NASAHA
Na. 049 Jumatano Mei 24 - 30, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
‘Kutoweka’ kanda ya Kakobe:
CCM yatuhumiwa

Na Mwandishi Wetu

Wasiwasi na hofu vimeendelea kujengeka miongoni mwa wananchi juu ya iwapo chama tawala cha CCM kinajenga mazingira ya kuwepo kwa uchaguzi wa haki na huru kwa kutoingilia uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa watu kutoa maoni yao, imefahamika.

Hali hii imetokana na kushindikana kurushwa hewani kipindi maarufu cha televisheni cha Kiti Moto ambapo mgeni mwalikwa katika kipindi hicho alikuwa Askofu Mkuu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship ambaye katika siku za hivi karibuni aliwahi kukikosoa hadharani Chama cha Mapinduzi(CCM) kwa madai kuwa viongozi wake ni waoga na wanafiki.Gazeti moja la kila siku la Mei 21 liliripoti kuwa viongozi wa CCM ndio walioshinikiza 

kanda hiyo isitangazwe.

Shutuma hizo za Askofu Kakobe zilijibiwa na viongozi wa chama hicho akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Philip Mangula na Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM, Bw. Emmanuel Nchimbi, ambapo wote wawili walimponda Askofu huyo.

Katika maelezo yake, Bw. Mangula alimwelezea Askofu Kakobe kuwa ni mtu anayestahiki "kusamehewa tu na CCM", wakati Bw. Nchimbi alimtaka Askofu Kakobe achague kati ya siasa au dini.

Mpambano huo kati ya Askofu na viongozi wa chama tawala ambao ulitoa mvuto wa aina yake kwa wananchi inaaminika ndio uliopelekea kuandaliwa kwa kipndi hicho na kumshirikisha Askofu kakobe ambaye alihudhuria na kipindi kurekodiwa kama kawaida.

Kipindi cha Kiti Moto kwa kawaida hurushwa hewani siku ya Alhamisi na Kituo cha Televisheni cha DTV; na kipindi hicho kilichomrekodi Askofu Kakobe kilitarajiwa kutoka wiki iliyopita lakini mpaka sasa hakijatolewa hadharani na wala hazijaelezwa sababu zozote kuhusiana na hali hiyo isiyo ya kawaida.

Nasaha jana iliwasiliana kwa simu na ofisi ya Askofu Kakobe kutaka kujua iwapo kuna habari zozote za kuhusu sababu za kipindi hicho kutorushwa hewani na ni nini maoni na nasaha zake kwa watanzania. Hata hivyo Katibu Muhstasi wa Askofu huyo alijibu kwamba Akofu Kakobe hakuwepo ofisini kuweza kuzungumzia suala hilo na kwamba hapakuwa na kiongozi mwingine yeyote wa Kanisa ambaye angeweza kuzungumza kwa niaba ya Askofu Mkuu huyo wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship.

Aidha Katibu huyo muhtasi alifafanua kuwa Askofu Kakobe alikuwa nje ya ofisi akishughulika na wanafumnzi wake.

Hivi karibuni Kanisa hilo lilipata wachungaji wa kwanza ambao walibarikiwa na Askofu Kakobe mwenyewe.

Nasaha pia iliwasiliana kwa simu na Ofisi za DTV kutaka kujua kilichokwamisha kipindi hicho ambacho uchunguzi wa gazeti hili umebaini kilikuwa kikingojewa kwa hamu na wananchi ambapo msemaji wa ofisi hiyo ‘aliutupa mpira’ kwa waandaji wa kipindi hicho, Maasai studio.

"...tafadhali wasiliana na Maasai Studio, wao ndio walioandaa..."

Juhudi za kuwasiliana na Maasai Studio hazikufanikiwa.

Wachunguzi wa masuala ya kisiasa na kijamii nchini wanadai kuwa kanda hiyo imezuiliwa isitoke kwa shinikizo la CCM kwa vile "yaliyomo katika kanda hiyo ni mapigo dhidi yake".

Hofu ya CCM kuporomoshwa kutokana na shutuma za viongozi wa dini zimeongezeka kwa vile shutuma hizo za Askofu Kakobe zimekuja sambamba na shutuma dhidi ya viongozi wa siasa nchini zilizomo katika kitabu kilichotolewa na Tume ya Haki na Amani ya Baraza la maaskofu nchini ambapo watu wengi wameeleza kuwa viongozi wa kisiasa waliokusudiwa katika kitabu hicho ni wa CCM kwa vile wao ndio wenye serikali.

Kadhalika viongozi wa kiislamu nchini wamekuwa wakiishutumu serikali kwa kutowatendea haki waislamu hususani suala la mauaji ya Mwembechai.

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
KERO katika Elimu ziondolewe haraka

Chuo Kikuu Dar wafanya mitihani katika Bwalo la chakula

Udini wa CCM utaisambaratisha nchi -Tambwe

‘Kutoweka’ kanda ya Kakobe: CCM yatuhumiwa

Maalim Seif awaambia Wazanzibari: Wenye mamlaka ya kumuweka mtu Ikulu ni wananchi

Mkapa afurahia maendeleo Pwani

Wapinzani wajiimarisha Moro

‘Zawadi’ ya Uchaguzi yatishia kusambaratisha taasisi ya Kiislam Tanga

Serikali yakemea mwanamke kudhalilishwa

Ushauri Nasaha
Umuhimu wa kushirikiana na majirani katika malezi ya watoto

MAKALA
Afande Mahita, wananchi hatutaki Dola ya kipolisi

Makala
CCM hawawezi kuondoa umasikini, ndio tegemeo lao

Kalamu ya Mwandishi
Makubaliano kwa vitendo Z'bar

MAKALA
CCM na sera za maendeleo (5)

Makala
Wanawake na maendeleo: Je ni wimbo wa kuchaguliwa?

Makala
CCM inatawala badala ya kuongoza

Habari za Kimataifa

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra -4

Lishe
Unachotakiwa kufanya kabla ya kuweka chakula kwenye jokofu

BARUA

MASHAIRI

MICHEZO

  • Raza kufungua mashindano ya Wavu Zanzibar
  • Real Madrid yaota Ubingwa  leo
  • Kajumulo asema Yanga timu ya Wananchi

  •  


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita