|
|
|
Wadai wauaji wafikishwe mahakamani Waliowadhalilisha wanawake waadhibiwe Wamuunga mkono Sheikh Bafadhil Na Mwandishi Wetu, Morogoro
WANAWAKE wa Kiislamu mjini Morogoro wamesema kwamba wanaungana na Waislamu kote nchini katika juhudi za kuondoa dhulma dhidi ya Waislamu na kwamba hawatarudi nyuma wala hawatahofu mpaka haki ipatikane. Aidha, wanawake hao wamesema kwamba wanalaani mauaji ya Waislamu yaliyofanywa na polisi Mwembechai na kile kitendo cha wanawake kudhalilishwa na kunyanyaswa mikononi mwa polisi na askari Magereza. Katika tamko lao baada ya mkutano wao wa Juni 28, 1998 nje ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mjini Morogoro, wanawake hao wamelaani matumizi ya mabavu katika uendeshaji wa shughuli za serikali na hususani kitendo cha askari polisi kuua wananchi, kuvamia na kunajisi Misikiti, kuwapiga na kuwatesa wananchi kinyume na taratibu za kisheria. Aidha, wamesema wanaungana na Masheikh na Maimamu wao wanaosimama kueleza na kupinga dhulma dhidi ya Waislamu. Katika nukta hii, wamesema wanamuunga mkono Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Sheikh Omar Bafadhil kwa jitihada anayoifanya kutetea haki za Waislamu. Awali, katika kuwasilisha mada ya mjadala, akina mama hao walisisitiza kwamba, muda wote Waislamu ni wagumu kwa makafiri na madhalimu wote, ila huwa wapole na wenye kuhurumiana wao kwa wao (48:29). Ni kwa ajili hiyo wamesema, wamelazimika kukutana kuzungumzia madhila waliyofanyiwa Waislamu wa Mwembechai. Wakitoa mada katika kongamano hilo, wanawake toka Msikiti wa Mafiga waliwakumbusha wanawake wa Kiislamu warejee historia ya Uislamu, waone jinsi wanawake walivyotoa mchango mkubwa katika kuuhami Uislamu. Pamoja na matamko yaliyotolewa katika kongamano, lakini kubwa zaidi, wanawake wamehimizwa wawe tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya dini yao.
|
TAHARIRI Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke Kujua
lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi Intifada
ndio jibu (2)
Kusema
ukweli ni sehemu ya uadilifu
Mafumbo
ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai Asiye
na elimu kwa mujibu wa Biblia
TAMTA
yaadhimisha miaka 36
Muumini
aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30 Lishe
: Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili
|