NASAHA
Na. 042 Jumatano Aprili 5 - 11, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
'Tume ya Keenja' haikufanya ilichoagizwa - Wananchi 

Na Waandishi Wetu 

ILIYOKUWA tume ya Jiji la Dar es Salaam imelaumiwa kwa kile kilichoelezwa na wananchi waliotoa malalamiko yao kuwa ni'iliacha kazi iliyoagizwa na kukimbilia mambo mepesi ya kuwaletea sifa haraka haraka."

Lawama hizo kwa tume hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Bw. Charles Keenja zimetolewa na wakazi wa Jiji la Dar es Salaamu kufuatia kero ya barabara na maeneo kadhaa ya Jiji hili kujaa maji kutokana na mvua za siku mojamoja zilizoanza kunyesha mwishoni mwa mwezi uliopita. 

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliozungumza na gazeti hili wamesema iliyokuwa tume ya Jiji iliundwa mahususi kushughulikia uchafu uliodaiwa kukithiri baada ya iliyokuwa Halmashauri ya Jiji wakati huo kusemekana imeshindwa kuliweka Jiji katika hali ya usafi. 

"Tuliambiwa Halmashauri(ya Jiji) ilikuwa imeshindwa kulisafisha Jiji, Meya na madiwani wake wakaondolewa... akaletwa Bw. Keenjana wakurugenzi wake, sasa hao wamemaliza kazi yao lakini mitaro yote imeziba", alisema mkazi mmojawa Jijini, aliyejitambulisha kwa jina la Gaspar Mrutu. 

Bw. Mrutu, ambaye anafanya biashara ya kuuza kadi navifaa vya kuandikia katika eneo la Posta mpya, ameilaumu iliyokuwa tume ya Jiji kwa "kujiingiza" katika mradi wa kuegesha magari (TPS) badala yakusafisha Jiji. 

"Mie nashangaa sana, tume badala ya kuzibua mitaro, mvua zikinyesha tusihangaike wao(tume) wamejiingiza kwenye parking system na sasa hata hizo sehemu za parking zinazo jaa maji" amelaumu Bw. Mrutu. 

Eneo la Posta Mpya, katika makutano ya Barabara za Azikiwe na Ali Hassan Mwinyi ni moja ya sehemu zilizojaa maji na kutokana na mvua hizo, na hivyo kusababisha usumbufu kwa wapita kwa miguu na pia magari yatumiayo barabara hizo. Kujaa maji huko kulisababisha hata kituo cha daladala ziendazo Mwananyamala, Kawe na Mwenge kilichopo mkabala na jengo la YWCA kuhamishwa kwa muda. 

Eneolingine liliojaa maji ya mvua hizo kutokana mitaro kuwa imeziba ni kipande cha Barabara ya Uhuru toka katika makutano ya barabara hiyo na ile ya Msimbazi hadikilipo kituo cha Daladala ziendazo Buguruni, Vingunguti, Gongo la Mboto na Pugu. 

Akiongea na mwandishi wa habari hizi katika eneo hili mkazi wa Jiji, Bwa. Maganyane, aliilaumu iliyokuwa tume ya Jiji kwa kukosa mipango mizuri na "mipango endelevu." 

Bw. Magayane ambaye alijitambulisha kuwa ni mtumishi wa serikali alisema tume ilitakiwa kutafuta eneo linalofaa kibiashara na kuwahamisha wafanyabiashara ndogondogo, Wamachinga, ambao kwa sasa wamefurika katika eneo la Shule ya Uhuru ikiwemo eneo lilo lojaa maji. 

"...Wafanya biashara hawa (Wamachinga) na wateja wao wote hawana sehemu za kutupa taka taka zao, badala yake wanazisokomeza katika hii hii mitaro ya maji, sasa mvua zikinyesha matokeo yake ndio kama hivi...." Alisema Bw. Magayane huku akionesha kwa kidole chake maji yaliyotuama barabarani hapo. 

"Hapo walipojenga shule ya City palifaa zaidi kuwa soko kuliko Shule. Lakini tume ya Keenja imefanya viroja kujenga shule sehemu ile iliyojaa vurugu za magari na wafanyabiashara" alilalamika Bw. Magayane. 

Akiendelea kuchambua kile alichokiita "mipango mibovu ya Tume ya Keenja" Bw. Magayane alisema mahali ilipojengwa Shule ya Sekondari ya City, palifaa kujengwa soko ambapo Wamachinga wale wangeeweza kuendesha biashara zao chini ya udhibiti wa Jiji. 

Alisema eneo lile ni kituo cha mkusanyiko wa watu watokao na kwenda sehemu mbalimbali za Jiji hivyo ni kivutio kwa wafanyabiashara. 

Bw. Magayane aliongeza kusema kuwa iwapo soko lingejengwa sehemu hiyo, basi kero ya Wamechinga katika eneo la Shule ya Uhuru ingemalizika. 

Mkazi mmoja wa Makumbusho Jijini ameeleza kuwa uamuzi wa serikali kuivunja iliyokuwa Halmashauri ya Jiji wakati ule "ulifanyika kwa papara." 

