|
Na. 036 Jumatano Februari 23 - 29, 2000 |
|
|
|
|
|
Clinton kusaidia amani Burundi Washington, DC. RAIS Bill Clinton wa Marekani ameahidi kutoa msaada wowote ili kufanikisha zoezi la kurudisha hali ya amani nchini Burundi. Akihutubia hapo jana mjini Arusha, Tanzania Rais huyo awali alitoa pongezi kwa Bwana Nelson Mandela ambaye ndiye kiongozi mkuu wa usuluhishi. Hotuba yake iliyochukua dakika 10 ilitolewa kwa njia ya 'Internet'. Katika mkutano huo unaotarajiwa kuendelea kwa siku 10 za majadiliano ulihudhuriwa na vyama 10 kati ya kumi na nane . Viongozi wa vyama hivyo wametoa mwito kuwa tume iundwe ili iandae mapendekezo kabla ya kuidhinisha mpango huo wa amani. Bwana Nelson Mandela alilazimika kuingilia kati katika mazungumzo hayo pale viongozi wa vikundi hivyo walipokamiana kwa maneno . Msuluhishi wa mgogoro huo Bwana Mandela anatarajiwa kufanikisha zoezi
hili kutokana na kutoegemea upande wowote kwa dhati ya dhamira yake.
Nigeria yaazimia kuwa taifa la Kiislamu Kaduna,NIGERIA. Mapigano kati ya Waislamu na Wakristo yaliyozuka siku ya jumatatu wiki hii yamesababisha watu ishirini na tano kufariki dunia. Chanzo cha mapigano hayo ni Wakristo wa jimbo la Kaduna kupinga mwenendo wa waislam wa kutaka kuanzisha sheria za kiislamu katika mpango mzima wa Nigeria kukamilisha azma yake ya kuwa Dola ya kiislamu. Nchi hiyo iliyopo magharibi mwa Afrika ina idadi kubwa ya watu, wengi wao wakiwa ni waumini wa dini ya kiislamu. Jimbo la Kaduna ni moja ya majimbo yaliyoazimia kuanzisha utawala wa kiislamu baada ya jimbo la Zamfara kutangaza rasmi kufuata sheria za kiislamu mwanzoni mwa mwaka huu. Azma hiyo imepingwa vikali na wakristo wa Nigeria wakidai kuwa sharia ya kiislamu itawabagua , wakati waislamu wameeleza kuwa sheria hizo haziwahusu wasiokuwa waislamu. Nigeria ni nchi yenye nguvu za kijeshi na ushawishi mkubwa katika ukanda wa magharibi mwa Afrika. Oktoba mwaka huu Nigeria itaadhimisha miaka 40 tangu kujipatia uhuru
kutoka kwa wakoloni ambao walikuwa ni wafuasi wa dini ya kikristo.
Serikali mpya Mali BAMAKO,Mali. Rais wa Mali ametangaza jana Serikali mpya itakayoiongoza Mali katika kipindi kijacho. Kutangazwa kwa Serikali mpya hiyo kunafuatia kujiuzulu kwa Serikali ya Waziri Mkuu aliyepita kujiuzulu. Serikali mpya hiyo itakuwa na wanachama kumi na tano wapya. Nchi hiyo yenye Waislam wengi ni moja ya nchi zenye eneo kubwa barani
Afrika na ipo Afrika ya Magharibi.
Askari wa Urusi wawatesa raia Matukio kadhaa yametokea dhidi ya raia wasio na hatia wa Chechnya. Matukio hayo yamefanywa na askari wa Urusi katika maeneo mbalimbali ndani ya Chechnya. Katika jimbo la Urus-Martan kijiji cha Katyr-Yurt kati ya raia 300 hadi 400 wameuawa kwa risasi ambazo zilikuwa zinapigwa mfululizo katika makazi ya raia hao.Nyumba nyingi katika eneo hilo zimechomwa moto na kuharibiwa kabisa.Tukio jingine lilitokea katika mji wa Gekhi-Chu ambapo raia kadhaa wameuawa na wasichana wengi kubakwa. Majeshi ya Urusi pia yamekuwa yakiwakamata wanaume na kuwazika wakiwa hai. Imeripotiwa kuwa wasichana watatu ambao walikuwa wanarejea Grozny kutoka
katika makambi ya wakimbizi ili kukagua nyumba zao baada ya mapigano kusimama
katika mji huo waliuawa kikatili na askari wa Urusi. Askari wa Urusi waliwakamata
wasichana hao na kuwaziba kwa vitambaa kwenye uso na baadae wakawapiga
risasi.
Yugoslavia yailalamikia UN NewYork,UMOJA WA MATAIFA. Yugoslavia imetoa malalamiko yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya askari wa kulinda amani walioko nchini Yugoslavia. Taarifa hiyo imeeleza kuwa askari wa Umoja wa Mataifa walioko huko wameonesha tabia mbaya na utumiaji nguvu huko Kosovaska. Kikosi cha askari wa Umoja wa Mataifa kinaendesha kampeni nyumba hadi
nyumba katika zoezi la kunyang'anya silaha.
Taiwan yaionya China SERIKALI ya Taiwan imeionya China kuwa iache mawazo yake ya kuwa Taiwan ni jimbo la China, kwani Taiwan ni Taifa linalojitegemea. Waziri wa Mambo ya Nje wa Taiwan amesema kuwa Taiwan itaongeza uwezo wa kijeshi kwa kupata silaha toka Marekani ili kujilinda dhidi ya uonevu wowote wa China. Naye Waziri wa Mambo ya Ndani wa Taiwan amesema kuwa China ikome kutaka kuitawala Taiwan. Kwa muda mrefu hivi sasa China na Taiwan zimekuwa katika mgogoro na kutoelewana katika nyanja za utawala na siasa. China ambayo bado inashikilia msimamo wake wa kuendeleza itikadi ya Ukomunisti, itikadi ambayo ilipigwa mweleka na demokrasia mwanzoni mwa miaka ya tisini. Taiwan na China ni Mataifa yaliyopo katika bara la Asia. |
YALIYOMO
Tahariri:
‘CUF tumejiandaa kuchukua serikali' Suala la Mwembechai lazua mtafaruku Mabadiliko ya katiba ya Zanzibar: CCM Z'bar ina nafasi ya ushindi MPASHO
NASAHA
Habari
za ndani
Ushauri
Nasaha
MAKALA
WAZO
LA WIKI
Makala
ya Kimataifa
Kalamu
ya Mwandishi
MAKALA
LISHE
|
|
|
|
|