Je, unajua haki yako unapokamatwa
na polisi?
-
Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe
kwako.
-
Mwulize jina lake
-
Mwulize namba yake ya uaskari
-
Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa
mashaka ama kukamatwa.
-
Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama
sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya
Kuzuia Rushwa.
-
Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati
akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
-
Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo
cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
-
Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa
wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi
mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
-
Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo
cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
-
Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi
yake.
-
Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu
vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi
ya Kuzuia Rushwa.
-
Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na
polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na
vile vile kwa mwanamume.
-
Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika
muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
|
YALIYOMO
KAULI
YA WAISLAMU
BAKWATA na Kanisa
Karume
adaiwa ‘kutafuta ujiko’ kwa kutofautiana na Mkapa
Mkapa
akiuka sera yake-Chuo Kikuu
Uandikishaji
wapiga kura waanza
NLD,
NRA, PONA vyamruka Mrema
CUF
yataja wagombea wake Temeke
CCM
yamtuhumu Mwenyekiti wake pandikizi
Propaganda
ya Udini itaisambaratisha nchi - CHADEMA
USHAURI NASAHA
Kumsaidia
mtoto aweze kujitegemea
MAKALA
Lengo
la propaganda
MIPASHO NASAHA
NJOZI!
NJOZI!
MAKALA
Tujihadhari
na risasi za sukari
KALAMU YA MWANDISHI
Popo
Bawa la kisiasa
Je,
unajua haki yako unapokamatwa na polisi?
Habari
za Kimataifa
LISHE
Ulaji
wa matunda
MASHAIRI
MICHEZO
Baada ya kuitumia kuigaragaza
Simba: Shungu akiri ‘ngangari' ni kiboko
Manga azikwa Moro
•••Dewji ahusishwa na kifo cha
mnyama Simba
Lunyamila, Kayoza waongoza kwa
mabao
|