AN-NUUR
Na.158 Rabi' Awal 1419, Julai 17 - 23, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 Mafundisho ya Qur'an
 
Kanuni za kumkumbuka Allah na kutumia katika njia yake

Kuna kanuni za jumla na kanuni maalum katika suala zito la kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Kanuni hizo zinatajwa na Aya zifuatazo. 

Mkumbukeni Mwenyezi Mungu msimamapo, mkaapo na (mlalapo) ubavu. Na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufaulu. (4:103) 

Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana zipo hoja (Ayat) kwa wenye akili. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa na wakilala. Na hufikiria umbo la mbingu na ardhi (kwa makini) husema: "Mola wetu hukuviumba hivi bure." 

Kuna Aya nyingi zaidi ya hizi ambazo zimeamriwa kuendelea kumkumbuka Mungu siku zote katika kila hali kwa sababu kumkumbuka Mungu ndiko kunakoyaweka matendo ya mtu katika njia iliyosahihi. 

Wakati wowote mtu awapo hamjali au hamkumbuki Mungu, haja za kimwili na matamanio yake humtawala, matokeo yake ni kwenda kinyume na kukiuka mipaka ya Njia iliyonyooka katika maisha yake. 

Kanuni Maalumu ya kumkumbuka Allah huonekana katika Swala ambayo ni mara tano kwa siku. Hii haina maana kuwa baada ya swala mtu yuko huru. La hasha wakati wote wa saa ishirini na nne unatakiwa umkumbuke Mwenyezi Mungu. 

Na hivi ndivyo ilivyo kwenye kutoa katika Njia ya Allah; kuna hukumu ya jumla na hukumu Maalumu. 

Kanuni za jumla kuhusu kutumia katika Njia ya Allah 

Upande mmoja inaamriwa: Jizuie na ubakhili na uchoyo kwa kuwa ni chanzo na ni mambo mabaya katika jamii. Katika vile ambavyo Mwenyezi Mungu ambae nyakati zote anawashushia viumbe wake ameamuru kutumia chochote awezacho mja katika njia yake. 

Weka akiba kiasi utachoweza kutokana na mahitaji yako na kutokana na akiba yako tosheleza mahitaji ya watumishi wengine wa Mungu ambao ni wahitaji. 

Kamwe usiache kujitolea maisha yako na mali yako katika kulitukuza neno la Mwenyezi Mungu na kuitumikia Dini Yake tu. Kama unampenda Mwenyezi Mungu basi toa pendo la mali kwa Mwenyezi Mungu. 

Hii ndio hukumu ya jumla ya kutoa katika njia ya Allah kama Aya zisemavyo: 

"Hamtaweza kuufikia wema khasa mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda; na chochote mnachokitoa, basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua." (3:92). 

"Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema, hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema". (2:195). 

"Shetani anakuogopesheni ufukara na anakuamrisheni ubakhili; na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha, utokao kwake na ihsani (kubwa pindi mkitoa); na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa mkubwa na Mwenye kujua." (2:268). 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI  

Maoni yetu: Wananchi kataeni kupotoshwa 

SUALA LA MWEMBECHAI: Wabunge wataka kujua nani aliamrisha kuua 
Na Mwandishi wetu  

Katiba ya nchi yapuuzwa: Waislamu wapigwa marufuku kuhubiri  

Mtihani darasa la saba 1998: Manispaa Moro yaagiza ipewe majina ya wanafunzi Wakatoliki 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

 “Wushu”ya Waislamu wa China na jinsi ilivyowasaidia kupambana na dhulma dhidi yao 
Na MUSSA ALLY  

Yesu wa kwenye Mathayo siyo Yesu wa kwenye Luka 
Na. Masoud Mohammed 

Ni nani hawa Waislamu wa Siasa Kali ? 
Na USTADH  A.S. FUNDI  

Waislamu tuondokane na unyonge 
Na Abubakar Marwilo 

Maisha ya ndoa kwa Mwislamu 

Waislamu wana mwelekeo wao 
Na Sheikh Pandukizi Dilunga 

Ni mwaka gani Yesu alianza kuitwa Mungu 
Na MCHUNGAJI A.T. MANONI  

Wanawake wameamua kuwa wazi kweli kweli 
Na Bi. Fatma Musa 

Kimya kingi kina mshindo mkuu: Vipi Mhe. Rais wale walioua? 
Na Mussa Ally 

Mtazamo wa madhalimu wa Tanzania kwa Waislamu 
Na Rajab Isa 

Aliyoyasema KK bungeni 

Waislamu mkoa wa Morogoro wampinga Yahya 
Na. Abu Adli  

Polisi wachafua mazingira ya msikiti wa Mwembechai 
Na Badru Kimwaga 

Wanawake wa Kiislamu Ubungo darajani wamuunga mkono Sheikh Bafadhil 
Na Kassim Juma 

Barua za wasomaji  

Mashairi  

Mafundisho ya Qur'an: Kanuni za kumkumbuka Allah na kutumia katika njia yake 

Masomo  

Chakula na lishe: Lishe ya mtoto aliyekuwa mgonjwa 
Na Mujahiid Mwinyimvua 
 

 

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita