili Agosti 6, 2000, nilipokuwa nikisikiliza mdahalo baina ya wagombea wa kiti cha Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamadi wa chama cha wananchi (CUF) na Mheshimiwa Amani Abeid Karume wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa mara nyingine nikayambuka yale maneno ya mwana propaganda wa Hitler, Gobbels. Kwa nini? Ni kwa sababu mmoja kati ya wale waliopewa fursa ya kumwuliza maswali mgombea wa CUF, Maalim Seif, alishindwa kuitumia nafasi yake hiyo aliyopewa, na badala yake alitumia fursa hiyo kummiminia shutuma mgombea huyo pamoja na chama chake cha CUF. Alidai kuwa chama cha CUF eti kina udini. Ni chama cha Waislamu. Aliendelea kudai kuwa eti chama hicho kinawatumikia Waarabu na kwamba Maalim Seif akishinda uchaguzi mkuu ujao na kuingia madarakani atavunja Muungano wa Tanzania! Maalim SeifShariff,ambaye pia, ni Katibu Mkuu wa Chama Cha \cU\f, alikanusha shutuma hizo. |Alimjibu mtu huyo kuwa maneno yakehayo hayana msingi wo wote. Ni shutuma tupu. Niuzushi uliopandikizwa na chama kinachokipinga chama cha CUF. Maalim Seif alisema hana mpango wo wote wa kuvunja muungano; bali anakusudia kuuimarisha zaidi. Alisema sera ya chama hicho ya kuwa na muungano wa serikali tatu inakusudiwa kuondoa matatizo yanayotokea mara kwa mara katika muungano huo, ambayo mara nyingi yametishia kuuvunja hata muungano wenyewe. Katika mdahalo huo ulioandaliwa na shirika la utagazaji la BBC, na kutangazwa moja kwa moja kutoka Zanzibar, mgombea huyo wa kiti cha Urais wa Zanzibar, kwa tiketi ya chama cha CUF, Maalim Seif, aliendelea kusema kuwa chama cha CUF ni chama cha siasa kama vilivyo vyama vingine, na wala hakina udini. Alieleza kuwa kwa mujibu wa sheria za nchi, vyama vya kisiasa vinatakiwa viwe vya kitaifa, si vya kikabila wala kidini. Na CUF imetimiza shuruti zote hizo, ndiyo ikapata usajili wa kudumu. Kama chama hicho kina udini, mbona Msajili wa vyama vya siasa amenyamaza kimya, hakuchukua hatua yoyote? Huo ni ushahidi tosha kuwa Msajili anaridhika kuwa CUF ni chama cha siasa, na hakina udini. Ama kuhusu Waislamu wengi kujiunga na CUF, Maalim Seif aliuliza kuna dhambi gani kwao kufanya hivyo? Alisema Waislamu wa Tanzania ni raia kama walivyo raia wengine, kwa hivyo wana haki na uhuru wa kujiunga na chama cho chote wanachokitaka! Kwa kweli madai ya kwamba CUF ni chama chenye udini ni uzushi uliopandikizwa na wapinzani wa chama hicho. Ni madai yasiyokuwa na chembe na ukweli ndani yake. Lakini kwa vile yamekuwa yakikaririwa, mara kwa mara na viongozi wa chama cha CCM na kutangazwa na vyombo vya habari, basi yanaonekana kama yamekubalika. Ndiyo maana hata yule mwulizaji, badala ya kutumia fursa aliyopewa kuuliza swali, yeye akapandwa na jazba na kutawaliwa na chuki, akatoa shutuma za udini dhidi ya chama cha CUF. Mtu huyo bila ya kufanya uchunguzi kuthibitisha madai hayo ya udini dhidi ya chama hicho, yeye alikuwa tayari amekwishajenga dhana potofu kuwa chama cha CUF kina udini. Alikubali kuamini uvumi! Ni hadithi ile ile ya Popo Bawa! Madamu kila mtu alikuwa akizungumzia juu ya Popo Bawa, watu wengi, bila ya kujijua wakajikuta wakiamini kuwa kweli kulikuwapo na Popo Bawa. Ilichukua muda mkubwa ndiyo wakaja kung'amua kuwa ule ulikuwa ni uvumi tu. Hakukuwapo na Popo Bawa wala Popo Unyoya! Basi na hizi shutuma za sasa kwamba eti CUF ni chama cha udini ndiyo maana kikaungwa mkono na Waislamu wengi, hazitofautiani na ule uvumi wa kuwepo kwa Popo Bawa. Shutuma zinazotokana na ile ile sera ya Gobbels ya kwamba ukitaka jambo likubalike lirejee kulitangaza mara kwa mara. CCM ilianza kutoa shutuma kuwa CUF ni chama cha udini; vyombo vya habari vikatangaza na kukariri, basi watu wakaamini! Lakini safari hii likawageukia walewale walizozianzisha shutuma hizo. Tokea chama cha CUF kianzishwe nguvu zake kubwa zilikuwa zipo Visiwani Zanzibar, na hasa katika Kisiwa cha Pemba. Huku Bara chama hicho kilikuwa hakina nguvu na kwa kweli kilikuwa hakina wafuasi. Ikasemwa kuwa chama hicho ni cha Wapemba. Vyombo vya habari vikawa vinatangaza hivyo na watu wengi wa huku Bara wakaamini hivyo. Nini basi kilichosababisha chama hicho kikubalike huku Bara? Ni ile ile propaganda ya Gobbels. Kwa siku nyingi Waislamu wa Bara wamejenga hisia kuwa wanapunjwa katika elimu na ajira pamoja na nafasi za uongozi katika serikali. Na kweli wanafunzi wa Kiislamu wanaopata nafasi ya kuingia shule za sekondari imekuwa siku zote ni baina ya asilimia 20 na 30. Na wale wanaopata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu haizidi asilimia 20. Katika nafasi za uongozi serikalini na mashirika ya umma mambo ni mabaya zaidi. Waislamu wakilalamika wanaambiwa hakuna udini. Viongozi wa Kiislamu wanaojitokeza kuonesha kasoro hizo, pamoja na kudai haki, wamekuwa wakiandamwa na vyombo vya dola na mara nyingine hupewa mkong'oto. Wamekuwa wakipachikwa kila aina ya majina. Mara waitwe, "wenye siasa kali", mara "Mujahidiana", mara "wachochezi" wanaotaka kuhatarisha amani! Ilipotokea kadhia ya MwembeChai ikatangazwa kuwa fujo zile zilitokana na fujo zilizoanzishwa na Waislamu wenye siasa kali. Waislamu wasiopungua wawili wakauawa kwa kupigwa risasi na Polisi, na mwanafuzi mmoja wa shule ya Al-Haramain, Chuki Athumani akapigwa risasi na kupata ulemavu wa kudumu! Waislamu wakaomba ufanywe uchunguzi wa kisheria kutafuta chanzo cha fujo zile; serikali kwa upande wake, ikakataa na kusema hakukuwa na haja ya kufanya uchunguzi juu ya kadhia hiyo. Na hata Waislamu walipoomba ifanywe "INQUEST" kuchunguza vifo vya wale Waislamu waliouawa katika kadhia ile ya Mwembe Chai serikali ilikataa! Na kumbe kwa mujibu wa seria za nchi kifo chochote kinachotokea mikononi mwa Polisi au Magereza kinabidi kifanyiwe uchunguzi wa kisheria (INQUEST). Kuona hivyo, Waislamu wa Bara wakajenga hisia kuwa serikali inayoongozwa na CCM haiwatendei haki Waislamu. Waliposikia kuna chama kinatangaza kuwa sera yake ni HAKI SAWA KWA WOTE, wakaona wajiunge na chama hicho. Nacho ndicho hicho chama cha CUF. Viongozi wa CCM walipoona Waislamu wengi wanakihama chama chao cha CCM na kujiunga na CUF ndiyo wakaanza kukipakazia kuwa chama hicho kina udini. Eti ni chama cha Waislamu. Na vyombo vya habari navyo vikaubeba ujumbe huo na kuanza kuutangaza kwa mapana na marefu! Ikiwa ni hadithi ile ileya Popo Bawa. Ulianza uvumi mwisho watu wakaamini. Basi na hili la udini wa CUF ni uvumi ulioanzsishwa kwa lengo la kuwaogopesha watu wasijiunge na chama hicho; lakini kwa vile Waislamu wanahisi CCM inawapunja na haitaki kuwasikiliza malalamiko yao, na kwamba CCM hiyo hiyo inawatangazia kuwa CUF ni chama cha Waislamu basi ndiyo Waislamu wengi wakaona wakiunge mkono chama hicho. Lakini hata kama chama cha CUF kitaungwa mkono na Waislamu wengi kuna dhambi gani, kama alivyouliza Maalim Seif? Hao Waislamu wote waliojiunga na CUF asili yake wametokea huko huko CCM. Mbona wakati huo haikusemwa kwamba CCM kilikuwa na udini? |
YALIYOMO
KAULI
YA WAISLAMU
Karume adaiwa ‘kutafuta ujiko’ kwa kutofautiana na Mkapa Mkapa akiuka sera yake-Chuo Kikuu Uandikishaji wapiga kura waanza CUF yataja wagombea wake Temeke CCM yamtuhumu Mwenyekiti wake pandikizi Propaganda ya Udini itaisambaratisha nchi - CHADEMA USHAURI NASAHA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
Je, unajua haki yako unapokamatwa na polisi? LISHE
|
|
|
|
|