|
|
| Maoni
yetu
Tusianze kuulizana tena shida yenu nini TUNASHUKURU kwamba kila ambalo Waislamu wamekuwa wakilalamikia au kudai kama haki yao, wameliwekea kumbukumbu ambazo zaweza kuwasilishwa katika Mamlaka, Majlis na Mahakama yoyote duniani kama ushahidi. Huko Serikalini nako, kumbukumbu zipo. Waziri wa Elimu wakati fulani alishaandaa dokezo rasmi kutaka mfumo wa elimu uangaliwe ni vipi unakwaza sehemu ya jamii kupiga hatua. Dokezo hilo lilijadiliwa hadi katika vikao rasmi vya chama CCM. Na haya aliyozungumza Mbunge wa Kigamboni, Mh. Kitwana Kondo bungeni ni ushahidi na kumbukumbu nyingine. Alhamdulillah kumbukumbu za vikao vya Bunge la Tanzania litakuwa limerekodi hoja za Waislamu juu ya dhulma zinazofanywa dhidi ya Waislamu. Wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 1995, Waislamu waliulizwa shida yenu nini, matatizo yenu nini. Sasa baada ya yote haya pamoja na yale aliyosema Mh. Kitwana Kondo, Waislamu hawategemei kuulizwa tena "shida yenu nini". Mwananchi ni haki yake kupiga kura na yeyote ana haki kushawishi wapiga kura wamchague. Lakini sio katika vikao vya chakula vya kibarazani. Itakuwa ni jambo la kushangaza sana na kwa kweli kejeli kubwa kama baada ya "piga yule", baada ya "Mohamed Omar", baada ya "Chuki Athumani" na haya aliyosema Mh. Kondo, atatokea Mheshimiwa mwingine kuuliza "shida yenu nini". Shida yetu dhulma iondoke. Shida yetu walioua wakamatwe, wafikishwe mahakamani,. Shida yetu "Inquest". Mheshimiwa Kitwana Kondo kahitimisha, kaweka kumbukumbu. Msemo wa AN-NUUR isije semwa hatukusema. Tunayasema haya kwa sababu kesho na keshokutwa wasijeitwa watu katika vikao vya pembeni vya kahawa na visheti na kuulizwa shida yenu nini! Mkaanza kuongopeana hamjui na hamna watu wa kuwaambia. K.K. hamkumsikia? Waraka wa Ponda hamkuusoma? Abu Azizi naye vipi? Sivalon je! Yaliyomsibu Chuki Athumani hayawatoshi kuwa somo! Shida yetu dhulma iondoke lakini pamoja na haya, Mtume (s.a.w.) anasema: Muislamu ni yule ambaye Waislamu wenzake wamesalimika na ulimi wake. Sio kuwakera kila siku hata katika masiku yao ya furaha na sherehe. Na hivi karibuni tutawasikia katika Baraza la Maulid. Wamepigwa risasi watu na kuuliwa, wengine sasa vilema na wengine bado wanateseka magerezani. Chimbuko la yote ni kukiri kwao upweke wa Mungu Muumba na kuukataa Utatu. Wengi yamewakuta yaliyo wakuta kwa kukataa kwao kuimba wimbo wa "pambio". Heri yao walioimba kwa hiari yao waliimba kwa furaha na kunyanyua mikono juu. |
TAHARIRI Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke Kujua
lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi Intifada
ndio jibu (2)
Kusema
ukweli ni sehemu ya uadilifu
Mafumbo
ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai Asiye
na elimu kwa mujibu wa Biblia
TAMTA
yaadhimisha miaka 36
Muumini
aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30 Lishe
: Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili
|