AN-NUUR
Na.164 Jamada Awal 1419, Agosti 28 - Septemba 3, 1998
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
Mahojiano kati ya CNN na Bwana Usama bin Ladin

Ulimwengu hivi sasa umegubikwa khofu ya kinachoitwa ugaidi wa kimataifa. Hofu hiyo imeongezeka zaidi baada ya kulipuliwa balozi mbili za Marekani nchini Tanzania na Kenya. Kufuatia milipuko hiyo, vyombo vya habari hapa kwetu na sehemu mbali mbali duniani vikiongozwa na Marekani vimekuwa vikihusisha milipuko hiyo na takriban kadhia nzima ya ugaidi na nchi au makundi ya Kiislamu yanayodaiwa kuwa na msimamo mkali wa kidini. Na zaidi mtandao huo wa habari umekuwa ukimtaja Bw. Usama bin Ladin kwamba ndiye kiongozi na mfadhili mkuu wa milipuko na ugaidi wa kimataifa. Kwa manufaa ya wasomaji gazeti hili, tunarudia kuchapisha mahojiano kati ya mtangazaji wa kituo cha kurushia matangazo cha CNN Bw. Peter Arnett na Bw. Usama Bin Ladin yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka wa jana (1997). Mahojiano hayo ya muda wa saa moja yalikuwa kama ifuatavyo:-

Arnett: Sijui unaweza kuieleza Amerika dosari kuu za ukoo wa kifalme unaotawala Saudi Arabia hivi sasa?

Bin Ladin: Kosa la kwanza la utawala wa Saudi Arabia na nchi nyingine za Kiarabu ni lile la kujitweza kwa Marekani, hii ni kusema tatizo letu kubwa ni Marekani, ndio Saudia ina Serikali lakini Serikali hiyo ni kama taasisi tu ya Marekani au tuseme Karagosi. Kwa kuitii Marekani,Serikali ya Saudi Arabia imekuwa ikitenda mambo dhidi ya Uislamu. Imeacha kuwaongoza watu kwa mujibu wa Qur’an. Kilichofuatia baada ya kukiukwa kwa msingi huu mkuu wa uongozi ni nchi kuhujumiwa kiuchumi, kijamii na kadhalika.

Arnett: Iwapo harakati za Kiislamu zitafaulu kulikamata bara Arabu, ni jamii ya aina gani mtakayounda nchini Saudi Arabia ukirejea mfano wa jinsi sheria zilivyokuwa wakati wa Mtume?

Ladin: Tunaamini, kwa rehema za Mwenyezi Mungu mtukufu Waislamu watashinda na dini ya Mwenyezi Mungu itakuwa juu ya uongozi katika bara hili.

Arnett: Iwapo harakati za Kiislamu zitafaulu kuishika Saudi Arabia, mtakuwa na msimamo wa aina gani kwa nchi za magharibi na je bei ya mafuta itapanda?

Ladin: Dini (ya Kiislamu) imekwishafafanua mahusiano baina ya mtu na mtu, wajibu wa muumini kwa Mwenyezi Mungu na mahusiano kati ya nchi ya Kiislamu na nchi nyingine katika nyakati za amani na nyakati za vita. Tukiangalia historia (ya Kiislamu) tunaona kwamba hata huko nyumba yalikuwepo mahusiano kati ya Taifa la Uislamu na mataifa mengine katika nyakati za amani na vita, kulikuwa na mikataba na masuala ya kibiashara.

Kuhusiana na mafuta, hii ni biashara ambayo bei yake itategemea uzalishaji na mahitaji. Tunahakika kwamba bei za sasa si bei halisi kutokana na ukaragosi wa Saudi Arabia kwa Marekani. Shinikizo la kuongeza uzalishaji wa mafuta ambalo Marekani imeiwekea Saudi Arabia limepelekea kuvurugika kwa soko la mafuta jambo linalosababisha kushuka kwa bei ya mafuta.

Arnett: Bwana Ladin, ninyi mmetangaza jihadi dhidi ya Marekani, je unaweza kuieleza Amerika kwanini mmefanya hivyo? Na je jihadi hiyo ni dhidi ya Serikali ya Marekani au dhidi ya Wanajeshi wa Marekani waliopo Saud Arabia? Na vipi kuhusu raia wa Marekani waliopo Saudia na wale waliopo Marekani?

Bin Ladin: Tumetangaza jihadi dhidi ya Marekani kwa sababu ya udhalimu na uovu wa serikali yake.

Marekani imekwishafanya mambo (mengi) ya kidhalimu ama yenyewe au kupitia kwa Mayahudi, wanaikalia kimabavu Palestina. Tunaamini kuwa Marekani inahusika kabisa na mauaji katika nchi za Palestina, Lebanon na Iraq. Kutajwa kwa Marekani kunanikumbusha watoto waliokatwa katwa vichwa na mikono yao katika mlipuko wa bomu uliotokea mjini Qana nchini Lebanon hivi karibuni.

Serikali ya Marekani imekosa hata hisia za huruma kufanya maovu ya kinyama kama haya. Kwa sababu hii na nyinginezo tumetangaza vita dhidi ya Marekani. Ni jukumu letu kuendesha jihadi hadi kuwaondoa Wamarekani katika nchi za Waislamu.

Arnett: Bwana Bin Ladin tusimulie vita ya Afghanistani na mlichokifanya wakati wa vita hiyo.

Bin Ladin: Mimi nimenufaika sana na vita (jihadi) ya Afghanistan, sidhani kama ningepata faida kama hiyo mahala pengine popote.

Pamoja na maguvu ya Urusi, tulikuwa tukisonga mbele kwa kujiamini. Mwenyezi Mungu aliitumia Marekani kwa manufaa yetu ambapo tulisafirisha zana za kivita kutoka Saudia mamia kwa mamia ya matani yakiwemo madoza, matingatinga, malori na vifaa ya kuchimbia mahandaki, hatimaye Taifa kubwa likasambaratishwa na kufutilia mbali ubabe wake. Ushindi wa Afghanistan umewaondolea Waislamu uchovu na woga.

Arnett: Hivi sasa Marekani inasema kwamba wewe bado unaendelea kuipa mapesa Afghanistan kwa ajili ya kudumisha kambi za mafunzo ya kijeshi kwa wanamgambo wa Kiislamu na kwamba wewe binafsi ndiye mdhamini wa ugaidi wa kimataifa.Lakini kuna wengine wanaosema wanakuona wewe kama shujaa wa ulimwengu wa Waarabu na Waislamu, sijui wewe mwenyewe unaweza kujielezea vipi?

Bin Ladin: Baada ya kusambaratika kwa Urusi kutokana na laana za Mwenyezi Mungu kwa kupigo walichopewa na mujahidina wa Afghanistan, Marekani inaongeza kibri na majivuno ikijiona kuwa ndio bwana wa ulimwengu na ikazua kitu kinachoitwa "new world order" (muundo mpya wa ulimwengu) inataka kuwadanganya watu kuwa inauwezo wa kufanya lolote ilitakalo lakini katu haiwezi. Ilituzushia mimi na wenzangu tuhuma nyingi tu zikiwemo hizo ulizozitaja. Marekani kutokana na kiburi chake imebuni mtindo wa kumuita gaidi mtu yeyote anayepinga udhalimu inaoufanya.

Yenyewe inataka ikalie tu nchi zetu na kuiba raslimali zetu huku ikitupachikia vibaraka wa kutuongoza kinyume na Atakavyo Mwenyezi Mungu na sisi tukubali tu, tukikataa basi inatuita magaidi.
 

Juu

YALIYOMO

TAHARIRI: Dawa ya ugaidi si kufanya ugaidi ndani ya ugaidi

Bakwata yalaani ubabe wa Marekani
Na Mwandishi Wetu

Wanakijiji wawapiga Polisi Olesiva
Na Mwandishi wetu, Arusha

Waislamu washinda kesi Same
Na Mwandishi Wetu, Same

Wasafiri ATC wadai ndege ya Jeddah inahujumiwa 
Na Mwandishi Wetu

KOSOVA: Bosnia nyingine

Mahojiano kati ya CNN na Bwana Usama bin Ladin

Historia ya damu za mashujaa Afghanistan

Msikiti wa Wagoma Kigoma wapata viongozi wapya
Na Suleiman Simba, Kigoma

Muhadhara wanguruma Masjid Hijaz
Na Said Shariff

Waislamu waitumie Misikiti ipasavyo
Na Ashraf Yusuph, Moshi

Mpango wa kudhibiti uzazi utawaangamiza wengi
Na Mwandishi Wetu

Hoja za kutofautisha Yesu na Issa ni udhaifu,  ni uzushi mtupu! - 3
Na Muhibu Said

Wanawake wa Kiislamu washiriki maonyesho ya kilimo
Na Habiba Swedi

Wanawake wa Kiislamu washauriwa kupigania haki zao
Na Habiba Swedi, Arusha

Africa Muslims Agency: Inavyohudumia jamii
Na Mwandishi Wetu

Kitengo cha Zakkah chasafirisha wanafunzi
Na Mwandishi Wetu

Kupinga kifo cha Yesu ni kumpinga Mungu?
Mahfudhi M. Mahfudhi

MAONI: Porojo za Ngatara -2

Zanzibar na  biashara ya utumwa
Na J. Hussein

Marekani ishitakiwe
Na Abubakar Msham

MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 3

Mafundisho ya Quran

Barua za wasomaji

Mashairi

Masomo ya dini ya Kiislam

Chakula na Lishe
 
 
 

 

 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org

Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita