NASAHA
Na. 042 Jumatano Aprili 5 - 11, 2000
Ukurasa wa mwanzo
Islam Tanzania
Matoleo yaliyopita
Maalim Seif afunguliwa mashitaka 

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Shariff Hamad na wanachama wengine wanane wa chama hicho jana walifikishwa mahakamani mjini Zanzibar wakituhumiwa kushambulia na kujeruhi na kupora silaha.

Katika mahakama ya Hakimu Mkazi Vuga, mbele ya Hakimu Abraham Mwampashi, ilidaiwa kwamba Maalim Seif na wana-CUF hao walifanya kitendo hicho Jumapili Aprili mbili mwaka hhuu katika eneo la Magomeni, mjini Zanzibar. 

Hata huyo imefahamika kwa mujibu wa kanuni kuhusiana na shughuli vyama vya siasa Zanzibar, chama cha siasa hakiwajibiki kuomba ruhusa toka Polisi kabla ya kukusanyika sehemu zisizokuwa wazi. 

Shambulio hilo na uporaji huo unadaiwa kutokea baada ya Polisi kuvamia mkutano wa faragha wa chama hicho cha siasa na kuuvunja kwa kile kilichodaiwa kuwa mkutano ule haukuwa na kibali cha serikali. 

Watuhumiwa wote nane (8) walikana mashitaka na wote wameachiwa kwa dhamana ya maandishi ya shilingi milioni 28 kila mmoja. 

Wanachama wa CUF wanaoshitakuwa kwa pamoja na maalum Seif ni Mbaruki, Hajj, Gharib Omar, Busi Amir na Muumii Abdallah. 

Wengine waliotajwa katika tuhuma hizo ni Ismail Juma, Rashidi Daki na Haji Hassan. 

Habari kutoka Visiwani humo zinaeleza wanaodaiwa kushambuliwa na wana-CUF hao ni askari polisi wanne akiwemo Asha Mohamed ambaye ni mkuu wa kituo cha Polisi cha Magomeni. 

Habari zaidi zinaeleza kuwa askari polisi hao waliingia katika mkutano wa ndani wa chama hicho uliokuwa ukihuhutubiwa na Maalim Seif. Katibu Mkuu huyo wa CUF alilazimika kufanya mkutano huo wa ndani baada ya chama chake kunyimwa kibali cha kufanya mkutano wa hadhara. 

Aidha silaha inayodaiwa kuporwa ni bunduki aina ya SMG na risasi 10 ambayo ilitoweka katika shambulio dhidi ya askari polisi hao. 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 18 mwaka huu itakapotajwa tena. 

Kesi hii imeanza kuwakabili wana-CUF hao siku moja tu baada ya Mahakama Kuu ya Zanzibar kusema kuwa wanachama wangine 18 wa chama hicho wanaotuhumiwa kwa uhaini wanayo kesi ya kujibu. 

Juzi Jumatatu Jaji Mkuu Msaidizi wa Zanzibar Garba Tumaka, aliyatupa maombi yote ya upande wa utetezi uliotaka kesi hiyo ya uhaini ifutwe na watuhumiwa wapewe dhamana. 

Katika uamuzi wake huo, Jaji Tumaka ambaye anatoka Nigeria, alisema Zanzibar ni dola yenye mamlaka ambayo ina mahakama, serikali na Baraza la wa wakilishi. 

Juu
 

YALIYOMO
 

Tahariri
Mnaodhulumiwa lindeni kura zenu

Mbukuzi anguruma Chuo Kikuu:
Wasomi mnatakiwa kukomesha dhuluma

Kuelekea uchaguzi mkuu 2000:
CUF yaiteka Dar

Maalim Seif afunguliwa mashitaka

‘Tume ya Keenja’ haikufanya ilichoagizwa - Wananchi

MPASHO NASAHA
WE THIO LAFKIYANGU TEENA!

Ushauri Nasaha
Namna ya kumfanya mtoto wako aweze kuzungumza

MAKALA
Kwanini tunataka CCM ing’oke madarakani

WAZO  LA  WIKI
Ajenda mpachiko

MAKALA
Kuporomoka kwa maadili  katika jamii yetu; Sababu na utatuzi wake

Kalamu ya Mwandishi
Ulaya yaiambia Afrika iboreshe demokrasia kabla ya kufutiwa madeni yake

Makala
Wasifu wa marehemu Sheikh Said Sabiq

MAKALA
Uchaguzi Mkuu Mwaka 2000 (5):
Wananchi mjiandae kulinda kura

HABARI ZA KIMATAIFA

Riwaya
Kisasi cha mauti -2

Lishe
Ni kwa jinsi gani wanawake wanapata utapiamlo

MASHAIRI

MICHEZO

  • Kajumulo atishia kuwanyang’anya Kibadeni Simba
  • Kipukuswa kufuata nyayo za ‘Mgosi’ Hazali
  • Hazali sio Yanga ni Simba ‘kindakindaki’

  • Madadi azionya timu za Ligi Kuu
     


       Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:Bonyeza hapa
    Au
    Andika barua  kwa: nasaha1420@yahoo.com

    Ukurasa wa mwanzo
    Islam Tanzania
    Matoleo yaliyopita