AN-NUUR 
Na.181 Ramadhan 1419, Desemba 25 - 31, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Waislamu Tunduma waswali ndani ya kilabu cha ulanzi  

BAADHI ya waumini wa Msikiti wa Ijumaa Tunduma wameamua kuhamishia darsa lao amoja na kuswali ndani ya jengo lililokuwa baa maarufu mjini hapa. 

Hatua hiyo imekuja baada ya kutokea kutokuelewana baina ya makundi mawili pinzani. Waliohama na kukodi jengo lililokuwa baa mashuhuri kwa jina la ‘Kilimanjaro Bar’ ni waumini wote waliokuwa wanahudhuria darsa iliyokuwa ikiendeshwa Msikitini hapo na Ustadh Nassoro Abdallah. 

Imedaiwa kwamba Sheikh huyo wa Wilaya wa Bakwata Sheikh Abdallah Mwapyate hakubaliani na utaratibu wa kutumia fedha za Msikti kuendeshea madrasa ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara ya waalimu. 

Kutokana na mgongano uliopo kati ya Kamati ya Msikiti na Sheikh wa Wilaya, Kamati iliamua kujiuzulu na wakati huo huo Sheikh akateua Imam mwingine kinyume na yule aliyewekwa na waumini. 

Hali hiyo ilizaa jamaa mbili ndani ya Msikiti ambapo Sheikh alichukua hatua ya kulisimamisha darsa hadi baada ya Ramadhani. 

Waumini waliohama Msikiti wamedai kwamba wamekuwa wakipachikwa majina kama "wenye itikadi kali" kwa lengo la kuwafitini kwa serikali na jamii inayowazunguka. 

Wamesema kwamba ili kuepusha shari wataswalia kwenye jengo hilo la baa kwa muda huku wakifanya juhudi za kujenga Msikiti wao. 

Kwa upande wa Sheikh wa Wilaya imeelezwa kwamba yeye hakutaka fedha za Msikiti zitumike kuendesha madrasa bali wazazi wachange. 

Aidha, imeelezwa kwamba Sheikh ana mpango wa kuleta waalimu wengine kutoka Tanga kwa madai kwamba aliyeko ambaye ni Ustadh Nassoro hajulikani ametokea wapi na amesomeshwa na nani. 

Madrasa hiyo yenye wanafunzi 35 watu wazima wanaume, 42 wanawake na watoto 100 ilifungwa hivi karibuni na Sheikh wa Bakwata wa Wilaya kwa visingizio mbalimbali. 

 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Hakuna Idd kwa wanafunzi Waislamu mwaka huu 

Baada ya wanafunzi Wakristo kusherehekea Krismasi: Wanafunzi Waislamu kuikosa  Id el Fitr 

Hoi hoi zatawala ziara ya Mwinyi Mwanza 

Waislamu Tunduma waswali ndani ya kilabu cha ulanzi  

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: FROTTEURISM 

Barabara za Tabora zimepitwa na wakati 

Jicho la Uzalendo: Nihiari yetu kuendelea kujidanganya! 
Na Sompo wa Kahambwe 

Kuanza na kwisha mwezi wa Ramadhani 

Taarifa ya Kamati  juu ya yaliyotokea Mwembechai 

Hotuba ya Mwenyekiti wa Wanawake wa Kiislamu katika Kongamano lililofanyika Masjid Nnuur Sinza  19/12/1998 

Maazimio ya kongamano la wanawake wa Kiislamu 

Waislamu kijijini Kidunda Moro wahitaji mwalimu 

Waislamu Mtwara wadai jengo la Wakfu kwa CCM 

Wakati Makanisa yakimeremeta: Msikiti wageuka gofu Sanya Juu 

Sheikh Khalifa Suleiman afariki dunia 

Sheikh wa wilaya ya Lushoto afariki 

Ijue Madrasat Riyaadhwa ya mjini Dodoma 

Somo la Zaka 

Maiti ya Muislamu yasusiwa 

Mwinyi apongeza juhudi za kulea yatima Mwanza 

Tuhuma za kupindua uongozi wa Bakwata: Sheikh Hamim Boza akanusha kuhusika 

Kuongezeka kwa ajali za barabarani 

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache - 4 
Na Yasin Valerian Massawe 

Matajiri wahimizwa kutoa zaka 

Saggaf awataka watoto wahifadhi Qur'an 

Waislamu watakiwa kujitolea kupigania dini yao 

Kesi  nyingine Mwembechai yaahirishwa  

Sayansi na Teknolojia  
[Kuirekebisha Modem Yako]  

Masomo ya Dini ya Kiislamu  

Barua za Wasomaji  

Mashairi  

Chakula na lishe  
[Saumu na lishe ya mama mjamzito] 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita