|
Na. 060 Jumatano Agosti 9 - 15, 2000 |
|
|
|
|
|
Lengo la propaganda PROPAGANDA ni uenezi wa nadharia fulani katika
jamii. Na kwa kawaida inakuwa na sura mbili moja ni uhalisi na pili kupotosha
itikadi inayopingana na hiyo unayoeneza.Kisiasa propaganda lazima ieneze
itikadi yako kwa uhalisi wake ili kuwavuta watu waipende na pia kupotosha
itikadi pinzani ili ichukiwe. Lakini lengo la propaganda hii ya udini lipo
katika sura ya kupotosha tu (kulaghai na kudanganya). Katiba 13(1)inatoa
haki ya usawa wa watu kisheria,hivyo uamuzi wa mtu kufuata chama chochote
ni wa mtu binafsi na huwezi kulaumu wingi au uchache wa wafuasi wa dini
fulani katika chama fulani. NA ABU KAWTHARA ANAENDELEA...
KWA mfano mwenyekiti wa CCM akiongea na wazazi alidai sera ya haki sawa kwa wote ni dhana potofu. Kikatiba hiyo ni haki yake kulingana18(1) inatoa haki ya maoni kama raia. Kikatiba dhana yoyote isiyovuka mipaka ya katiba ni sahihi na hapa tukumbuke kuwa kauli hiyo ilitolewa kisiasa na mwanasiasa kwa wafuasi wake kisiasa wala asingethubutu kuitoa kiserikali ingekuwa ni kuvunja katiba. Kwa kawaida propaganda yoyote ya kupotosha hufa pale tu muda unapokwisha na lengo lake kutimia. Mfano ni ile ya ukabila dhidi ya NCCR mwaka 1995 ambayo ilikufa baada ya kushindwa uchaguzi na hatimaye kugawanyika kwa chama hali iliyopelekea kupoteza hadhi yake ya kisiasa. Kwa sasa propaganda yoyote inalenga katika uchaguzi mkuu baada tu ya uchaguzi kama CCM itashinda basi ndiyo mwisho wa propaganda ,ila juhudi zitafanyika kukihujumu na hatimae kukisambatatisha chama tuhumiwa kama ilivyokuwa kwa NCCR.Lakini kama CCM itashindwa basi propaganda haitokoma mpaka ushindani mwingine. Wakati wa awamu ya pili Wakristo walimlaumu sana Mwinyi kuwa ni mdini lakini wakati wa awamu wa ya kwaza Waislamu hawakumlaumu Mwl. Nyerere kwa udini naye aliwasifia sana kwa msaada waliompa wao wengi yeye peke yake ingawa alipata kutoa matamshi ya kidini kama vile:- - mimi ni mlei lakini nataraji kulipatia kanisa fursa nzuri ili nisilaumiwe kama mkatoliki na ukatoliki usilaumiwe katika Tanzania. - Nitahakikisha sera ya ujamaa haipingani na Ukristo na nimewaweka mapadre wawili katika baraza la mawaziri na mmoja kuongoza idara ya siasa ya chama ili kufanikisha hayo. (rejea dini na maendeleo katika Tanzania). Kikatiba kama ahadi ingekuwa ni kutoa fursa nzuri kwa Waislamu na Wakristo ni kitu halali haki ikielemea upande mmoja sio halali kikatiba. Hapa tunapaswa kujua kuwa propaganda ni michezo maalum kisiasa na mtego mkubwa na ni kawaida kuwepo propaganda katika ushindani wowote ule. Kama kuna makundi mawili yanashindana basi lazima baadhi ya vitu vifanyike. i) propaganda (maandalizi ya kisaikolojia) yenye lengo la kuupa matumaini upande wako na kuunyima utulivu upande pinzani. Mfano nitamuuwa mpinzani wangu raundi ya nne, tutawafunga magoli kumi, nitakupiga hata kama nimetoka usingizini, mwenzangu anatumia madawa ya kuongeza nguvu, mwenzangu ni mdini n.k. ii) mazoezi ya viungo kuwafanya watu wawe tayari iii) mfumo wa ushindani kama 4:4:2 au sera kisiasa iv) mbinu za kichezaji (taticks, technics) kama hadaa za kisiasa v) uhamasishaji wa washangiliaji au wapiga kura katika siasa Kivita pia unatoa hadaa mbalimbali ambazo zinalenga kumfitinisha mpinzani wako na washirika na marafiki zake. Kama kudai huyu ni muuaji, mtesi wa watoto na kinamama, mdini, jasusi n.k. hii inafanya akose msaada wa watu walio nje ya uwanja wa mapambano. Kama itikadi yako inapotoshwa basi utajikuta