AN-NUUR
Na.158 Rabi' Awal 1419, Julai 17 - 23, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Yesu wa kwenye Mathayo siyo Yesu wa kwenye Luka

Na. Masoud Mohammed 

Barua iliyoandikwa na Ndugu Agustine Mwinuka katika gazeti la Msemakweli toleo Namba 018 la tarehe 5-11, Julai 1998 haiwezi kupita bila kuchangiwa. 

Mwandishi wa barua hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari Nabii Issa na Yesu kweli hawahusiani, amejitahidi kufanya uchambuzi japo siyo yakinifu na kuona kuwa kuna tofauti fulani juu ya sifa za Yesu kama zinavyoelezwa katika Biblia na sifa za Issa kama zinavyoelezwa katika Qur’ani tukufu. 

Ni kutokana na tofauti hizo ndiyo Ndugu Mwinuka anahitimisha kuwa Yesu wa kwenye Biblia siyo Issa wa kwenye Qur’ani." 

Pamoja na juhudi zote alizofanya, kwa bahati mbaya sana Ndugu Mwinuka alikosa uhuru wa mawazo na hivyo kuishia katika kutoa hitimisho nusu. Kama angelikuwa huru na mwaminifu kwa kuanza kuichunguza historia ya Yesu ndani ya Biblia yenyewe siyo ajabu kwamba kabla hajagundua kuwa Yesu wa kwenye Biblia siyo Issa wa kwenye Qur’ani, angegundua kwanza kwamba Yesu wa kwenye Mathayo siyo Yesu wa kwenye Luka. 

Ninasema hivyo kwa sababu ukoo wa Yesu wa kwenye Injili ya Mathayo unaanzia kwa Solomon, Roboam, Abia, Asa, Japhat…. Na kizazi cha 25 akiwa ni Jakobo aliyemzaa Yusufu aliyemzaa Yesu (Taz. Mathayo 1:1-18). Kwa upande mwingine ukoo wa Yesu wa Injili ya Luka ni mwingine kabisa ukiwa na majina tofauti na Yesu wa kwenye Mathayo. Ukoo huu unaanzia kwa Mathani, Mattatha, Menan…. Kizazi cha 40 kikiwa ni Heli aliyemzaa Yusufu aliyemzaa Yesu. (Taz. Lk. 3:23-31). Tofauti kubwa iliyopo kwa Mayesu hawa wawili ni kwamba yule wa kwenye Mathayo anatokana na ukoo tofauti kabisa na yule wa Luka. Ni jina moja tu la Yusufu linalopatikana kwa Mayesu hawa wawili na hata Mayusufu hawa wanaonekana kuwa tofauti. 

Wakati Yusufu wa kwenye Mathayo alizaliwa na Yakobo, Yusufu wa kwenye Luka alizaliwa na Heli. Hii ilikua ni hoja ya msingi kabisa kumfanya Bwana Mwinuka aamini kuwa Yesu wa kwenye Luka siyo wa kwenye Mathayo, lakinihilo hakuliona. 

Tofauti nyingine inahusiana na namna hawa Mayesu wawili walivyokufa. Yesu wa kwenye Mathayo neno lake la mwisho kutamka kabla hajakata roho ni Mungu wangu Mungu wangu mbonaumeniacha?" (Taz. Mathayo 27:45) wakatiYesu wa kwenye Luka neno lake la mwisho kutamka kabla ya kufa ni "Roho yangu naiweka mikononi mwako". Taz. (Lk.23:46). 

Hali kadhalika tukiangalia historia ya kufufuka na Mayesu hawa wawili ni rahisi kugundua kuwa walikuwa watu wawili tofauti. Kaburi la Yesu wa kwenye Mathayo lilitembelewa na wanawake,Mariamu Magdalena na Mariam wa pili siku ya kufufuka na kwamba wanawake hawa wawili walitokewa na malaika mmoja (Taz. Mathayo 28:1-8), kwa upande wa Yesu wa kwenye Luka yeye kaburi lake lilitembelewa na wanawake watatu ambao walitokewa na malaika wawili na siyo mmoja siku ya kufufuka (Tz.LK. 24:1-12) 

Ni kutokana na maelezo hayo juu ndiyo nimesita kumjibu Ndugu Mwinuka neno kwa neno ili kumpa nafasi aweke wazi zaidi misingi ya hoja yake. 

Haieleweki kama anataka kuonyesha kuwa kuna tofauti katika maelezo ya historia ya Yesu katika Biblia na katika Quraani na hivyo tuangalie ni ipi historia sahihi ya Yesu? Au anataka kumaanisha kuwa Jesus wa kwenye King James Version ni tofauti na Yesu wa Biblia ya Kiswahili? Na kama hivyo ndivyo la kwanza kufanya ilikuwa ni kutuonyesha ukoo wa Yesu na Issa na mengine yangefatia baadaye. 

Yote katika yote ningemuomba sana ndugu yangu Mwinuka afafanue juu ya hayo, na kama atakubaliana\ na maelezo hapo juu kuwa Yesu wa kwenye Mathayo si yule wa kwenye Luka, kwa mtizamo huo sitakuwa na sababu ya kung’ang’ania kwamba Yesu wa kwenye Luka ndiyo Isa wa kwenye Quraani. Kwani hata Qur-an haisemi kuwa Yesu ni Yesu kwa sababu yumo katika Biblia. Zaidi ya hapo ningependa ndugu huyu afafanue zaidi na hatimaye nipate nafasi ya kumpatia ushahidi wa kimaadiko (Qurani na Biblia), ushahidi wa kihistoria na ushahidi kutoka katika matamshi ya mapadri na wachungaji wake toka katika madhehebu mbalimbali wakishuhudia kuwa Yesu wa kwenye Quraani ndiye Yesu wa kwenye Biblia. 
 

Juu 
 

YALIYOMO
 
TAHARIRI  

Maoni yetu: Wananchi kataeni kupotoshwa 

SUALA LA MWEMBECHAI: Wabunge wataka kujua nani aliamrisha kuua 
Na Mwandishi wetu  

Katiba ya nchi yapuuzwa: Waislamu wapigwa marufuku kuhubiri  

Mtihani darasa la saba 1998: Manispaa Moro yaagiza ipewe majina ya wanafunzi Wakatoliki 
Na Rajab Rajab, Morogoro 

 “Wushu”ya Waislamu wa China na jinsi ilivyowasaidia kupambana na dhulma dhidi yao 
Na MUSSA ALLY  

Yesu wa kwenye Mathayo siyo Yesu wa kwenye Luka 
Na. Masoud Mohammed 

Ni nani hawa Waislamu wa Siasa Kali ? 
Na USTADH  A.S. FUNDI  

Waislamu tuondokane na unyonge 
Na Abubakar Marwilo 

Maisha ya ndoa kwa Mwislamu 

Waislamu wana mwelekeo wao 
Na Sheikh Pandukizi Dilunga 

Ni mwaka gani Yesu alianza kuitwa Mungu 
Na MCHUNGAJI A.T. MANONI  

Wanawake wameamua kuwa wazi kweli kweli 
Na Bi. Fatma Musa 

Kimya kingi kina mshindo mkuu: Vipi Mhe. Rais wale walioua? 
Na Mussa Ally 

Mtazamo wa madhalimu wa Tanzania kwa Waislamu 
Na Rajab Isa 

Aliyoyasema KK bungeni 

Waislamu mkoa wa Morogoro wampinga Yahya 
Na. Abu Adli  

Polisi wachafua mazingira ya msikiti wa Mwembechai 
Na Badru Kimwaga 

Wanawake wa Kiislamu Ubungo darajani wamuunga mkono Sheikh Bafadhil 
Na Kassim Juma 

Barua za wasomaji  

Mashairi  

Mafundisho ya Qur'an: Kanuni za kumkumbuka Allah na kutumia katika njia yake 

Masomo  

Chakula na lishe: Lishe ya mtoto aliyekuwa mgonjwa 
Na Mujahiid Mwinyimvua 
  

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita