|
|
| Agizo
la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani Kosa walisema
Yesu si Mtoto wa Mungu!
Ni Mzee Chata na Katambo Washindwa kutembea: WAZEE watatu, Mzee Chata; Mussa Katambo na Abdurahman Kipochi ambao walikamatwa kabla hata ya tukio la Mwembechai Februari 12, bado wanateseka rumande na afya zao zinaelezwa kuwa mbaya. Wazee hao ambao baadhi yao umri wao ni zaidi ya miaka 70 ni Maimamu na viongozi wa Misikiti ya Mtambani na Kibo, walikamatwa katika hatua za awali za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Yusuf Makamba kuitikia kilio cha Paroko Lwambano. Misikiti wanayoongoza wazee hao ni miongoni mwa ile ambayo Paroka Lwambano alidai kwamba inamtukana Yesu. Baadhi ya watuhumiwa wa kesi za Mwembechai walioachiwa hivi karibuni wamesema kwamba, matatizo makubwa yaliyoko magerezani ni huduma mbovu za chakula, maji na afya (matibabu). Kutokana na matatizo hayo; wamesema wazee hao ambao miili yao kutokana na umri wao haiwezi kuhimili mateso hayo, hali zao hivi sasa ni mbaya kiafya. Mzee Abdallah Mohamed Chata mwenye umri wa zaidi ya 75 alikamatwa Februari 10, 1998 kabla ya polisi kuvamia Msikiti wa Mwembechai na kuua Waislamu. Taarifa kutoka kwa mke wake zimeeleza kwamba hali yake ni mbaya kisi kwamba hawezi kutembea. Toka Juni 25, mwaka huu, Bi. Mkubwa huyo hajamuona mumewe kwani kila anapokwenda kumpelekea chakula huambiwa kwamba hawezi kunyanyuka na kuja mlangoni. Mzee Chata pamoja na Mzee Mussa Katambo mwenye umri usiopungua miaka 80 wanakabiliwa na shitaka la kuhubiri ‘kashfa’ kwa kusema Yesu si Mtoto wa Mungu na Biblia siyo kitabu cha kweli. Shitaka lingine ni kufanya muhadhara bila kibali cha polisi. Toka wamekamatwa wamekuwa wakinyimwa dhamana hadi leo. Akizungumza Bungeni Juni Mhe. Kitwana Kondo alieleza kwamba Mhe. Rais alishatoa maagizo Wazee wote, watoto na wanawake waachiwe. Haieleweki ni kitu gani kilichozuia utekelezaji wa agizo hilo la Rais. Au kama pengine kulikuwa na wazee zaidi ya hawa. wazee hao ni miongoni mwa ile ambayo Paroka Lwambano alidai kwamba inamtukana Yesu. Baadhi ya watuhumiwa wa kesi za Mwembechai walioachiwa hivi karibuni wamesema kwamba, matatizo makubwa yaliyoko magerezani ni huduma mbovu za chakula, maji na afya (matibabu). Kutokana na matatizo hayo; wamesema wazee hao ambao miili yao kutokana na umri wao haiwezi kuhimili mateso hayo, hali zao hivi sasa ni mbaya kiafya. Mzee Abdallah Mohamed Chata mwenye umri wa zaidi ya 75 alikamatwa Februari 10, 1998 kabla ya polisi kuvamia Msikiti wa Mwembechai na kuua Waislamu. Taarifa kutoka kwa mke wake zimeeleza kwamba hali yake ni mbaya kisi kwamba hawezi kutembea. Toka Juni 25, mwaka huu, Bi. Mkubwa huyo hajamuona mumewe kwani kila anapokwenda kumpelekea chakula huambiwa kwamba hawezi kunyanyuka na kuja mlangoni. Mzee Chata pamoja na Mzee Mussa Katambo mwenye umri usiopungua miaka 80 wanakabiliwa na shitaka la kuhubiri ‘kashfa’ kwa kusema Yesu si Mtoto wa Mungu na Biblia siyo kitabu cha kweli. Shitaka lingine ni kufanya muhadhara bila kibali cha polisi. Toka wamekamatwa wamekuwa wakinyimwa dhamana hadi leo. Akizungumza Bungeni Juni Mhe. Kitwana Kondo alieleza
kwamba Mhe. Rais alishatoa maagizo Wazee wote, watoto na wanawake waachiwe.
Haieleweki ni kitu gani kilichozuia
utekelezaji wa agizo hilo la Rais. Au kama pengine kulikuwa na wazee zaidi
ya hawa.
|
Maoni yetu:Tusianze kuulizana tena shida yenu nini Agizo la Rais Mkapa lapuuzwa:Wazee wa miaka 80 wateseka Gerezani Wanawake wasema hawatarudi nyuma mpaka dhulma iondoke Kujua
lugha ya Kiarabu sio kuujua Mwongozo wa Allah
Serikali isidhani kuwa Waislamu wa Tanzania wamelala usingizi Intifada
ndio jibu (2)
Kusema
ukweli ni sehemu ya uadilifu
Mafumbo
ya imani yabakie ndani ya Makanisa
Tamko la Wanawake wa Kiislamu mkoa wa Morogoro kuhusu kadhia ya Mwembechai Asiye
na elimu kwa mujibu wa Biblia
TAMTA
yaadhimisha miaka 36
Muumini
aliyeachiwa aeleza jinsi Waislamu wanavyoteswa Segerea
Wakwama kujenga msikiti kwa miaka 30 Lishe
: Mtoto anyonye maziwa ya mama miaka miwili
|