unashughulishwa usiende mbele ubakie (katika mtego wa buibui)unacheza katika kutoa majibu yale yale na kumwacha mpinzani wako akiwa likizo na aweze kupanga mipango ya kwenda mbele. Kilicho bora ni kukwepa mtego wa kushughulishwa na kutafuta mbinu ya wakati unasafisha njia yako pia unamwekea miiba mwenzio. Unatoa udhaifu wa mpinzani katika namna inayomgusa kila mtu na kuacha athari ya kuendelea huku yeye akitoa dhana ambayo ni madai tu yanayo pingana na ushahidi. Ukichukulia uduni wa hali za watu wa kawaida,mtego wa udini unawanasa wachache sana kuliko mguso wa watu unaonyeshwa na sera za CUF. Tukirudi katika katiba 12(1,2) -uhuru, usawa kuthaminiwa utu wa kila mtu, au 15((1) haki ya kuwa huru, au 14 haki ya kuishi, 17(1) uhuru wa kuishi popote, 16(1) hifadhi ya nafsi. Vipengele vyote hivyo havimzuii mtu kujipamba na vazi lolote. Viongozi Wakristu wa kitaifa huvaa mavazi ya Kiislamu kama ishara ya kuungana nao, kutoa salaam za kidini katika hadhara za kisiasa, kusoma dua za kidini katika hadhara za kisiasa. N.K. Mfano katika kila mkutano wa kisiasa sasa mwenyekiti wa CCM analazimika kutoa salaam maalum ya Kiislamu na pia kwa vijana kwa Asalaam alaykum na Mambo! Ili kurudisha imani ya makundi hayo kwake japo keshachelewa sana kutokana na kuhamwa na makundi hayo na sasa limeanza la wazee baada ya kinamama. Wakati wa bajeti ilibidi waziri wa fedha aanze kwa bismillah ikitanguliwa na Asalaam alaykum ili kuwafariji Waislam waliokubali siku ya kusheherekea maulid iwe ni bajeti. Nina hakika kuwa kwa dharura yoyote iwayo Wakristu hawawezi kuthubutu kukubali bajeti isomwe wakati wa siku kuu ya Christmas itapigwa kelele kwamba kiwewe cha sherehe kitafanya wabunge na watu wasifuatilie vema hotuba ya bajeti ya serikali; Ajabu ya Mungu hakuna chombo chochote cha Kiislamu kilicholaumu juu ya uamuzi huo wa serikali, hata ilipoamriwa watoto wa Kiislamu wafanye mitihani wakati wa Eid -el-Fitri hakuna aliejali ingawa mwaka uliopita matokeo ya mitihani ya shule za msingi yaliahirishwa kutangazwa ili kutoathiri wanafunzi Wakristu kusherehekea Christmas. Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa ilibidi uanze saa tano ili kuwapa nafasi waumini kwenda makanisani. Kwa hiyo Waislamu hawaendekezi udini kwa serikali kama inavyofanya kwao mfano:- a) kutotoa nafasi huru ya kushiriki ibada ya Ijumaa. Nafasi ambayo ni lazima iwe rasmi yaani hakuna kazi ofisi zote zifungwe tuseme saa sita ndio mwisho wa kazi kwa Ijumaa na masaa yaliyoathirika kutawanywa katika siku zingine. b) Wakati wenzao Wakristu wanapata siku mbili kamili za kupumzika yaani Jumamosi na Jumapili iwapo nchini kuna dini kuu mbili yaani Uislamu na Ukristu kwa nini za mapumziko zisiwe Ijumaa na Jumapili? Au Ijumaa na Jumamosi? Kwa uwakilishi wa makundi ya dini kuu? c) Wakati madai ya Waislamu hayashughulikiwi kwa kutowaudhi Wakristu yale ya Wakristu hushughulikiwa hata kama ni kwa kuwaudhi Waislam d) Ratiba ya taarifa za habari za vyombo vyote vya umma na vya binafsi zinaingiliana na vipindi vya sala kwa Waislam na sio kinyume chake. Sala kwa Waislamu imewekewa wakati maalum hivyo utachagua kati ya Mungu na taarifa na hii inakiuka haki ya kuwapa raia wote habari. e) Ijumaa vikao vya bunge huendelea wakati vinaahirishwa Jumamosi na Jumapili f) Upendeleo katika kupanga idadi ya siku za kupumzika. Mfano mwaka mpya,pasaka (siku nne), Christmas (sikumbili) jumla siku saba kwa Wakristu. Lakini kwa upande wa Waislamu siku za kupumzika ni nne tu yaani Eid-el-Fitr (siku mbili), Eid-el Hajj, na maulid wakati mwaka mpya si siku ya mapumziko. g) Msajili wa vyama kuamua kukutana na baraza la maaskofu kuwapa taarifa juu ya maandalizi ya uchaguzi hili iliyopelekea kuangua kilio kwa kupinga tuhuma za upendelo lakini bila kuona umuhimu wa kuzungumza na masheikh. h) Bodi nyingi kukutana siku za Ijumaa bila kujali kuwa wajumbe wengine ni Waislam i) Kutoteua viongozi kulingana na uwiano wa wananchi na makundi mbalimbali nchini mfano kazi ya kusimamia uchaguzi haihitaji utaalam maalum lakini zaidi ya asilimia 90 ya wasimamizi wakuu na wale wasaidizi ni wa imani moja tu. j) Serikali bila kuwa na sheria rasmi imefanya sherehe za Kikristu zipambwe katika maofisi yote kwa gharama za watu wote huku zile za Kiislam hazipati umuhimu kama huo. Kwa hiyo katiba inatoa uhuru kamili wa kuabudu na mtu anaweza kuabudu dini yake wakati wowote, mahali popote, na kwa namna yeyote ili mradi havunji sheria ndio maana mbali na nyumba za ibada, sehemu za wazi, mashule na hata kumbi za mikutano hutumika kwa ibada na ikumbukwe Muislamu hutakiwa kusalia ale muda wa sala ulipomkuta. Kudhania mavazi ni kielelezo rasmi cha imani ya mtu ni upotoshaji mkubwa sana. Mfano kila mvaa kanzu, kofia, hijabu si lazima awe mwislamu japo sheria haimchaguilii mtu mavazi. Mfano Mkristu akivaa kanzu au kofia hilo tu halibadilishi imani yake wala mwislamu kuvaa vazi la Kiislam haimuondolei imani yake. Mavazi hutumika kama utamaduni wa watu au matukio au kielelezo cha imani. Chukulia mfano wa nchi zote za Afrika magharibi watu wote huvaa mavazi yanayofanana Waislam na Wakristu. Zanzibar au Uarabuni ni hivyo hivyo. Mikoa ya pwani kadhalika. Napenda kuhitimisha nukta hii kuwa propaganda ya kisiasa ni mbinu ya ushindi na likitimia lengo lake na kwisha muda wake basi itakufa kifo cha kawaida. Mfano tukio la mashule yote nchini kugaiwa biblia bila kujali imani ya wanafunzi, kushiriki michango ya makanisa au misikiti,kusikiliza mahubiri ya nyumba kwa nyumba ya walokole, kuchangisha michango ya madrasa mabarabara ni ni vitu vya kawaida nchini vinavyothibitisha kutokuwepo fitna baina ya waumini Waislamu na Wakristu. Tatizo lipo katika fitna inayoundwa na CCM na serikali yake. Mfano akihutubia mkutano mkuu maalum wa CCM Dodoma mapema mwezi huu Mwenyekiti wake na mgombea wa chama hicho alithibitisha kuwa hakuna chama chochote chenye itikadi au sera ya kidini katika katiba yake ili kuthibitisha kuwa kina Udini lakini baadhi ya kauli za kidini (kutoka vitabu vya kidini zinazotumiwa kisiasa) ndio zinaonyesha ni vyama vyenye udini. Kauli pekee iliyotokea kuonekana ni ya kitisho ni ile ya'JINO KWA JINO' kauli ambayo ni tukufu kutoka kwa Mungu ikiwa katika Taurati na Qur'an tukufu vitabu vinavyotumiwa kwa kutolea viapo vya viongozi wa kisiasa. Yusuf Makamaba hutumia kauli nyingi kutoka katika biblia na Bwana Mrema hutumia kauli kutoka katika msahafu wakati kauli ya jino kwa jino inatokana na vitabu vyote na ni kauli ya kisiasa tu. Mbona Mkapa asemapo atahakikisha anashinda kwa gharama yoyote haionekani ni kitisho?, je kama gharama hiyo ni kuua utasemaje?. Hizi ni kauli za kisiasa tu na sio za kumshughulisha mtu. Mwl Nyerere aliwahi kusema asingeweza kwenda kulala Butiama na kuacha nchi itawaliwe na mbwa, je kauli hii si ya kitisho?. Kauli zote zitumikazo kisiasa zinatakiwa kutafsiriwa kisiasa tu na si vinginevyo. Ndugu Mugabe amedai kuwaachia nchi wapinzani ni kuwaachia mashetani watawale je wapinzani ni kweli mashetani?. Ikumbukwe