|
|
.Katiba ya
nchi yapuuzwa:
HUKU serikali ikiendelea na madai yake kwamba haina chuki na Waislamu na kwamba haijazuia mahubiri ya dini, mjini Mwanza Kamanda wa Polisi Wilaya amepiga marufuku mahubiri hayo kinyume na katiba ya nchi. Kwa mujibu wa barua ya kamanda huyo kwa tawi la Almallid mjini Mwanza yenye kumbukumbu Na. MZA/B.3/24/Vol.1/235 ya Juni 3, 1998, mahubiri ya dini yamezuiliwa mjini humo kwa muda usiojulikana. Haikuelezwa sababu hasa za kuzuia mahubiri hayo, lakini taarifa zinafahamisha kwamba huenda huo ukawa ni mkakati wa jeshi hilo kufuta mihadhara inayodaiwa kuwa ni ya kashfa. Mihadhara hiyo ni pamoja na ile ya Waislamu ambayo hueleza kuwa Yesu si Mungu wala si Mtoto wa Mungu. Hata hivyo wakati mihadhara ya Waislamu ikipigwa marufuku mkoani humo, kuna taarifa kwamba Wakristo wameendelea kuhubiri kwa vishindo kwamba Yesu ni Mungu Mkuu na kwamba asiyekubali imani hiyo amepotea. Mahubiri hayo ya Wakristo yamekuwa yakifanyika katika viwanja vya furahisha chini ya Mchungaji aliyefahamika kwa jina la moja la Mkova. Mahubiri mengine yamekuwa yakiendelea katika viwanja vya Kitangiri, Kilimahewa, Igogo na sehemu nyingine. Wakati huo huo, Mwandishi Idi Katimba anaripoti kutoka mjini Mtwara kwamba Wakristo wa dhehebu la Walokole wamekuwa wakiendesha mahubiri yanayodai Yesu sio Mwislamu bali ni Mungu Mkuu na kwamba wasioikubali imani hiyo wamepotea na watakwenda Jahannam. Miongoni mwa waliotajwa kwenda Jahanam ni pamoja na Waislamu na Wakatoliki. Taarifa kutoka mjini humo zinaeleza kuwa wakazi wa mji huo ambao sehemu kubwa ni Waislamu, wamepigwa na butwaa kufuatia mahubiri hayo ambayo yamekuwa yakiendelea kwa masiku kadhaa. Halikadhalika mjini Songea nako hali si shwari kwa upande wa Waislamu, huko imeripotiwa kwamba mwishoni mwa wiki iliyopita Waislamu wanne walipata mkong’oto kutoka kwa polisi wa mjini humo kwa madai ya kuuza kanda zinazodaiwa kukashifu dini nyingine. Waislamu hao wametajwa kuwa ni Bwana Mohamed Kawanga, Abdallah Hussein, Ali Kipande na Mzee Kalungo. Gazeti hili liliwasiliana na kamanda wa polisi mkoani humo siku ya Jumatano kuthibitisha taarifa hizo, hata hivyo kamanda huyo alisema hana taarifa kamili na aliahidi kutoa maelezo siku iliyofuata. Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni jitihada za kuwasiliana tena kamanda huyo hazikufanikiwa. |
TAHARIRI Maoni yetu: Wananchi kataeni kupotoshwa SUALA LA MWEMBECHAI: Wabunge
wataka kujua nani aliamrisha kuua
Katiba ya nchi yapuuzwa: Waislamu wapigwa marufuku kuhubiri Mtihani darasa la saba 1998: Manispaa
Moro yaagiza ipewe majina ya wanafunzi Wakatoliki
“Wushu”ya Waislamu wa China
na jinsi ilivyowasaidia kupambana na dhulma dhidi yao
Yesu wa kwenye Mathayo siyo Yesu wa
kwenye Luka
Ni nani hawa Waislamu wa Siasa Kali
?
Waislamu tuondokane na unyonge
Waislamu wana mwelekeo wao
Ni mwaka gani Yesu alianza kuitwa
Mungu
Wanawake wameamua kuwa wazi
kweli kweli
Kimya kingi kina mshindo mkuu:
Vipi Mhe. Rais wale walioua?
Mtazamo wa madhalimu wa Tanzania
kwa Waislamu
Waislamu mkoa wa Morogoro
wampinga Yahya
Polisi wachafua mazingira
ya msikiti wa Mwembechai
Wanawake wa Kiislamu Ubungo
darajani wamuunga mkono Sheikh Bafadhil
Mafundisho ya Qur'an: Kanuni za kumkumbuka Allah na kutumia katika njia yake Chakula na lishe: Lishe ya
mtoto aliyekuwa mgonjwa
|