|
Na. 050 Jumatano Mei 31 - Juni 5, 2000 |
|
|
|
|
|
Supu na umuhimu wake mwilini CHAMOS, H.J Pamoja na kuwa tunaendelea na mfululizo wa matumizi ya jokofu, tutahama kidogo kuangalia vitu vingine na kwa majaaliwa ya manani tutaendelea na mada za "jokofu" hapo baadaye. Supu ni kitoweo kilicho katika hali ya majimaji chenye michanganyiko tofauti ya vyakula. Supu yaweza kuwa ya rangi au ladha yeyote kutegemea na matakwa binafsi. Mara nyingi supu huwa nyepesi na si yenye mabonge mabonge au vipande vya vyakula. Vipande vidogo vidogo vyaweza kuonekana iwapo wakati wa matayarisho, chakulainisha(blender) hakikuwepo. Supu moto huchukua nafasi ya chai mahala penye baridi au supu baridi mahali penye joto badala ya vinywaji baridi kama soda au maji ya matunda. Karibu aina zote za vyakula zaweza kutumika kutengeza supu. Ukianzia na vyakula vyenye asili ya wanyama (Mfano nyama na samaki), vyenye asili ya mimea Mfano matembele, bamia, mchicha, bilinganya na vinavyo fa nana na hivyo na vyakula vitokanavyo na mbegu za mimea mbalimbali mfano karanga, korosho, ufuta n.k. Asilimia kubwa ya supu ni za chumvi chumvi, ni nadra sana kupata supu zenye ladha ya sukari. Supu yaweza kunywewa mwanzoni au mwishoni mwa chakula kulingana na matashi yamtu. Kama supu inaywewa asubuhi ni bora ikanywewa kabla ya mlo ikichukua nafasi ya chai. Na kama nijioni ni vyema supu ikanywewa baada ya chakula kama kiburudisho. Faida za supu ni nyingi, kwa ufupi ni kama ifuatavyo: Supu husaidia kuamsha hamu ya kula kwa yule aliyekuwa hana na humuongezea hamu ya kula kwa yule aliyenayo. Na hii hasa hupatikana iwapo supu itakuwa na viungo mbalimbali vyenye harufu na ladha tofauti. Supu huficha ubaya wa ladha ya chakula iwapo itaandaliwa vizuri na kunywewa baada ya mlo. Iwapo itatokea mtu hakupendezwa na ladha au harufu ya chakula, supu humsaidia kuficha au kuisahau hadha hiyo. Hii humfanya aridhike kama vile tangu mwanzo amekula chakula kizuri (akipendacho). Kwa kuwa nivigumu kujua ni chakula kipi kitamfaa yupi, ni vyema kuwa na angalau supu pembeni kama ziada ya mlo. Supu hurahisisha mlo kuwa kamili hasa kwa wale wasioweze kutafuna au kula vyakula vya kawaida, mathalani, wagonjwa, wazee, vibogoyo au watoto. Supu hutengenezwa kwa kuchanganya vyakula mbalimbali ambavyo kwayo kwa kawaida mtu hawezi kuvila. Mfano kwa mtu amwenye meno mazima atakula nyama, atakuwa sawa na mzee au kibogoyo atakae kunywa supu yenye mchuzi wa nyama usioungwa. Kwa upande mwingine mgonjwa anaweza kukataa kula aina fulani ya chakula na labda pengine ni muhimu kwa afya yake, kinachoweza kufanywa ni kutengeneza supu kutokana na chakula hicho na kuichanganya na michuzi ya vyakula kisha kumpatia mgonjwa. Supu huburudisha na kuchangamsha huku ikikupatia virutubisho kedekede kwa ajili ya afya yako. Badala ya kununua vinywaji baridi vyenye kuburudisha lakini visivyonufaisha mwili zaidi ya kukufilisi, ni bora kujenga tabia ya kujiandalia na kunywa supu. Miongoni mwa faida za supu uwezo wake wa kupunguza kasi ya kuongezeka uzito wa mwili. Hii hutokea hasa kwa wale wanaotunza uzito wao usiongezeke, ambapo hupunguza kula na badala yake kunywa supu na kuifanya afya kundelea kuwa nzuri. Vile vile supu hupunguza matumizi na upotevu wa mabaki ya vyakula. Mara nyingi mchuzi utumikao kutengeneza supu auhitaji vyakula kama vilivyo. Mathalani nyama au samaki vyaweza kuchunwa na mifupa yake huchemshwa kupata mchuzi. Au badala ya kutupa mifupa au majani basi unayatumia tena. Hivyo ni muhimu ndugu wasomaji kujenga mazoea
ya kutumia supu.
|
YALIYOMO
TAHARIRI
Zanzibar wadai kuyumbishwa na Bara Serikali yatoa muelekeo wa Bajeti na kutangaza njaa Habari za ndani
SMZ haishughulikii mikarafuu -Maalim Seif Mwalimu Mkuu Msimbazi Mseto atishia kujiuzulu Hizi ni 'arobaini' za mapandikizi Waislamu Mbeya wamsusa Sheikh Mkuu wa BAKWATA Masheikh wa BAKWATA waongoza sherehe za kuwasimika makamanda wa vijana wa CCM MAKALA
Makala
MPASHO NASAHA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Habari za Kimataifaza Kimataifa Lishe
RIWAYA
Ambari, Mwakipesile wajitosa kugombea DRFA |
|
|
|
|