kuwa vijembe na kauli kama hizi huwa ni za kisiasa tu na mara nyingi husababishwa na dhulma na ukandamizaji katika jamii. Hebu chukulia kauli za viongozi wa CCM kama ile ya shavu kwa shavu au zile za Malecela, Kapinga na Nchimbi dhidi ya wale waliotarajia kumpinga Mkapa sio za vitisho? Binafsi natishwa sana na ile ya rais kuhakikisha yeye na mgombea wa Zanzibar na chama chake vinashinda kwa gharama yoyote huku akiwa ndie Rais na amiri jeshi mkuu na mkuu wa nchi ama kweli nyani haoni kundule. Pamoja na CCM Kutumia vyombo vyote vya habari kutoa propaganda na vitisho nakupotosha habari za wapinzani,kutumia dola kutisha watu, kutumia bunge kupitisha sheria za kuipendelea, kutisha wafanyabiashara, kuzuia wenye mahoteli na kumbi kuwapa nafasi wapinzani kufanyia mikutano yao kama ilivyokuwa kwa CUF Mwanza kulazimisha wajumbe kufanya mkutano nje, kunyimwa mahoteli kuwasilisha mswada wa masanduku ya kura kutofungwa na baada ya kura yahamishwe na wasimamizi na kwenda kuhesabia popote hata kama ni nyumbani kwake na mengi mengine, upinzani umepata nguvu ya ajabu na kuwatia kiwewe kikubwa. Kwa hakika nguvu ya upinzani dhidi CCM inatisha Wananchi lazima wapuuze propaganda zote na kuleta mabadiliko ya kidemokrasia kwani sasa CCM haina mvuto kwa watu tena.Kilichobaki ni kutisha watu kwa kila aina ya propaganda kupitia vipindi mbalimbali vya vyombo vya habari vya kitaifa na vyombo vya dola.Lakini juu ya yote hayo maneno tu sio suluhisho la matatizo ya Watanzania ila mabadiliko ni limekuwa kimbilio la na faraja pekee inayoweza kunusuru nchi. Kama imefikia mahala hali ya maisha imekuwa ngumu kuliko wakati wowote katika historia ya nchi hii, watu kukosa uhakika wa maisha yao, kuishi kwa mlo mmoja tu kwa siku, bei za vitu ziko juu kuliko uwezo wa watu kununua, ajira ni tatizo sugu, matibabu duni, vitendo vya kukata tamaa kuongezeka (kama utumiaji wa madawaya kulevya utupaji wa watoto, watu kushindwa hata kumudu gharama za daladala n.k), kushuka kwa wastani wa umri wa Mtanzania, watu kutumia migomba kama sanda kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari, wagonjwa kulala mzungu wa nne, kulundikana mahabusu na wafungwa kwa ukosefu wa karatasi. Wakati yote haya yakimwelemea raia fukara; serikali inatanua, wabunge wanapuuza vikao kwa hofu ya kupoteza majimbo, TOT kupewa roli la kifahari kwa kampeni tu, kubainika kwa hujuma ya ulegezaji masharti ya kibishara (maarufu kwa soko huria katika nyanja kama nishati, fedha na mawasiliano), kutengwa kwa asilimia 47 ya matumizi ya serikali mwaka huu kwa utawala na majeshi tu wakati kilimo na viwanda kama vyanzo vya uzalishaji havikupatiwa kipaumbele. Imefika mahali tuseme imetosha sasa kama ni shati limekwisha choka bora kuvaa lingine sasa. Ikumbukwe kuwa chimbuko la mapinduzi ya kijamaa sehemu zote duniani lililotokana na tishio la pengo kubwa kati ya matajiri na makabwera hali iliyodhahiri sasa hapa nchini. Sasa tuna nchi iliyo kama bomu litakalolipuka wakati wowote. Viongozi wasichaguliwe kishabiki ila kwa kuangalia nani ataleta mabadiliko yanayokusudiwa. Ahsanteni sana. |
YALIYOMO
KAULI
YA WAISLAMU
Karume adaiwa ‘kutafuta ujiko’ kwa kutofautiana na Mkapa Mkapa akiuka sera yake-Chuo Kikuu Uandikishaji wapiga kura waanza CUF yataja wagombea wake Temeke CCM yamtuhumu Mwenyekiti wake pandikizi Propaganda ya Udini itaisambaratisha nchi - CHADEMA USHAURI NASAHA
MAKALA
MIPASHO NASAHA
MAKALA
KALAMU YA MWANDISHI
Je, unajua haki yako unapokamatwa na polisi? LISHE
|
|
|
|
|