AN-NUUR 
Na.181 Ramadhan 1419, Desemba 25 - 31, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Maiti ya Muislamu yasusiwa 
 
  • Yadaiwa alikuwa ‘tarkuswalat’
  • Sheikh asema asiyeswali asiswaliwe
  • Maiti yake yasafirishwa na baskeli kutoka hospitali
  • Azikwa na ‘masela’ wenzake
MAITI ya mkazi mmoja wa kijiji cha Makole kilichoko kata ya Kwafungo, tarafa ya Bwembwera wilaya ya Muheza alizikwa bila kusaliwa kama ilivyo kawaida ya Kiislamu baada ya Waislamu wa kijiji hicho wakiongozwa na Sheikh na tarafa hiyo, Sheikh Yahya Mohammed Kiduo kumsusia maiti huyo. 

Habari zilizopatikana kutoka kijiji hicho zimeeleza kuwa kususiwa kwa maiti hiyo kunatokana na marehemu kutojishughulisha na ibada yoyote katika uhai wake zaidi ya vitendo vya maasi. 

Imeelezwa kuwa marehemu huyo aliyetajwa kwa jina moja tu la Saidi alikuwa Muislamu aliyeachana na sala. Alifia katika hospitali teule iliyopo wilayani Muheza baada ya kuugua kwa muda mfupi na baada ya taarifa za kifo chake kusambazwa, Sheikh wa kijiji hicho ambaye pia ni Sheikh wa tarafa alidai kuwa hatamzika wala kumsalia kwa sababu marehemu alikuwa tarkuswalat (haswali). 

Kutokana na Waislamu wengi wa kijiji hicho kuweka msimamo wa kutomswalia wala kumzika mtu aliyekuwa haswali, maiti ya marehemu ilitekelekezwa hospitali kwa siku mbili na siku ya tatu yake inadaiwa ni vijana wa maskani waliokwenda kuichukua hospitali kwa kutumia baiskeli ambapo ilifungwa kwenye kiti cha nyuma na kusafirishwa hadi kijijini hapo. 

Walioshuhudia tukio hilo walieleza kuwa vijana hao ndio waliomuosha kijana mwenzao wakamvisha sanda na kwenda kumzika wanavyoweza bila kumsalia wala kumuombea dua yoyote ile. 

Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina la Bakari Ramadhani alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na tukio hilo alisema Waislamu wa kijiji hicho wameweka msimamo wa kutomsalia wala kumzika Muislamu yeyote anayejishughulisha na vitendo vya shirk au kukataa kuswali. 

Alisema marehemu Saidi alikuwa tarkuswalaat na aliingia siku moja tu kwenye Msikiti baada ya kuchukuliwa na vijana wa Answar Sunna ambao walikuwa wakiendesha Da’awa kijijini hapo. 



Mwinyi apongeza juhudi za kulea yatima Mwanza 

RAIS mstaafu Ali Hassan Mwinyi amewakumbusha Waislamu kwamba kutunza mayatima sio hiari bali ni amri kama zilivyo amri nyingine ndani ya maagizo ya Allah (s.w.). 

Akiongea na Waislamu waliohudhuria katika kituo cha mayatima cha Ilemela, Mwanza kinachoendeshwa na taasisi ya Ilemela Yatima Foundation alisema kuwa Mwenyezi Mungu ameahidi ujira na faida mbalimbali kwa anayejishughulisha na ulezi wa mayatima. 

Kabla ya kuzungumza hayo ndani ya jengo linalokusudiwa litakapokamilika kuwa mahali pa kulia chakula, mikutano, semina na shughuli mbalimbali zinazojumuisha watu wengi, alipata fursa ya kusali sala ya alasiri ndani ya Msikiti uliojengwa na Africa Muslims Agency na alitembezwa maeneo mbalimbali ili kujionea mazingira ya kituo hicho. 

Kabla ya kumkaribisha kuongea na Waislamu pamoja na yamatima wenyewe, watoto hao chini ya mwalimu wao ambaye ndiye mkuu wa kituo hicho Ustadh Nasib Issa, walionyesha mambo mbalimbali wafundishwayo hapo kituoni. 

Waliimba nyimbo zilizokuwa na ujumbe kwa kuwahimiza watu kuwajali watoto wenye matatizo mbalimbali, hasa mafunzo ya tabia njema kwa ujumla, waliigiza kwa lugha ya Kiarabu, Kiswahili na Kiingereza. 

Baadaye Mwenyekiti wa Bodi wa kituo hicho Sheikh Jabir Yusufu Katura alisoma historia ya kituo na kutoa shukrani za pekee kwa wafadhili mbalimbali waliojitokeza mara moja baada ya mfadhili mwanzilishi marehemu Bashiri Hussein Sherally kufariki kwa ajali ya ndege huko Kenya mwishoni mwa mwaka juzi. 

Mwenyekiti huyo alisema kuwa kituo kilianza Desemba 26, 1997 kikiwa na watoto 16, hivi sasa wako 26, alisema kituo kinatoa huduma za kulea, chakula, malazi, mavazi, matitabu ambapo kwa sasa hivi mtoto mmoja anagharimu shilingi 25,000 kwa mwezi. Sheikh Jabir aliomba wafadhili mbalimbali wajitokeze kwani kituo kinahitaji zaidi ya shilingi laki tisa kwa mwezi. 

Akiongea, Alhaj Mwinyi alisema kuwa mwanzo tayari umepatikana, sasa ni juu ya Waislamu wote kwa ujumla kuuendeleza mwanzo. Aliahidi yeye kupitia kwa marafiki zake kuchangia chochote watakachopata ili nao wapate fadhila za sadakat-jaria (sadaka yenye kudumu). Awali aliombwa kuwa mlezi wa kituo na alikubali bila ya pingamizi kwa kusema kuwa hilo ni jambo la kheri na hakuna awezaye kupinga. 

Wakati huo huo, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi amewataka Waislamu kuchukua hadhari kubwa kutokana na uharibifu mkubwa wa kimaadili unaofanywa na nchi za Ulaya. 

Amesema nchi hizo kupitia mtandao wa vyombo vya habari; wamekuwa wachafuzi wa maadili na mila za Kiislamu hivyo hapana budi kwa Waislamu kuwa na taratibu madhubuti za kukabiliana na uharibifu huo. 

Nasaha hizi Alhaj Mwinyi alizotoa wakati akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya shule ya Thaqafa kitengo cha Dini. 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Hakuna Idd kwa wanafunzi Waislamu mwaka huu 

Baada ya wanafunzi Wakristo kusherehekea Krismasi: Wanafunzi Waislamu kuikosa  Id el Fitr 

Hoi hoi zatawala ziara ya Mwinyi Mwanza 

Waislamu Tunduma waswali ndani ya kilabu cha ulanzi  

MARADHI YA KISAIKOLOJIA: FROTTEURISM 

Barabara za Tabora zimepitwa na wakati 

Jicho la Uzalendo: Nihiari yetu kuendelea kujidanganya! 
Na Sompo wa Kahambwe 

Kuanza na kwisha mwezi wa Ramadhani 

Taarifa ya Kamati  juu ya yaliyotokea Mwembechai 

Hotuba ya Mwenyekiti wa Wanawake wa Kiislamu katika Kongamano lililofanyika Masjid Nnuur Sinza  19/12/1998 

Maazimio ya kongamano la wanawake wa Kiislamu 

Waislamu kijijini Kidunda Moro wahitaji mwalimu 

Waislamu Mtwara wadai jengo la Wakfu kwa CCM 

Wakati Makanisa yakimeremeta: Msikiti wageuka gofu Sanya Juu 

Sheikh Khalifa Suleiman afariki dunia 

Sheikh wa wilaya ya Lushoto afariki 

Ijue Madrasat Riyaadhwa ya mjini Dodoma 

Somo la Zaka 

Maiti ya Muislamu yasusiwa 

Mwinyi apongeza juhudi za kulea yatima Mwanza 

Tuhuma za kupindua uongozi wa Bakwata: Sheikh Hamim Boza akanusha kuhusika 

Kuongezeka kwa ajali za barabarani 

Njia ya uzimani ni nyembamba,  waionao ni wachache - 4 
Na Yasin Valerian Massawe 

Matajiri wahimizwa kutoa zaka 

Saggaf awataka watoto wahifadhi Qur'an 

Waislamu watakiwa kujitolea kupigania dini yao 

Kesi  nyingine Mwembechai yaahirishwa  

Sayansi na Teknolojia  
[Kuirekebisha Modem Yako]  

Masomo ya Dini ya Kiislamu  

Barua za Wasomaji  

Mashairi  

Chakula na lishe  
[Saumu na lishe ya mama mjamzito] 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita