|
|
|
Sheikh Hamim Boza akanusha kuhusika MHUBIRI wa dini ya Kiislamu wa muda mrefu, Sheikh Hamim Boza amekanusha tuhuma za kuhusika na yaliyodaiwa mapinduzi ya kuuondoa uongozi wa juu wa Bakwata zilizopelekea baadhi ya Masheikh kuhojiwa na polisi Kituo cha Kati wiki mbili zilizopita. Sheikh Boza alisema kuwa yeye hajui wala hana mpango wowote wa kuivamia Bakwata na wala hakuwa na mawasiliano yoyote na baadhi ya Masheikh waliotajwa kwamba wanahusika katika uvamizi huo. Alisema kuwa yeye tangu Februari 7, mwaka huu alikuwa na ziara za vijiji vya mkoa wa Tanga. Alisema Novemba 19, mwaka huu ndipo alikanyaga katika ardhi ya Jiji la Dar es Salaam akitokea Mombasa ambako alikaa zaidi ya miezi mitatu. Hata hivyo, hakulala hapa Jijini bali alipitiliza moja kwa moja kwenda nyumbani kwa mzee wake Turiani. Aliongeza kwamba taarifa za kuipindua Bakwata alizohusishwa zilimkuta Turiani baada ya waumini wengi kusoma gazeti la AN-NUUR na kukuta jina lake. "Ni taarifa ambazo ziliwastua wengi wakiwemo Masheikh ambao muda wote nilishirikiana nao katika kufanya mihadhara na shughuli zingine za kimaisha", alisema Sheikh Boza. INASIKITISHA kusikia kila uchao watu wengi wanapoteza maisha yao kutokana na ajali za barabarani. Wiki na nenda kwa usalama barabarani ambayo huadhimishwa katika wiki ya tatu ya mwezi wa tisa kila mwaka, ilianzishwa mwaka 1977 Jijini Dar es Salaam na baadaye kuwa utaratibu kamili katika nchi nzima kwa lengo la kutoa maelimisho zaidi kwa wananchi kuhusu matumizi ya barabara ili kuepusha ajali ambazo kimsingi zinaweza kuepukika. Mwandishi Abdallah Ahmad Seif, Dodoma anachambua zaidi. Pamoja na maelimisho ambayo hutolewa kwa jamii na suala zima la usalama barabarani, lakini cha kusikitisha ajali zimekuwa zikizidi kuongezeka mwaka hadi mwaka na kupoteza maisha ya watu pamoja na uharibifu wa mali zao ajali ambazo huwa ndani ya uwezo wa kuepukika. Mara nyingi ajali zimekuwa zikitokea kutokana na uzembe wa madereva kuendesha magari kwa kasi na bila mpango, au kuendesha magari wakiwa wamelewa, ujuzi mdogo au kutojua kabisa kuendesha gari, kutojua sheria za barabarani, ubovu wa magari ikiwa ni pamoja na gari kukosa vitu muhimu kama vile breki, taa, honi, uchakavu wa matairi n.k. Kwa upande mwingine nao waenda kwa miguu wamekuwa wakichangia kwa sehemu kubwa kutokea kwa ajali hizo kwa sababu ya kutokua makini wakati wakiwa barabarani na hivyo kusababisha ajali ambazo chanzo chake kinakuwa ni uzembe. Lakini tukizidi kuchambua kiundani tunakuta ajali zinachangiwa na sehemu nyingine pia ikiwa ni pamoja na kikosi chenyewe cha usalama barabarani, hali kadhalika mahakama. Hii inakuja kutokana na tatizo sugu la rushwa ambalo kwa sasa limeota mizizi karibu katika kila sekta hapa nchini kwetu. Ni jambo lisilopingika kwamba kuna magari mengine mabovu yapo katika hali mbaya lakini utakuta yanatembea barabarani na hata kubeba abiria na huku yakipishana na wana usalama barabarani na hata itokeapo kukaguliwa na kuonekana na upungufu mkubwa usioruhusu yatembee barabarani lakini huendela kuchapa kazi na kwa kuwa magari hayo huwa na kasoro nyingi basi huwa haichukui muda kabla halijasababisha ajali na kugharimu miili na roho za watu. Gari isiyokuwa na breki, taa, honi, tairi zimechakaa, kwenda kwake mpaka isukumwe, gea yake hadi iwe inashikiliwa na "msaidizi wa dereva". Lazima tukubali gari ya namna hiyo haifai kwa matumizi ya binadamu. Lakini cha kushangaza "wakemia" (trafiki) hulithibitisha kwa matumizi ya binadamu na kwa kuwa ni bovu na halifai kwa matumizi basi huleta zahama kubwa ya ajali na kupoteza maisha ya watu. Uwepo wa magari hayo bila kuchukuliwa hatua unaonyesha wazi wenye magari hayo hutoa chochote kwa wana usalama barabarani na kupewa ‘ruksa’ ya kutembea. Vile vile utoaji wa leseni mara nyingine hauzingatii uwezo wa mtu kumudu udereva na hivyo kujikuta leseni zinatolewa kwa watu ambao hawajajua vilivyo kuendesha gari, hili nalo ni tatizo linalopelekea kutokea kwa ajali, hivyo ni juu ya usalama barabarani kuliangalia kwa makini suala hilo kwani kuna asilimia kubwa ya ajali nayo huchangiwa kutoka huko, na dhahiri kuna baadhi ya watendaji ambao si waaminifu huchukuwa rushwa na hivyo kuachia makosa yatawale, hivyo inabidi huko nako kuangaliwe na kudhibitiwe. Hali kadhalika mahakama nazo zimekuwa zikichangia kutokana na madereva wengi ambao hufikishwa mahakamani kwa makosa yaliyo wazi lakini huachiliwa katika mazingira ya kutatanisha au wakati mwingine kutolewa adhabu zisizolingana na makosa. Hapo suala la rushwa linatokeza na kudhihirisha athari yake katika jamii. Mtu anapoachiwa kutokana na makosa ya wazi anakuwa na kiburi cha kutojali taratibu za uendeshaji wa gari kwani hakuna popote anapoweza kuchukuliwa hatua, hivyo huendesha gari bila kujali waendao kwa miguu na hivyo kusababisha ajali. Hivyo suala la ongezeko la ajali
na jinsi ya kudhibiti ajali zitokanazo na uzembe, lazima liangaze katika
viini vyote, isiishie kuwahubiria waendao kwa miguu na madereva peke yao
bali wote ambao huchangia kwa namna moja au nyingine kutokea kwa ajali
hizo.
|
YALIYOMO
Tahariri Hakuna Idd kwa wanafunzi Waislamu mwaka huu Baada ya wanafunzi Wakristo kusherehekea Krismasi: Wanafunzi Waislamu kuikosa Id el Fitr Hoi hoi zatawala ziara ya Mwinyi Mwanza Waislamu Tunduma waswali ndani ya kilabu cha ulanzi MARADHI YA KISAIKOLOJIA: FROTTEURISM Barabara za Tabora zimepitwa na wakati Jicho la
Uzalendo: Nihiari yetu kuendelea kujidanganya!
Kuanza na kwisha mwezi wa Ramadhani Taarifa ya Kamati juu ya yaliyotokea Mwembechai Maazimio ya kongamano la wanawake wa Kiislamu Waislamu kijijini Kidunda Moro wahitaji mwalimu Waislamu Mtwara wadai jengo la Wakfu kwa CCM Wakati Makanisa yakimeremeta: Msikiti wageuka gofu Sanya Juu Sheikh Khalifa Suleiman afariki dunia Sheikh wa wilaya ya Lushoto afariki Ijue Madrasat Riyaadhwa ya mjini Dodoma Mwinyi apongeza juhudi za kulea yatima Mwanza Tuhuma za kupindua uongozi wa Bakwata: Sheikh Hamim Boza akanusha kuhusika Kuongezeka kwa ajali za barabarani Njia ya
uzimani ni nyembamba, waionao ni wachache - 4
Saggaf awataka watoto wahifadhi Qur'an Waislamu watakiwa kujitolea kupigania dini yao Kesi nyingine Mwembechai yaahirishwa Sayansi
na Teknolojia
Chakula
na lishe
|