|
Na. 049 Jumatano Mei 24 - 30, 2000 |
|
|
|
|
|
Bin Laden, Taliban kusaidia Chechnya MOSCOW. Utawala wa wanamgambo wa Kiislamu wa kikundi cha Taliban huko Afghanistan pamoja na Mwana Mapinduzi wa Kiislamu, Bwana Osama Bin Laden wamekubaliana kutoa msaada wa silaha pamoja askari kusaidia Waislamu wa Chechenya. Mwakilishi wa Rais wa Chechnya, Aslan Maskhadov walifanya mazungumzo na afisa mwandamizi wa Taliban pamoja na Bwana Osama kiasi cha wiki iliyopia Kaskazini mwa Afghanistan katika jiji la Mazar-I-Sharif. Mwisho wa mazungumzo kulisainiwa mkataba kati ya pande hizo kusaidia wapiganaji wa Kiislamu wa Chechnya kwa hali, silaha na Askari. Imeelezwa kuwa kambi mpya ya mafunzo ya askari kutoka Uzbekistan, Tajikistan naChechenya imekwisha kamilika huko Afghanistan karibu na Mazar. Baadhi ya askari wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni wamekwenda Chechnya kuwasaidia Waislamu hao waliovamiwa na Russia. Msaada huo unafuatia mwito uliotolewa na Rais wa Chechnya Bwana Maskohadov mwanzoni mwa Mei mwaka huu kuwasaidia Waislamu wenzao wa Chechnya dhidi ya uvamizi dhalimu wa Russia.
Israel yaondoka kwa aibu MSAFF-AL-HAWAWA, LEBANON, Israel imeanza kuondoa vikosi vyake katika eneo ililokuwa inalikalia kwa mabavu huko Lebanon. Vikosi vya Israel baada ya kusukumwa na wapiganaji wa Kiislmau wa Hizbullah katika vita vya chini kwa chini vilivyopiganwa takribani miaka 22 huko Lebanon. WaziriMkuu wa Israel, Bwana Ehud Baraka amesema, watakuwa wameondoka hadi kufika katika mpaka unaotambulika kimataifa siku chache zijazo. Huku wapiganaji wa Hizhullah wakisonga mbele kwa miguu na magari hadi eneo la amani. Wanamgambo wa Lebanon ambao ni Wakristo waungaji mkono wa Israel wamesambaratika na kuanza kujisalimisha kwa Hizbullah. Baada ya kuondoka wapiganaji wa Israel, Hizbullah wanatarajiwa kushika maeneo hayo na kumiliki ukanda kutoka bahari ya Meditteranian hadi mwanzo mwa miinuko ya Milima ya Golan. Kiongozi wa Hizbullah Sheikh Hassan Nasra Ilah amesema, wataendelea n avita dhidi yaIsrael. Israel ambayo imesema, milima ya Golan ni ya Syria na si ya Lebanon inaelekea kutokubali kuachia milima hiyo.
Mapigano yaendelea pembe ya Afrika ADDIS ABABA, Ethiopia. Vikosi vya majeshi ya Ethiopia na Eritrea hapo jana vimeendelea kupigana vikali, hali ya kuacha raia zaidi ya 100,000 wakiwa wakimbizi. Waziri mkuu wa wa Ethiopia, Bwana Zenawi akizungumza jana na mabalozi wa nchi mbalimbali waliopo hapa alisema, nchi yake ipo tayari kufikia amani kwa kutumia njia yoyote itakayoharakisha kufikia lengo hilo. Waziri huyo akionesha matumaini ya kumaliza vita hiyo hii leo kwa ushindi dhidi ya Eritrea, aliongeza kuwa tutapigana huku tunazungumza. Eritrea nayo imeimarisha vikosi vyake katika eneo la Ariza ambako kuna miinuko na hivyo kuwa vigumu kutekwa na vikosi vya Ethiopia. Mnamo 1993 Eritrea ilijikomboa kutoka utawala wa Ethiopia baada ya mapigano ya muda mrefu. Wajumbe wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU) waliwasili jana mjini Asmara ili kuimarisha mazungumzo ya amani kati pande hizo. Licha ya mapigano katika nchi hizo za Pembe ya Afrika zinakabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame. Shirika la mpango wa chakula (WFP) limetangaza kuwa kiasi cha watu laki tano na nusu wanahitaji msaada wa dharura, na kuahidi kuongeza chakula za ziada hivi karibuni. Nalo shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) limeongeza kuwa limeendelea kugawa Biskuti nachakula kingine katika mji wa Asmara kwa Wahanga wa njaa. Nchi hizo zipo katika mapigano wakati
kwa siku mimi na tatu hadi hii leo huku zikipigana kwa kugombea ardhi.
Mgao wa umeme Kenya NAIROBI, Kenya. Wananchi Kenya wiki hii wataanza kupata umeme kwa mgao kutokana na vyanzo vya nguvu hizo kupungua na hivyo kusababisha uzalishaji hafifu wa nguvu hizo. Baadhi ya wananchi wameilalamikia hali hiyo kuwa inahatarisha maisha yao na kuwa ya kubahatisha. Msemaji wa wenye viwanda nchi Kenya amesema, watu wengi watakosa kazi kutokana na baadhi ya viwanda kusimamisha uzalishai au kufungwa kabisa. Aliongeza, Kenya ina asilimia 30 ya watu wasio na ajira hivyo kuja kwa tatizo la umeme kutaongeza idadi ya wasio na kazi na kuongeza ugumu wa maisha kwa raia. Wamiliki hao wa viwanda wamedai kuwa serikali iwaondelee kodi ili waweze kugharamia nguvu zingine za umeme, na kusisitiza kuwa hakuna haja kwa serikali kuchukua kodi wakati viwanda havizalishi. Sekta nyingine zinazotarajiwa kuathirika kutokana na mgao huo wa umeme ni mitambo ya kusukuma maji hali ambayo itafanya wananchi kuhangaika kwa kukosa maji. Imeelezwa kuwa umeme unaozalishwa nchini humo hautoshelezi mahitaji na hivyo Kenya imekuwa ikiagiza umeme kutoka nchi jirani ya Uganda. Wananchi wengi wameilaumu serikali kwa kutokuwa na mpango madhubuti wa kukabiliana na hali hiyo. Wakati huo huo, wabunge wa nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza wanaendelea na mkutano wao mjini Nairobi. Huku wakiazimia kuimarisha ushirikiano kwa kubadilishana uzoefu wa kazi. Mkutano huo una lengo la kuboresha usimamizi wa fedha na Bajeti katika Mabunge ya nchi zao. Mjumbe kutoka Tanzania Bwana Simon Mbilinyi amesema, ili kuimarisha utendaji wenye ufanisi katika hilo ni budi kuanzisha kamati ya Bajeti katika Bunge. Kamati ya Bajeti ambayo itapitia kwa makini Bajeti za Wizara na Idara mbalimbali kabla ya Waziri wa Fedha hajawasomea wabunge bajeti ya mwaka wa fedha. Ameongeza kuwa, muda wanaopewa wabunge kuipitia bajeti ni mdogo hivyo hautoshi kwa mbunge kusoma kwa siku mbili na kisha akatoa mchango wake katika hilo, hali ambayo imepelekea bajeti kupitishwa bila ya uchambuzi wa kina toka kwa wawakilishi hao wa wananchi. Katika mkutano huo imeelezwa kuwa Afrika ya Kusini ni mfano wa kuigwa namna bunge linavyosimamia bajeti kwa kuwa na kamati ya Bajeti. Bwana Mbilinyi ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa serikali ya Rais Mkapa ambaye
alijiuzulu baadaye aliongeza kuwa kukiwa na kamati ya bajeti itakuwa na
kazi ya kusimamia miundo na maswala muhimu ya Bajeti.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Chuo Kikuu Dar wafanya mitihani katika Bwalo la chakula Udini wa CCM utaisambaratisha nchi -Tambwe ‘Kutoweka’ kanda ya Kakobe: CCM yatuhumiwa Maalim Seif awaambia Wazanzibari: Wenye mamlaka ya kumuweka mtu Ikulu ni wananchi Mkapa afurahia maendeleo Pwani ‘Zawadi’ ya Uchaguzi yatishia kusambaratisha taasisi ya Kiislam Tanga Serikali yakemea mwanamke kudhalilishwa Ushauri Nasaha
MAKALA
Makala
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Makala
Makala
RIWAYA
Lishe
|
|
|
|
|