AN-NUUR 
Na.173 Rajab 1419, Oktoba 30 - Novemba 6, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
Tahariri Wakipewa fursa watainusuru nchi 
  

Mwenyezi Mungu katika kitabu chake kitakatifu anatueleza kwamba:- 

Nyinyi ndio Umma bora kuliko Umma zote zilizodhihirishiwa kwa watu (Ulimwenguni) - mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamwamini Mwenyezi Mungu. (3:110). 

Aya hii kwa uchache inataja wajibu waliokabidhiwa Ummah wa Kiislamu nao ni kuwaongoza walimwengu katika kheri na kuwaondolea shari na maovu katika jamii zao. Na ili kuifanya kazi hiyo wakapewa mwongozo. 

Itakuwa ni kinyume cha mambo kama Waislamu watalipuuza jukumu lao hili na kuwaacha walimwengu watangetange kizani. 

Itakuwa ni kiroja zaidi kama wenye mwongozo watauweka uchagoni mwongozo wao na wakawatanguliza wasiojua pakwenda, wasiojua lengo la kuumbwa kwao bali wadhanio wapo hapa ili wale, wanywe, wazaaane na wastarehe waonavyo. 

Kiza kilichotanda katika jamii, haki haijulikani wala batili, mauaji, unyanganyi, ufuska, uharamia wa uadilifu kuwa bidhaa adimu, sheria kuwa na sura kisiasa; ubalakala na maadili kuporomoka kiasi cha kutisha, yote haya ni matokeo ya lazima ya kufuata miongozo inayotizama ulaji na unywaji kwa wasaa kuwa lengo kuu la uhai. 

Qur’an inasema, "Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa sababu ya yale iliyoyafanya mikono ya watu....." (30:41). 

Uangamizaji wa makazi ya watu; vurugu za kisiasa, vurugu katika jamii, vurugu katika uchumi na kukosekana amani na furaha ya kweli kwa Walimwengu, kwa yote haya lawama hurejea kwa wale walioambiwa: 

Na vivyo hivyo tumekufanyeni umati bora (kama kibla chenu tulivyokifanya bora) ili muwe mashahidi juu ya watu na Mtume awe shahidi juu yenu. (2:143). 

Hapana ‘White Paper’, dira ya nchi hadi 2025, vyama vya upinzani, makongamano, warsha wala midahalo itakayotatua matatizo ya nchi hii na kwingineko duniani. Ufumbuzi pekee ni kuibuka watu wenye mwongozo sahihi ambao wapo hadhiri na matatizo ya jamii yao na ambao hawapo tayari kuona kwamba jamii inatangatanga kizani wakati mwongozo usio na tone la shaka ndani yake upo. 

Hata hivyo uzoefu wa kihistoria unaonyesha kwamba kuwepo kwa watu hawa na hasa wanapojitokeza kama wasemaji na wakombozi wa watu, huonekana kuwa tishio kwa baadhi ya watu wenye kujali zaidi maslahi ya nafsi zao na utoshelezaji wa matamanio yao. 

Kwa hali hiyo wanaojitolea kuinusuru jamii mara zote hukabiliwa na mitihani, mateso na kusakamwa kwingi kwa namna tofauti tofauti. 

Pamoja na hayo jukumu hili halikwepeki kwa sababu ndio ukhalifa wenyewe vinginevyo maisha yote haya yatakuwa hayana maana. 

Tunapokutana kwenye darsa zetu, taasisi zetu, jumuiya zetu na misikiti yetu lengo liwe ni kuwaandaa "watu ambao biashara, kuuza na maslahi binafsi hayawashughulishi (hayawasahaulishi) kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na kusimamisha sala, na kutoa zaka, wanaiogopa siku ambayo nyoyo zitadahadari na macho (pia yatadahadari). (24:37). 

Watu wa namna hii pekee wakipewa fursa ya kuongoza na kusimamia mambo ndio watakaoinusuru jamii. 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
TAHARIRI 
Wakipewa fursa watainusuru nchi

Wasomi watetea haki ya wananchi kumiliki ardhi

Serikali izungumze na wananchi–Mzee Gonga

Akina mama watakiwa kushikamana na dini yao

Maoni
Serikali inaWhite Paper:  Wananchi mna nini?

Dondoo za Saikolojia: Hoja kengeza
Na Abu Halima Sa Changwa

Makala ya mtangazaji
Khatamy sio Gorbacheiv!!!

Makala
Malipo ya fadhila
Na Mohamed Saleh

Tanzania tuna sera gani kuhusu kanda
Na Abu Abdullah, Tanga

Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo- 2
Na Nandenga wa Mkomidachi

Teknologia
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (3)
Na Hassan Omar

Makala na habari
'Usiiparamie ovyo Theolojia'
Na Charles Kamuhabwa, DSA Mtwara

Mwinyimkuu kufanya sensa ya waumini Magomeni
Na Jamillah Nassoro

Same tusilimu upya

Wazazi Mwanza wahimizwa kuwashonea watoto wao Hijab
Na Idd Katimba, Mwanza

Tuwaige Wangazija, 'tutafanikiwa'
Mwandishi: Maalim Bassalah

Serikali imeweka rekodi ya kutisha – Sheikh Salim
Na Mwandishi Wetu

Muhadhara waunguruma Geita
Na Hussein Abdallah, Geita

Fuateni Sharia ya Allah - Sheikh
Na Badru Kimwaga

Wanawake wa Kiislamu Mburahati wahimizwa kutafuta elimu

Mafunzo ya Qur'an
Vijana wa pangoni

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na lishe
Chakula ni silaha ya kukabiliana na changamoto ya kansa
Na Mujahid Mwinyimvua

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita