AN-NUUR 
Na.173 Rajab 1419, Oktoba 30 - Novemba 6, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Fuateni Sharia ya Allah - Sheikh 

Na Badru Kimwaga 

Imeelezwa kuwa vitendo viovu na kuharibika kwa maadili ya jamii huchangiwa kutokana na kupuuzwa kwa sheria za Mweneyezi Mungu, ambayo inaelekezwa na Kitabu kitakatifu cha Qur-an na pia kudhaniwa kuwa sheria za Mwenyezi Mungu ndani ya Kitabu hicho kinawahusu Waislamu peke yao. 

Hayo yameelezwa na Sheikh Idd Mohamed alipokuwa akiongea na waumini wa Msikiti wa Bonde la Mpunga Msasani, mara baada ya swala ya Alasir, Msikitini hapo, jijini wiki iliyopita. 

Sheikh Mohamed alisema kuwa watu wengi hudhani kuwa Qur-an ni Kitabu cha Waislamu tu na sheria zake zinawahusu wao, wakati ukweli ni kwamba sheria za Mwenyezi Mungu zinawahusu binadamu yeyote aliye ndani ya zama za Umma wa Mtume Muhammad (s.a.w.). 

"Maovu yamezidi kutokana na sheria za Mwenyezi Mungu kutofuatwa, huku Waislamu wanapoitangaza na kueleza bayana wako watu wenye kupinga ilihali zina malengo ya kuendesha maisha ya binadamu zama hizi katika ulinganifu bila kuzingatia yupi dini ipi na yupi Muislamu "Alisisitiza Sheikh Mohamed. 

Aliongeza kuwa, sheria kama za kukataza watu kuzini kulingana na Qur-an inakataza, lakini watu wenye kumuhalifu Mungu, ndio kwanza husisitiza matumizi ya kondomu, ikiwa unataka kujiepusha na ukimwi, wakati kama ingetekelezwa sheria hiyo, hakungekuwa na magonjwa ya zinaa kama ukimwi. 

Pia aligusia mambo ya wizi, ubakaji na kunajisi na kusema kuwa hii ni kazi na laana ya kuacha sheria za dini ya Kiislamu, iliyo ndani ya kitabu cha Qur-an na kuwaomba Waislamu kuwa watendaji wakuu katika kuitekeleza iili kuwavutia watu wasio Waislamu kuona umuhimu wa kuzingatia sheria hizo. 

"Lau watu wangelishikama na sheria zangu ningeliwaneemesha neema mbalimbali (alinukuu Aya) lakini je tunashikama na kamba hiyo au ndiyo wenye kupinga na kujifanya binadamu tuna akili nyingi kuliko aliyetuumba, Astaqafirullah... "Alisema Sheikh Mohamed na kumalizia. 

Alitoa mfano kwa kusema nchi zinazozingatia Qur-an ugonjwa kama ukimwi na uhalifu hutendwa kwa asilimia kidogo kulinganisha na nchi nyingine zinazodai kustaarabika ingawa sio kweli. 



Wanawake wa Kiislamu Mburahati wahimizwa kutafuta elimu 

Wanawake wa Kiislamu Mburahati Jijini Dar es Salaam wamehimizwa kujipinda kuijua dini yao ili waweze kuishi kwa mujibu wa mafundisho yake. 

Wanawake hao wametakiwa pia kuwa na mapenzi miongoni mwao kwa kupeana sadaqa na kutembeleana. 

Hayo ni baadhi ya mambo yaliyoelezwa katika mada mbali mbali zilizowasilishwa katika kongamano la wanawake wa Kiislamu lililofanyika Oktoba 10, 1998 Masjid Aqswa Mburahati Jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza katika kongamano hilo Bi. Tunda alisema kwamba kutafuta elimu, upendo na utoaji wa sadaqa ni vitu vinavyoweza kumsaidia Mwanaadamu dunia na akhera, hivyo aliwataka wanawake hao kushikamana na vitu hivyo. 

Mzungumzaji mwingine Bi. Fatma alitolea mfano wa utekelezaji wa nguzo ya zaka kama ni moja ya mambo yanayoweza kustawisha udugu miongoni mwa jamii. 

Mzungumzaji aliyeonekana kuvuta hisia za wengi alikuwa Bi. Amina ambaye alizungumzia madhila mbalimbali yanayowafika Waislamu wa hapa nchini. 

Alisema kadhia ya Mwembechai imethibitisha malalamiko ya Waislamu kwamba hawatendewi haki sawa na raia wengine. 

Alitoa mfano wa mambo waliyotendewa wanawake wa Kiislamu Mwembechai na kuhoji ni hatua gani ilizochukuwa Serikali dhidi ya wahusika. 

Aidha, mzungumzaji huyo aligusia suala la Nzasa na kusema kwamba anasikitishwa na jinsi Serikali ilivyowatendea wananchi wa eneo hilo. 

 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 

TAHARIRI 
Wakipewa fursa watainusuru nchi

Wasomi watetea haki ya wananchi kumiliki ardhi

Serikali izungumze na wananchi–Mzee Gonga

Akina mama watakiwa kushikamana na dini yao

Maoni
Serikali inaWhite Paper:  Wananchi mna nini?

Dondoo za Saikolojia: Hoja kengeza
Na Abu Halima Sa Changwa

Makala ya mtangazaji
Khatamy sio Gorbacheiv!!!

Makala
Malipo ya fadhila
Na Mohamed Saleh

Tanzania tuna sera gani kuhusu kanda
Na Abu Abdullah, Tanga

Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo- 2
Na Nandenga wa Mkomidachi

Teknologia
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (3)
Na Hassan Omar

Makala na habari
'Usiiparamie ovyo Theolojia'
Na Charles Kamuhabwa, DSA Mtwara

Mwinyimkuu kufanya sensa ya waumini Magomeni
Na Jamillah Nassoro

Same tusilimu upya

Wazazi Mwanza wahimizwa kuwashonea watoto wao Hijab
Na Idd Katimba, Mwanza

Tuwaige Wangazija, 'tutafanikiwa'
Mwandishi: Maalim Bassalah

Serikali imeweka rekodi ya kutisha – Sheikh Salim
Na Mwandishi Wetu

Muhadhara waunguruma Geita
Na Hussein Abdallah, Geita

Fuateni Sharia ya Allah - Sheikh
Na Badru Kimwaga

Wanawake wa Kiislamu Mburahati wahimizwa kutafuta elimu

Mafunzo ya Qur'an
Vijana wa pangoni

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na lishe
Chakula ni silaha ya kukabiliana na changamoto ya kansa
Na Mujahid Mwinyimvua
 
 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita