|
|
| Kusema
ukweli ni sehemu ya uadilifu
A.S. Chachika Mtume (S.A.W.) amesema: "Haachi kusema uongo mmoja wenu mpaka jina lake liandikwe kwenye milango wa moto. Na Haachi kusema ukweli mmoja wenu mpaka jina lake liandikwe kwenye mlango wa peponi." Kutokana na mafundisho haya, kusema uongo ni aswi na kusema ukweli ni katika ibadat. Hapa Tanzania suala la ukweli na uongo linachukua sura tofauti. Wako wale ambao hukusudia kusema uongo ili kulinda ufisadi wao na kuwalazimishia maovu watu ambao hawana uovu. Wako pia ambao wanajitahidi kudumu katika kusema ukweli hata kama unawaudhi wakubwa na jamaa zao. Hawa mara nyingi wameitwa kwa majina wasiyostahili kama vile wachochezi, waliochoka na amani waleta vurugu na kadhalika. Kwa bahati mbaya uongo unaosemwa mara nyingi katika lengo la kuwalazimisha watu maovu, unaelekezwa kwa Waislamu. Mara kadha hili limetokea na kwa kweli linafanywa na vyombo vya habari hasa vya dola na baadhi ya viongozi wa dola ambao inaelekea kama walioandaliwa kufanya hivyo. Chukua mfano mdogo tu wa radio yataifa ‘RTD’. Kila mwaka mara mbili katika sikukuu za Kiislaam, utasikia RTD inawatangazia watu kuwa, ‘Leo Waislamu wa Tanzania wanajiunga na Waislaamu wenzao ulimwenguni kusherehekea Idi.’ Kauli hiyo mara nyingi inakuwa ya kuchekesha na kumshangaza hata huyo mtangazaji mwenyewe kwani ukweli ni kuwa mara zote sikukuu za Kiislamu Tanzania hufanyika siku moja baada ya Waislamu wengine kusali. Uongo kama huu unaweza kufikiriwa kuwa ni jambo dogo lakini kwa hakika unakusudiwa kuwafanya wale Waislamu ambao ndio hasa wanaoungana na Waislamu wa ulimwengu mzima waonekane kuwa wao ni wakorofi kama ambavyo wameshaambiwa mara nyingi. Mara kadhaa na kwa nyakati tofauti viongozi wa dola wemetoa shutuma za uongo dhidi ya Waislamu tena shutuma za kufanana kwa miaka tofauti. Kwa kweli ukiyatafakari kwa makini utakubaliana nasi kuwa shutuma hizo ni za kupangwa na kutolewa kwa makusudi maalumu katika kuficha ufisadi na hujuma juu ya Waislamu. Mwaka 1993 katika harakati za kuendeleza hujuma dhidi ya Waislamu kufuatia kadhia ya uvunjaji wa bucha za nguruwe, Bana Agostine Mrema akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi na kada wa CCM, aliwatuhumu Waislamu kuingiza kontena la silaha (majambia). Mwaka huu 1998 kiongozi wa dola wa ngazi ileile, katika kuficha unyama na aibu ya serikali katika kuua watu kwa kuwalenga shabaha na kuchagua yule na yule, ametoa madai kuna nchi na balozi zinazochochea vurugu kwa kuwatumia Waislamu. Hadi sasa hatujasikia nchi na balozi hizo licha ya kuchukuliwa hatua lakini hata kule kuzitaja tu. Hii inatuthibitishia kuwa hizo zilikuwa propaganda za kujaribu kuficha ukweli. Alhamdulillah, pamoja na propaganda dhidi ya Uislamu na Waislamu, wako watu ambao bila kuogofyiwa na vitisho na shutuma za dola na vyombo vya habari vya mlengo wa kando, wamedumu katika ukweli. Allah (S.W.) azithubutishe nyoyo zao katika hilo. Kuitwa wachochezi na waliochoshwa na amani kusiweze kuwagubika kwa kiza cha kukwepa ukweli. Ama Mwenyezi Mungu anapotaka kudhihirisha neema zake juu ya waja, huzipitishia popote apatakapo. Kwa msingi huo wamepatikana watu ambao japo madhila yanayowakumba walengwa hayawahusu moja kwa moja, wameibuka na ari na ujasiri wa kusema ukweli japo watachukia wakubwa na maadui wa walengwa. Hawa wameona ukweli uliopo juu ya ‘Vita Kuu ya Nne ya Dunia’ kama ilivyoelezwa na mkuu wa ujasusi wa Ufaransa Bwana Cont De Marenches katika (the 4th W.W. Diplomacy and Espionage in the Age of T errorism – 1986) alipobainisha kuwa, vita kuu ya nne ni vita dhidi ya Uislamu. Kufuatia kadhia ya Mwembechai wamejitokeza kina ‘Emanuel Kavishe wa Daily Mail’. Katika toleo la Machi 31, 1998 anasema: "I witnessed the beginning and the end of the riot. I was told by the group I had shelted with that they had reasons, a targent and courage to fight and set fire to what they considered to be an annoyance. The government does not care for our problems. The government is a father who should look after his children. We are the children, we are not being looked after …..This is CCM government and they are destroying us. This is why we are aiming our actions on them. Tafsiri: Nilishuhudia mwanzo – hadi mwisho wa ghasia. Niliambiwa na kundi la watu ambalo nilikuwa kati yao kuwa walikuwa na sababu, lengo na ubavu wa kupigana na kuchoma kile walikiona kuwa ni kero kwao. Serikali haijali matatizo yetu. Serikali ndiyo aba na haina budi kulea watoto wake. Sisi ndio watoto na hatuangaliwi. Hii ni serikali ya CCM na wanatuangamiza. Hii ndiyo sababu tunaelekeza vitendo vyetu kwayo. Mwingine aliyesukumwa na ukweli ni Bwana ‘Kajubi Mukajanga’ yeye katika toleo hilo hilo la 31 Machi, 1998 anasema: "When Mwembechai first erupted on February 12, force was used to queil the riots. Two people were killed by the riot police and other two hundred arrested. Debate still rages in as to whether the force was not excessive. But since then no porper inquiry has been done to establish the justification of police having to open fire into an unruly crowd. Tafsiri: Ghasia zilipolipuka Mwembechai mara ya kwanza Februari 12, nguvu za dola zilitumika kuzimisha ghasia. Watu wawili waliuliwa na polisi wa kutuliza fujo na wengine mia mbili kutiwa korokoroni. Bado mjadala unaendelea miongoni mwa wananchi wakihoji kuwa nguvuiliyotumika haikuvuka mpaka. Hata hivyo tangu wakati huo hakuna uchunguzi wowote uliofanyika kuhalalisha kitendo cha polisi kufyatua risasi katika kundi la watu ambalo limeparaganyika. Mabwana hawa wamesema ukweli kuhusu ushuhuda wao kulingana na kadhia ya Mwembechai iliyopelekea serikali kutumia silaha kwa raia ambao hakustahili kuuliwa. Bahati nzuri kwamba hawakuitwa wachochezi lakini hata hivyo ushuhuda wao bado hauwagusi viongoziwa dola hasa wale waliohusika na kashifa ya mauaji ya Mwembechai. Mbali na hao, liko kundi la wabunge waliotaka kupeleka hoja ya kuundwa tume. Hawa walipuuzwa. Wasomi wa ngazi za juu wamehoji hali hii; lakini kama kawaida yake dola imeziba masikio kwani waliohujumiwa raia wa daraja la chini! Hatimaye walijitokeza wabunge mashuhuri kwa nafsi zao. Mabwana Msabaha na Kitwana Kondo. Mheshimiwa K..K. Alichofanya ni kuweka bayana yale yote ambayo yamekuwa yakikaririwa mara kwa mara juu ya kuwekwa kando madai na haki za Waislamu. Tulivyoelewa sisi ni kuwa Mheshimiwa K.K. alielekeza ushauri wake kwa serikali na chama chake kama alivyosema mwenyewe. Tulishangaa kusikia anajibiwa na msemaji wa taasisi ya kidini (Bakwata). Kishamajibu yenyewe yakawa hayasadifu hoja za bwana K.K. Mhesimiwa K.K. amedai Waislamu wanadhulumiwa, watuhumiwa wa Mwembechai wananyimwa dhamana kinyume na ubinadamu. Msemaji wa Bakwata anajibu! Hatuelewi alichosema ni kauli ya serikali ambayo ndiyo iliyoelekezwa hoja hizo au ni kauli yaBakwata kwa niaba ya serikali. Kama ndivyo kwa niaba ya serikali kama nani kwa serikali. Kauli ya msemaji wa Bakwata inatukumbusha hekaya ya miti, shoka na mpini. Kwa ufupi hekaya hii inatufundisha kuwa binadamu hawezi kuidhuru miti bila kuwa na shoka; aidha shoka haliwezi kuidhuru miti bila kusaidiwa na mti (mpini). Hapo hakuna shaka Mhe. K.K. kasema ukweli na msemaji wa Bakwata hakika hakusema kweli. Hataacha kusema kweli mmoja wenu mpaka jina lake liandikwe katika mlango wa Pepo. Rabbi wajaalie wasema kwelimiongoni mwa hao watakao andikwa majina yao katika milango ya Pepo. Lipo suala la Waislamu kwa makusudi kabisa kuzuliwa uongo kuwa wanakashifu dini za wenzao kupitia mihadhara. Hili lina historia ndefu. Imedaiwa itolewe tafsiri ya kashfa katika maneno ya kidini tangu enzi za utawala wa awamu ya pili lakini hakuna aliyethubutu kudai kuwa Mwislamu ana haki ya kusema Yesu (A.S.) Si Mungu. Akisema hivyo kakashifu. Siku zote Wakristo wanasema Yesu ni Mungu kinyume na Qur’an (5:17). Wakisema hivyo wao wanadumishaamani wala hawakukashifu dini za wenzao. Hivi karibuni alijitokeza kiongozi mmoja wa serikali na tafsiri yake ya kashifa na kusema; ‘kama mimi nina chongo halafu ukaniambia nina chongo, basi umenikashifu". Hiyo ni tafsiri potofu na yenye mwelekeo maalumu wa ileile hekaya ya miti, shoka na binadamu. Tafsiri ya bwana mkubwa huyu inapelekea kuwaambia watu wasikataze maovu na kuamrisha mema. Kwa maana mtu akikanusha Aya za Mwenyezi Mungu asiambiwe kakufuru maana kuwambia hiyo utakuwa umemkashifu kwa mujibu wa tafsiri hiyo. Suala hili hivi karibuni limepata wasema ukweli tena Wachungaji, Maaskofu. Kundi la Maskofu walikutana na kupeleka mapendekezo yao kwa Mheshimiwa Spika wa Bunge la Muungano. Kuhusu suala la kashifa maaskofu hao wanasema! Mheshimiwa Spika, kashfa za kidini ni msamiati ambao umeendelea kuwa kitendawili katika jamii yetu, na sisi tungependa kutoa mapendekezo yetu kama ifuatavyo. Mambo ambayo sio kashfa za kidini: Waislamu wanaposema Yesu si Mwana wa Mungu na wala sio Mungu, bado hawaja ukashifu Ukristo, kwa sababu hivyo ndivyo wanavyoamini, na wana haki ya kutangaza imani yao hiyo. Wakristo wanaposema Yesu ni Mungu sio kashifa dhidi ya Waislamu kwa sababu imani hii imekuwepo hata kabla ya Uislamu kuwepo duniani. Waislamu wanapoikosoa Biblia na kusema kuwa haifai, bado hiyo nayo sio kashfa dhidi ya Ukristo, kwa sababu kwa asili Kuran imekuwepo ili kuipinga Biblia. Pia Biblia ieleweke sio ya Wakristo kama inavyoelezwa. Hicho ni kitabu huru kwa ajili ya watu wote wenye dini na wasio na dini.’ Rejea Msema Kweli Toleo N. 011 la tarehe 24-30, Mei Uk.8. Wachungaji hawa wanachojaribu kufanya hapa ni kuweka bayana tu mambo ambayo hakika ndivyo yalivyo. Wamekuwa wajasimu kusema ukweli kupingana na tafsiri potofu zinazolazimishiwa katika vichwa vya watu ili ipatikanetu sababu ya kuhujumu watu wasio na hatia. Tunalohofia sisi ni kuwa, huenda mawazo na ukweli wa Maaskofu hawa ukapuuza na mawazo yao yakatupiliwa mbali kwa sababu sio kwamba waliyosema sio ya kweli, bali inawezekana wao si katika kanisa teule. Wanayosema Waislamu kwa ujumla, wanayosema Maaskofu hawa, na alichosema Mheshimiwa K.K. ni ukweli ambao kuupinga ni kuonyesha jinsi gani wewe unayepinga ulivyo kinyume na ukweli. Tunachotaka kukumbusha hapa ni kuwa kupingwa kwa wasema kweli na watendaji kwa ajili ya maendeleo ya Waislamu sio jambo geni. Kuna sualala nyaraka. Katika kipindi chaawamu ya pili tulishuhudia mlolongo wa nyaraka za kichungaji. Nyaraka hizi zilikuwa zinapewa nafasi ya kwanza katika vyombo vya habari hasa radio ya taifa RTD na magezetiyaUhuru na Mzalendo. Tunaukumbuka zadi waraka wa Baraza la Maaskofu wa Kiktoliki uliopewa anuani: "TAMKO RASMI LA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA MINTAARAFU KASHFA ZA KIDINI." Tamko hili lilitolewa tarehe 28.2.93. Tamko hilo ambalo lilikuwa na Lawama, vitisho nautabiri wa umwagaji wa damu lilipokelewa kwa taadhima na chombo cha serikali yaani Radio Tanzania na gazeti la CCM Uhuru. Radio Tanzania ilichukua tamko hilo kuwa sio tamko la kupuuzwa. Redio hiyo ililiimba tamko hilo katika vipindi vyake vya mazungumzo baada ya habari kwa siku tatu mfululizo. Japo hayo na yaliyomo kwa ujumla katika waraka autamko hilo hayana ukweli wowote lakini yanaenziwa na kupewa nafasi ya kwanza katika vyombo vya habari. Linalohitaji tafakuri ya kina zaidi ni kuwa, miaka mitano baadaye katika mwezi ule ule , Februari 1998, ametokea Paroko akadai kuwa Yesu katukanwa katika mihadhara siku ambayo kwa kweli hapakuwa na mhadhara. Lakini kiongozi wa dola Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Luteni Makamba akaitikia kilio cha Paroko. Akafuatia kuwaomba radhi waumini wa Kikristu na siku inayofuatia askari wenye silaha wakavamia msikiti, wakavunja mlango na kutupa mabomu ya machozi ndani ya msikiti. Lililo baya zaidi wakawaua Waislamu kwa makusudi, si kwa bahati mbaya bali: Lenga yule, bado, ongeza! Luteni Makamba kaitikia kilio cha Paroko. Limetimia lililoandikwa katika Tamko la Maasikofu Katoliki! (1993). Upo pia waraka wa Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Waraka huo ulioandikwa tarehe 22 Oktoba, 1992 alipelekewa Mhe. John Malecela akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais. Waraka huo ulisainiwa na maaskofu 18 ulijaa lawama za wazi kwa Mhe. Malecela binafsi, CCM na serikali. Rejea Motomoto la tarehe 16-31 Desemba, 1992 Ukurasa wa 12. Waraka huu uliweka wazi namna ambayo Mhe. Malecela, Chama na Serikali walivyoshiriki katika kukuza vurugu za kidini za Meru. Huu ni waraka wa maaskofu hakuna anayethubutu kudai kuwa ni wa uchochezi. Huu na ule wa juu ni nyaraka takatifu. Mwaka huu Ndugu Ponda ameandikia serikali, vyama na taasisi mbalimbali waraka unaoeleza wazi na kwa ushahidi kamili juu ya madai ya kweli na haki ya Waislamu tena ya katiba ya nchi. Subuhanalla! Huku umeitwa ni waraka wa uchochezi. Masikini Ponda anasakwa kama ngedere. Kisa kawasemea raia wa daraja la chini! Lakini kila mtu anakiri kuwa Ndugu Ponda kasema Ukweli. Hataachakusema ukweli mmoja wenu mpaka jina lake liandikwe katika milango ya Pepo. Hivi katika nchi hii kuna waraka ambao umefichua siri ya serikali na CCM kwa kupitia uongozi wa Mwalimu Nyerere kuhusu njama na mikakati iliyoandaliwa madhubuti katika kukandamiza na kuuhujumu Uislamu kama waraka (kitabu) wa Dr. John C. Sivalon M.M. : ‘Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania Bara 1953 hadi 1985? Je ni nani aliyethubutu hata kukiri tu kuwa kuna waraka au kitabu hicho. Hata kama limefichua siri kazi iliyoko ni kufunika kwa ambavyo warakamwingine wa Kanisa ulioiwa, "SIRI UKISOMA MPE MKRISTO" ulivyobainisha kwa kusema, "Kitabu chaKanisa na siasa hakikupaswa kutawanywa kwani kimefichua uhusiano wetu na serikali, ni wajibu wetu kufunika." Nyaraka kama hizi haziitwi za uchochezi maana zinatokana na wana wa nchi.Ole wao wasio na majina wanasakwa kama ngedere, wanawasemea kina nani katika nchi hii! Ukweli unauma lakini kuusema ni katika njia ya UADILIFU.Wako viongozi wa dola ambao wako makini sana kukosoa mambo yanayoigusa dola hasa wale wenyemajina ya Kiislamu ambao hupenda kutumia misikiti katika sala za Iddi na mabaraza yaIddi na Maulid kutoa kauli za serikali. Hakuna hata mmoja aliyethubutu kusema lolote kuhusu nyaraka hizo lakini wanatumia mimbari za misikiti kuwtisha Waislamu na kuwanyamazisha wasidai haki zao na kuambiwa hata kule kuuliwa Waislamu Mwembechai ni sawa kwani polisi walichokozwa. Wako wapiga kelele za kudai haki za wanawake na kudai kuwatetea dhidi ya unyanyaswaji wao. Wako wabunge wanawake, iko TAMWA na kuna jumuiya nyingi za kina mama. Kwa kweli hawa wanapotoa sauti zao kuhusu masuala ya wanawake, dola, makanisa, taasisi za kimataifa kupokea na kutilia mkazo. Enyi viumbe dhaifu, imekuwaje nyote mkaa kimya kama mlionyang’anywa ndimi wakati askari wa serikali ya CCM tenawanaume wanawanyanyasa, kuwadhalilisha, kuwatesa na kuwatia vilema wanawake wa Mbwembechai. Hatimaye limekuja suala la ‘PAROLE’. Yaliyotokea hayana haja ya simulizi nyingi. Kuna mambo mawili ya kujifunza au tunayofunzwa na tukio hili la serikali kuchagua Wakristu watupu katika hizo kamati za kusamehe wafungwa. Jingine na muhimu tunalokumbushwa : Ahadi ya Malimu Nyrere kulipa Kanisa lake fursa nzuri, agizo la Papa wakatialipotembelea Tanzania, kumbukeni maneno aliyosema pale uwanja wa ndege wakati anaondoka. Je, hatukumbuki? Papa alisema, "Naikabidhi Tanzania chini ya Ulinzi wa Bikira Maria". Na mwisho ahadi ambayo Mheshimiwa Rais Mkapa alimpa Mhasham Kadinal P. Pengo wakati wa sherehe za kumpongeza. Nadhani tunakumbuka maneno haya: "Tutasaidia na kuongoza nchi". Kwa misingi hiyo uchaguzi huo haukuwa wa bahati tu bali ni katikautekelezaji wa mikakati iliyoratibiwa kwa makini na muda mrefu tangu 1953 kama anavyotutanabahisha Dr. John C. Sivalon’ Kilichokosewa tu hapa ni kuwa waliokua wakila na kipofu safari hii wamemshika kipofu mkono naye kapiga kelele sasa lazima nyama ndani ya bakuli zihesabiwe. |
Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke Kujua
lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi Intifada
ndio jibu (2)
Kusema
ukweli ni sehemu ya uadilifu
Mafumbo
ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai Asiye
na elimu kwa mujibu wa Biblia
TAMTA
yaadhimisha miaka 36
Muumini
aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30 Lishe
: Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili
|