|
Na. 049 Jumatano Mei 24 - 30, 2000 |
|
|
|
|
|
Na Mwandishi Wetu Mwenyekiti wa chama cha CUF Wilaya ya Temeke, ambaye pia ni mgombea wa ubunge wa chama hicho katika jimbo hilo amesema, udini wa CCM utaisambaratisha nchi. Akizungumza kama mgeni rasmi katika mkutano wa kumpongeza Prof. Lipumba kwa hatua yake ya kuchukua fomu za kugombea Urais uliofanyika Kigogo, jijini Mei 21 mwaka huu, Bwana Hiza alisema, CCM imekuwa ikiutumia wingi wa Waislamu kupata kura zao kwa kumtumia Sheikh Mkuu wa Bakwata kuwafanyia kampeni misikitini. Ili kuficha ukweli huo CCM imekuwa ikikituhumu chama cha CUF kuwa kinawatumia Waislamu kukifanyia kampeni misikitini. Huko nyuma Katibu Mkuu wa CCM Bwana Philip Mangula amewahi kuripotiwa akidai kuwa Waislamu wamekuwa wakihongwa kanzu, kanga na kofia ili kuendesha siasa misikitini. Kauli ya Katibu huyo wa CCM ililaaniwa vikali na viongozi wa Kiislamu ikiwemo Shura ya Maimamu inayoongozwa na Sheikh Mbukuzi iliyomtaka Bwana Mangula afute kauli yake na kuwaomba radhi Waislamu. Hata hivyo imefahamika hivi karibuni kuwa Sheikh Mkuu wa BAKWATA Hewmed Bin Jumaa akiongoza ujumbe wa chama hicho cha BAKWATA imeripotiwa akipita mikoani kuipigia kampeni CCM misikitini. Wakati ujumbe huo wa BAKWATA ukiwa mjini Iringa ilielezwa kuwa mmoja wa Masheikh katika ujumbe huo, Bwana Bafadhil alihamasisha kwa kusema "Mkapa juu". Akiendelea kufafanua Mhe. Tambwe Hiza alisema kuwa kitendo hicho si tu kuwa ni udini katika kampeni lakini pia ni kuwadhalilisha Waislamu kwamba si welevu na kwamba wao ni watu wa kutumiwa." Kwanini CCM haiwatumii mapadre na maaskofu kupiga kampeni, badala yake. Mwenyekiti huyo wa CUF Wilaya ya Temeke ambaye anapewa nafasi kubwa ya kushinda ubunge katika jimbo la Temeke na wananchi amesema kuwa CCM imekuwa ikipiga propaganda kuwa CUF ni chama cha Waislamu ili kuwazuia Wakristo wasijiunge nacho. Akasema hiyo ni hatua mbaya ambayo inaweza kuwagawa wananchi kwa dini zao kama wananchi wasipotumia akili zao vyema kung’amua propaganda hizo za CCM. Akaongeza kusema kuwa Wakristo warevu kama yeye hawababaishwi na propaganda hizo na wanaendelea kujiunga na chama hicho siku hadi siku. "Sisi katika CUF tunatambua kuwa huwezi kutumia
Biblia wala Qur’an katika kujenga barabara, mahospiali wala mashule. Bali
kuwa na mipango mizuri na kwa kutumia vyema kodi ya wananchi", alisema
Mhe. Tambwe na kuongeza kuwa propaganda hizo za CCM wao haziwasumbui na
ni dalili ya kufilisika kisiasa.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Chuo Kikuu Dar wafanya mitihani katika Bwalo la chakula Udini wa CCM utaisambaratisha nchi -Tambwe ‘Kutoweka’ kanda ya Kakobe: CCM yatuhumiwa Maalim Seif awaambia Wazanzibari: Wenye mamlaka ya kumuweka mtu Ikulu ni wananchi Mkapa afurahia maendeleo Pwani ‘Zawadi’ ya Uchaguzi yatishia kusambaratisha taasisi ya Kiislam Tanga Serikali yakemea mwanamke kudhalilishwa Ushauri Nasaha
MAKALA
Makala
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Makala
Makala
RIWAYA
Lishe
|
|
|
|
|