AN-NUUR
Na.158 Rabi' Awal 1419, Julai 17 - 23, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
    Mtihani darasa la saba 1998:
    Manispaa Moro yaagiza ipewe majina ya wanafunzi Wakatoliki
  • Wazazi Waislamu wapigwa na bumbuwazi
  • Walimu wakuu watuhumiwa
Na Rajab Rajab, Morogoro 

WASI WASI mkubwa umeanza kuwaingia wazazi Waislamu wa mjini hapa kufuatia kupatikana kwa barua kutoka ofisi ya Elimu Manispaa inayowaagiza walimu wakuu wote wa shule za msingi kupeleka majina ya wanafunzi Wakatoliki wa darasa la saba wa mwaka huu. 

Mapema juzi baadhi ya Waislamu walionekana kupigwa na bumbuwazi 

baada ya kupata taarifa hizo na baadhi yao wakiwa wameiona nakala ya barua hiyo. 

Gazeti hili lilifanikiwa kuipata nakala ya barua hiyo ambayo imetiwa saini na mtu aitwaye E.P. Mpessa kwa niaba ya Afisa Eimu wa Manispaa ya Morogoro. 

Katika barua hiyo yenye kumbukumbu namba E.10/MMC-1/183 iliyoandikwa Juni 9 mwaka huu, inawataka walimu wakuu wote wa shule za msingi Manispaa ya Morogoro kutuma majina ya wanafunzi Wakatoliki darasa la saba hadi kufikia Juni 12, 1998. 

Barua hiyo fupi haikufafanua kiundani majina hayo ni ya nini jambo ambalo limewafanya Waislamu wa hapa kuanza kuwatilia mashaka walimu wakuu wa shule hizo kuwa wanafahamu suala hilo kiundani zaidi ndio maana Mwandishi hakulazimika kufafanua. 

Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya Waislamu wamedai kuwa vitu vya namna hiyo ndivyo vinavyowafanya waumini wa dini ya Kiislamu kuituhumu serikali kuwa inawapendelea Wakristo katika nyanja zote na hususan katika elimu. 

"Hali hii na mikakati kama hii viongozi wetu wa Kiislamu walio serikalini hawajui na wakipewa taarifa kama hii huwa hawaifanyii kazi badala yake wanawarushia Waislamu kashfa kwa kuwaambia hawana dira", alisema kwa uchungu muumini mmoja wa eneo la Kingo Bwana Ally Seifu. 

Naye Bw. Athman Salim wa Mafiga amesema "hata watoto wetu wasipochaguliwa kujiunga na shule za sekondari za serikali mwakani tutaamini kuwa imetokana na njama hizi." 

Kufuatia kupatikana waraka huo baadhi ya waumini wametishia kulipeleka suala hili mbele ya sheria (mahakamani) kwa madai kuwa linahatarisha hali ya baadaye ya vijana wao kimasomo. 

Aidha baadhi ya waumini hao wa Kiislamu wameiomba serikali kutopuuzia hali hii na kwamba ufanyike uchunguzi wa kina kwa kuunda tume huru vinginevyo huenda kukatokea mgawanyiko miongoni mwa raia wake. 

Mitihani ya Darasa la Saba inatarajiwa kufanyika nchi nzima mwezi Septemba mwaka huu. 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 
TAHARIRI  

Maoni yetu: Wananchi kataeni kupotoshwa 

SUALA LA MWEMBECHAI: Wabunge wataka kujua nani aliamrisha kuua 
Na Mwandishi wetu  

Katiba ya nchi yapuuzwa: Waislamu wapigwa marufuku kuhubiri  

Mtihani darasa la saba 1998: Manispaa Moro yaagiza ipewe majina ya wanafunzi Wakatoliki 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

 “Wushu”ya Waislamu wa China na jinsi ilivyowasaidia kupambana na dhulma dhidi yao 
Na MUSSA ALLY  

Yesu wa kwenye Mathayo siyo Yesu wa kwenye Luka 
Na. Masoud Mohammed 

Ni nani hawa Waislamu wa Siasa Kali ? 
Na USTADH  A.S. FUNDI  

Waislamu tuondokane na unyonge 
Na Abubakar Marwilo 

Maisha ya ndoa kwa Mwislamu 

Waislamu wana mwelekeo wao 
Na Sheikh Pandukizi Dilunga 

Ni mwaka gani Yesu alianza kuitwa Mungu 
Na MCHUNGAJI A.T. MANONI  

Wanawake wameamua kuwa wazi kweli kweli 
Na Bi. Fatma Musa 

Kimya kingi kina mshindo mkuu: Vipi Mhe. Rais wale walioua? 
Na Mussa Ally 

Mtazamo wa madhalimu wa Tanzania kwa Waislamu 
Na Rajab Isa 

Aliyoyasema KK bungeni 

Waislamu mkoa wa Morogoro wampinga Yahya 
Na. Abu Adli  

Polisi wachafua mazingira ya msikiti wa Mwembechai 
Na Badru Kimwaga 

Wanawake wa Kiislamu Ubungo darajani wamuunga mkono Sheikh Bafadhil 
Na Kassim Juma 

Barua za wasomaji  

Mashairi  

Mafundisho ya Qur'an: Kanuni za kumkumbuka Allah na kutumia katika njia yake 

Masomo  

Chakula na lishe: Lishe ya mtoto aliyekuwa mgonjwa 
Na Mujahiid Mwinyimvua 
 

 

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita