|
Na. 042 Jumatano Aprili 5 - 11, 2000 |
|
|
|
|
|
Ajenda mpachiko NA Y. KIJUKUU KARIBUNI wapendwa wasomaji wa safu hii ili tuchambue kwa uchache yale yaliyojitokeza katika jamii yetu juma hili. Leo tutalenga katika kile kinachoitwa siku ya wajinga duniani na ujinga ulivyojitokeza Tanzania. Ni siku chache tu zimepita tokea wajinga wa hapa nchini kama kweli wapo, walipoungana na wale wenzao wa duniani katika kusheherekea siku yao hii ambayo sijatambua ni nani aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya maadhimisho hayo kitaifa. Ni jambo la kusikitisha kuona asubuhi na mpema tu siku hiyo ya tarehe 1/4/2000, vyombo vingi vya habari nchini vikakosa mambo ya maana kuyatangaza au kuyaandika na badala yake vikaanza kutangaza na kuandika upuuzi ambao kwa namna moja au nyingine vimeonesha jinsi gani vyombo hivyo vilivyodhamilia kuiporomosha jamii hii masikini. Vilevile hatua hiyo ya vyombo vyetu vya habari vimeonesha jinsi gani vilivyokosa ubunifu wa mambo ili kuiletea jamii hii maendeleo hasa katika kipindi hiki kigumu kiuchumi, kijamii na kisiasa. Nahisi kinyaa kuelezea ni nini kilichotokea lakini ni vema nieleze angalau kwa ufupi kuhusiana na huo uvundo uliopeperushwa na vyombo hivyo. Umati wa Watanzania ambao mimi naamini kuwa si wajinga ulisikia kutoka katika radio na kujionea katika magazeti mbalimbali hoja za uongo ambazo kwa jinsi nionavyo zinaweza kuleta tafrani katika jamii yetu. Walianza kwa kusema kuwa Mkuu wa Mkoa anagawa fedha bure, mabasi ya daadala yatasafirisha abiria bure jijini, radio Clouds kufungwa rasmi, Mrema kurudi CCM, Serikali kumwaga vifusi katika mambonde yasumbuayo jijini na mengi mengine ambayo sitaki kuyataja. Vyombo vyote vilivyotangaza au kuandika hayo vimekosa watendaji wenye upeo wa kuona mbali na walishindwa au hawakutaka kabisa kuelewa jinsi gani uchovu wao huo ulivyoathiri umma wa Watanzania. Ni vema nikachukua fursa hii kuwakumbusha wanahabari kuwa wao wanao wajibu na jukumu zito dhidi ya kuliendeleza Taifa hili kwa kuandika au kutangazia wananchi yale yaliyo na msingi ili kutuletea maendeleo bila kujali tofauti zozote za kiitikadi zilizopo miongoni mwa wananchi wema. Pia kama miongoni mwa jamii ya waliokwenda shule ni vipi imeamua kuidharaulisha na kuifedhehesha fani yao kwa kutangaza uongo ambao baadye walikiri kuwa huo ulikuwa uongo. Hivi tujiulize kati ya wananchi waliosikiliza na ninyi mliotangaza na kuandika uongo ni kundi lipi lina haki ya kimsingi kuitwa wajinga? Aidha kwa upande mwingine inashangaza kuona Serikali inakaa kimya dhidi ya uchochezi, udhalilishaji na kebehi zilizotolewa na vyombo hivi bila kuvichukulia hatua za kinidhamu. Kimya cha serikali kinaashiria kufurahia hatua hiyo bila kujali wangapi wameathirika na hilo. Wanachi, hizi ni ajenda ndogondogo ambazo kwa kiasi kikubwa wataalamu wa mambo wamewaandalia ili ziwashughulishe na mkasahau ile ajenda yenu kuu mliyojiwekea. Msianze kung'aa macho, hii ndiyo Tanzania na ukweli wa vyombo vya habari mnaulewa hususan katika masuala ya siasa hapa nchini. Shikeni uzi uleule kwani ninyi si wajinga, waacheni watangaziane wenyewe kwa wenyewe. Hebu jiulizeni hivi kama kweli vinawapenda na kuwatakia kila la kheri,
vipi yale yanayosemwa na wapinzani hasa kuhusu maendeleo ya nchi wasiandike
au kutangaza badala yake wanaleta ujinga masikioni na machoni mwenu.
|
YALIYOMO
Tahariri
Mbukuzi
anguruma Chuo Kikuu:
Kuelekea
uchaguzi mkuu 2000:
Maalim Seif afunguliwa mashitaka ‘Tume ya Keenja’ haikufanya ilichoagizwa - Wananchi MPASHO NASAHA
Ushauri Nasaha
MAKALA
WAZO LA WIKI
MAKALA
Kalamu ya Mwandishi
Makala
MAKALA
Riwaya
Lishe
Madadi azionya timu za Ligi Kuu |
|
|
|
|