|
Na. 050 Jumatano Mei 31 - Juni 5, 2000 |
|
|
|
|
RAIS Benjamin Mkapa ameuzuru mkoa wa Pwani ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia hali ya kiuchumi na kisiasa nchini.Akizungumzia hali ya kiuchumi Mh. Rais alieleza kuwa uchumi wa nchi umekuwa kwa kiwango cha kuridhisha. Katika ziara yake hiyo, Rais Mkapa ametembelea wilaya za Mafia, Kibaha, Bagamoyo, Kisarawe, Mkuranga na Rufiji ambapo katika baadhi ya sehemu hizo alikagua na kufungua miradi ya maendeleo. Rais Mkapa ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama tawala CCM aliwaeleza wananchi katika maeneo hayo kwamba uchumi wa Tanzania umekua kiasi cha kuwaridhisha wahisani ambao sasa wamekubali kuifutia Tanzania sehemu ya madeni yake. Mwenyekiti huyo wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ndiye pekee aliyechukua fomu za kuomba kugombea urais wa Jamhuri kwa tikiti ya chama hicho aliwahimiza wananchi kutumia rasilimali zilizopo na nguvu zao ili kujiletea maendeleo badala ya kutegemea wahisani. Msafara wa Rais Mkapa katika ziara hiyo ulipata 'bahati mbaya' ambapo gari moja katika msafara huo lilimgonga mwananchi mmoja na kusababisha kifo chake papo hapo. Marehemu alitambuliwa kuwa ni mtoto wa miaka 11, Hussein Rajab. Ajali hiyo ambayo ilisababisha watu wengine wanane kujeruhiwa ilitokea Kisarawe ambako Rais Mkapa alifanya ziara ya siku moja. Watu walioshuhudia ajali hiyo walieleza kuwa gari lililomgonga marehemu Hussein lililazimika kusimama ghafla jambo ambalo lisababisha magari mengine mawili katika msafara huo kugongana. Waliyataja magari hayo kuwa moja ni la Televisheni ya Taifa (TVT)na jingine ni la Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo yote yalikuwa yamewachukuwa waandishi wa habari. Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Dk. Ahmed Mtambo, iliwataja majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea saa tisa alasiri kuwa ni Bw. Mbaga na Bi. Mariam Komanya wa TVT, Bi. Nyambona Masamba, Juma Ngondai na Shabani Himba wote wa RTD. Wengine waliojeruhiwa, kwa mujibu wa Dk. Mtambo, ni Bw. Nuru Shija (Uhuru na Mzalendo), Bw. Suleiman Kumchaya (Ofisi ya Rais) na Bi. Jasmin Bagdela ambaye ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) unaoongozwa na mke wa Rais, Mama Anna Mkapa. Majeruhi wote hao walilazwa katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe na taarifa zilizopatikana juzi zilieleza kwamba hali za majeruhi hao zilikuwa zinaendelea vizuri. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Zanzibar wadai kuyumbishwa na Bara Serikali yatoa muelekeo wa Bajeti na kutangaza njaa Habari za ndani
SMZ haishughulikii mikarafuu -Maalim Seif Mwalimu Mkuu Msimbazi Mseto atishia kujiuzulu Hizi ni 'arobaini' za mapandikizi Waislamu Mbeya wamsusa Sheikh Mkuu wa BAKWATA Masheikh wa BAKWATA waongoza sherehe za kuwasimika makamanda wa vijana wa CCM MAKALA
Makala
MPASHO NASAHA
Kalamu ya Mwandishi
MAKALA
Habari za Kimataifaza Kimataifa Lishe
RIWAYA
Ambari, Mwakipesile wajitosa kugombea DRFA |
|
|
|
|