Mkazi huyu aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Mwinyimbegu na kwambaali wahi kufanya kazi katika Halmashauri ya Jiji, alisema ingawa Halmashauri hiyo ilijieleza sababu za kushindwa kulisafisha Jiji, serikali haikusikiliza. 

"Halmashauri(ya Jiji)haikuwa na vyanzo vingi vya mapato, ilipoomba bajeti toka wizarani haikupewa kiasi cha kutumia kama ilivyopanga..... na kilichokuwa kinakusanywa na Halmashauri, haikuruhusi wa kutumia bila idhini hata kama ni kuzibulia mitaro", alifafanua Mzee Mwinyimbegu. 

"Nimelitumikia Jiji mpaka wakati wa Kitwana Kondo, wakati mwingine Halmashauri ilikuwa ikilaumiwa hata kwa uharibifu wa barabara zilizochini ya Serikali kuu", alieleza mtumishi huyo wa zamani wa Halmashauri za Jiji. 

Amesema pamoja na tume ya Jiji kupewa kazi hiyo na kuongezewa muda mara kwa mara bado malundo ya takataka ya naonekana Jijini na barabara nyingi hasa katikati ya Jiji "zimefurika" maji taka. 

Mama mmoja anayemiliki kibanda cha kuuza maziwa Manzese amesema, "Ilipokuja tume ya Keenja tuliamini mambo yange kuwa mazuri na mifereji ya maji machafu ingeshughulikiwa...." 

Alipoulizwa ni kwa nini aliamini hivyo. Mama huyo ambaye alionesha woga mkubwa kutaja jina lake alisema, "sasa je, tume yenyewe imeundwa na Waziri Mkuu, na ilipewa mamlaka makubwa kweli(sana), kila kitu walikitoza kodi mpaka wenye vitumbua, na kwa kweli walikusanya hela nyingi sana." 

Bw. Norbert Mandago, muuza magazeti Posta ya Zamani ameeleza kuwa ilichokosea tume ya Jiji ni kujiingiza katika miradi mikubwa kama ile ya shule ya Sekondari ya City(sasa inaitwa Benjamin Mkapa) na uzio wa viwanja vya Mnazi Mmoja uliogharimu fedha nyingi. 

"....ndio maana tume washangaa tume, wamejenga majengo makubwa na kuweka vyoo pasipo kuweka utaratibu(mfumo) mzuri wa kupitisha maji machafu(majitaka), sasa maana yake karo na mabomba ya vyoo yanafurika",alisema Bwa. Mandago. 

Alisema yeye na wenzake walishangaa kuona Mwenyekiti wa Tume Bw. Keenja na tume yake wakisifiwa na akauliza, "au walisifiwa kwa kuongeza vyanzo vya kipindupindu na homa ya matumbo." 

Mfanyabiashara mmoja anayemiliki mgahawa uliopo Kariakoo amesema iliyokuwa tume ya Jiji ilikusanya fedha nyingi kama kweli. 

"Mimi ninaiomba Serikali ihakikishe tume hii ya Keenja inakabidhi kumbukumbu safi (sahihi)za mapato yake, na matumizi yake na balance (salio)", alisema mfanyabiashara huyo. 

Aidha alimalizia kwa kusema kuwa tume hiyo pia itaje takwimu za watu waliokufa kwa kipindupindu na homa ya matumbo kutokana na tume hiyo kushindwa kuzoa malundo ya takataka na kuzibua mifereji. 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Mnaodhulumiwa lindeni kura zenu

Mbukuzi anguruma Chuo Kikuu:
Wasomi mnatakiwa kukomesha dhuluma

Kuelekea uchaguzi mkuu 2000:
CUF yaiteka Dar

Maalim Seif afunguliwa mashitaka

‘Tume ya Keenja’ haikufanya ilichoagizwa - Wananchi

MPASHO NASAHA
WE THIO LAFKIYANGU TEENA!

Ushauri Nasaha
Namna ya kumfanya mtoto wako aweze kuzungumza

MAKALA
Kwanini tunataka CCM ing’oke madarakani

WAZO  LA  WIKI
Ajenda mpachiko

MAKALA
Kuporomoka kwa maadili  katika jamii yetu; Sababu na utatuzi wake

Kalamu ya Mwandishi
Ulaya yaiambia Afrika iboreshe demokrasia kabla ya kufutiwa madeni yake

Makala
Wasifu wa marehemu Sheikh Said Sabiq

MAKALA
Uchaguzi Mkuu Mwaka 2000 (5):
Wananchi mjiandae kulinda kura

HABARI ZA KIMATAIFA

Riwaya
Kisasi cha mauti -2

Lishe
Ni kwa jinsi gani wanawake wanapata utapiamlo

MASHAIRI

MICHEZO

  • Kajumulo atishia kuwanyang’anya Kibadeni Simba
  • Kipukuswa kufuata nyayo za ‘Mgosi’ Hazali
  • Hazali sio Yanga ni Simba ‘kindakindaki’

  • Madadi azionya timu za Ligi Kuu 


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita