NASAHA
Na. 050 Jumatano Mei 31 - Juni 5, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Serikali yatoa muelekeo wa Bajeti na kutangaza njaa 

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imetoa muelekeo wa budget ya mwaka wa fedhaujao 2000/2001, na hapo hapo kutoa tahadhari ya njaa inayokabili nchi mwaka huu.

Taarifa hiyo ya muelekeo wa bajeti imetolewa na Waziri Daniel Yona mbele ya kamati ya Bunge ya Fedha, uchumi na Huduma za Jamii, tarehe Mei 29, 2000 kwenye ofisi za Bunge jijini. 

Taarifa hiyo imeonesha kwamba serikali itatumia jumla ya shilingi bilioni 1,389.5 kwa ajili ya maendeleo na matumizi ya kawaida. 

Pamoja nataarifa hiyo, Serikali pia imetangaza kuwa hali ya chakula nchini ni mbaya kuashiria kuwepo kwa njaa mwaka huu kuanzia mweziJulai. 

Taarifa hiyo ya kuwepo kwa njaa ilitolewa naWaziri wa TawalazaMikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Kingunge Ngombale Mwiru juzi Mei 29, mwaka huu wakati akiwasilishamuelekeo wa bajeti ya Wizara yake kwa kamati za Bunge za Fedha na Huduma za Jamii katika ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam. 

Mhe.Kingunge alieleza kuwa sababu ya hali hiyo ya njaa inatokana na upungufu wa mvua za msimu wa vuli ambao umeathiri umefifisha tegemeolakupata mavunano katikamaeneo ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Pwani,Lindi, Mtwara, Singida, Dodomana Tabora. 

Mhe. Kingunge alieleza kuwa kwa kuwa asilimia 80 ya wananchi wanaishi vijijini, ni vyema wananchi hao na wananchi wote kwa ujumla wao kuiwekea akiba ya chakula kitakachopatikana baada ya mavuno. Alishauri piawalewatakaopata mavuno machachewanunue na kujiwekea akiba. 

Taarifa ya Mhe. Kingunge ingawa ni ya kuhuzunisha, imepongezwa nabaadhi ya wananchi kwa kuwa imeweka wazi mambo ambayo huko nyumayalikuwa hayatolewi njemapema. 

Maka 1998 maeneomengi ya nchi yalikumbwa nanjaa kiasi cha baadhi yaokufa kwa njaa hiyo Wilayani Ulanga. Taarif aza njaa ya mwaka huo hazikuwekwa wazi mapema na hata taarifa za vifo hivyo awali zilianza kukanushwa. 

Juu
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI
Tahadhari ya Warioba juu ya rushwa isipuuzwe

Mkapa afanya ziara Pwani

CCM ‘inaweweseka’ - Sheikh

Zanzibar wadai kuyumbishwa na Bara

Serikali yatoa muelekeo wa Bajeti na kutangaza njaa

Habari za ndani
Wapinzani kusimamisha mgombea Urais mmoja 

SMZ haishughulikii mikarafuu -Maalim Seif

Mwalimu Mkuu Msimbazi Mseto atishia kujiuzulu 

Hizi ni 'arobaini' za mapandikizi

Waislamu Mbeya wamsusa Sheikh Mkuu wa BAKWATA 

Masheikh wa BAKWATA waongoza sherehe za kuwasimika makamanda wa vijana wa CCM 

Wakristo waishitukia CCM

MAKALA
Dini na siasa haviwezi kutenganishwa

Makala 
Mikutano ya Prof. Lipumba 'yaendelea' baada ya kuondoka 

MPASHO NASAHA
MATATA! MATATA!

Kalamu ya Mwandishi 
Wapinzani epukeni patupu 

MAKALA
CCM na sera za maendeleo (6)

Habari za Kimataifaza Kimataifa

Lishe 
Supu na umuhimu wake mwilini

BARUA

MASHAIRI

RIWAYA
Mapinduzi ya fikra - 4 

MICHEZO

  • Uchaguzi Yanga Julai
  • BATA yahimiza usajili michezo
  • 'Simba SC, Singida United baba mmoja mama mbali mbali' 
  • Tarimba akalia Kuti Kavu Yanga

  • Ambari, Mwakipesile wajitosa kugombea DRFA



       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita