AN-NUUR
Na.156 Rabi' Awal 1419, Julai 4 - 9, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
MASHAIRI
 

Nakupongeza Bi Batuli

Kalamu yangu nashika, salamu nakutumia, 
Nataraji bila shaka, Rabana akijalia, 
Waraka utakufika, hapo utakapokua, 
Nakupongeza Batuli, kwa shairi lako zuri. 

Kwa shairi lako zuri, Batuli nakupongeza, 
Kwani nimelikariri, hadi nimelimaliza, 
Hapakuwa na dosari, yote uloyaeleza, 
Nakupongeza Batuli, kwa shairi lako zuri. 

Dua ulizoziomba, kwetu inahitajika, 
Awalipie Muumba, wenzetu wameteseka, 
Makubwa yamewakumba, hakika twasikitika, 
Mauaji mwembe chai, mno yatuhuzunisha. 

Kama ulivyotamka, mikono umeinua, 
Kwa mola wetu Rabuka, ndie atae amua, 
Wote waliohusika, adhabu kuwafikia, 
Mauaji mwembe chai, mno yatuhuzunisha. 

Nimekuunga mkono, Bi Batuli nakwambia, 
Kwa hayo yako maneno, uliotuhadithia, 
Imekua ni mfano, kwa wote Islamia, 
Mauaji mwembe chai, mno yatuhuzunisha. 

Hakika watudhulumu, tena pasi na huruma, 
Hasa kwa Waislamu, huzidisha uhasama, 
Dhamana kwao haramu, yawanyima mahakama, 
Mauaji mwembe chai, mno yatuhuzunisha. 

Hatunalo la kusema, bali kwetu kushukuru, 
Kwa mola wetu Karima, ndie atae wadhuru, 
Tumlilie daima, maombi yawe kathiru, 
Mauaji mwembe chai, mno yatuhuzunisha. 

Suleiman Khamis, 
P.O. Box 571, 
Arusha. 
 
 

Muislamu kwao wapi?

Bismilahi naanza, Rahmani Rehemeza, 
Ndilo jina la Mweza, ambalo tunatukuna, 
Ambayo yanatukera, Roho zetu kuumiza, 
Mwislamu kwao wapi, Mwislamu wa Tanzania. 

Mwislamu si chochote, hapa kwetu Tanzania, 
Mwislamu si lolote, hapa kwetu Tanzania, 
Utu wake usilete, hapa kwetu Tanzania, 
Mwislamu kwao wapi, Mwislamu wa Tanzania. 

Popote anapokuwa, Mwislamu afukuzwa, 
Dayamondi alikuwa, Mwislamu kafukuzwa, 
Misikiti imekuwa, Mwislamu akimbizwa, 
Serikali tuambie, nyumbani kwetu ni wapi? 

Mabomu tunamwagiwa, risasi yateuliwa, 
Mwislamu auliwa, polisi wanawauwa, 
Utuwake wauliwa, Mwislamu wa Tanzania, 
Serikali tuambie, Mwislamu kwao wapi? 

Kina mama wamefuatwa, kule kwetu Mwembechai, 
Kule ndani wamefatwa, Msikiti Mwembechai, 
Milango yetu, kufyatwa, kule kwetu Mwembechai, 
Serikali tuambie, tukaishi kona gani. 

Islamu wameswekwa, Islamu Tanzania, 
Kule Keko wameswekwa, kunyanyaswa Tanzania, 
Rumande wameswekwa, Mwislamu wa Tanzania, 
Dhamana kwao hakuna, Serikali imesema. 

Huduma kwao hakuna, magonjwa yamewakumba, 
Madawa kwao hakuna, mauti yamewasomba, 
Serikali inatuna, kuwaona wanasombwa, 
Makamba Gewe mseme, Mwislamu ende wapi? 

Ukweli wetu kunena, Serikali hamtaki, 
Hivi sasa mnaguna, ukweli wetu shitaki, 
Lwambano naye anuna, Kanisa lake shitaki, 
Serikali tuambie, kanisa lawapa nini? 
Hata rungu mnashika, Islamu kuwapiga, 
Hata risasi mwashika, Islamu kuwapiga, 
Maneno mnayashika, yakanisa mnatwaga, 
Serikali tuambie, kwani ninyi dini gani? 

Tamati naishiliza,kwa nguvu zake Mweza, 
Muumba wetu Rabuka, Rehema zako Mweza, 
Rehema zako kushuka, Segerea nako Keko, 
Islamu uwaweke, kwa nguvu zako karima. 

Bi. G.J. Temba, 
DAR ES SALAAM. 
Juu 
 

YALIYOMO
 
TAHARIRI 

Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini 

Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani

Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke

Serikali kuzuia mahubiri ya Waislamu, kuvamia Msikiti, kukamata, kudhalilisha na kuua Wananchi ni kuvunja Katiba na Sheria za Nchi

Kujua lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Na Sadick M. Sadick"

Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi

Intifada ndio jibu (2)
Na Sheikh Pandukizi Dilunga

Kusema ukweli ni sehemu ya uadilifu
A.S. Chachika

Mafumbo ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Na J. Hussein

Majibu kwa Kamara Kusupa

Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai

Asiye na elimu kwa mujibu wa Biblia
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa

TAMTA yaadhimisha miaka 36
Na Masoud Mohamed Said, Tanga

Muumini aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Na Muhibu Said

Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30

Habari za Madrasa

Barua 

Mashairi 

Lishe : Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili 
Na Dk. Ali. A. Mzige
  

 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita