|
Na.164 Jamada Awal 1419, Agosti 28 - Septemba 3, 1998 |
|
TAHARIRI Dawa ya ugaidi si kufanya ugaidi ndani ya ugaidi
Akiongea baada ya shambulio la Agosti 21, dhidi ya Sudan na Afghanistan Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Bibi Albright alisema kwamba magaidi waweza kujificha lakini hawawezi kuukwepa mkono wa sheria. Naye Waziri wa Ulinzi Bw. William Cohen akasema kwamba hapatakuwa na vikwazo vyovyote katika azma ya Marekani kulinda raia wa Marekani na maslahi yao, pamoja na maadili ya demokrasia na sheria. Maneno ya wakubwa hawa hayana tatizo; swali ni je; Marekani yenyewe inafuata sheria; na je; inajali demokrasia. Je, kuipiga Sudan na Afghanistan bila ya ushahidi wowote wa kisheria unaotambulika na jumuiya ya kimataifa ndio sheria? Kujichukulia mamlaka mkononi bila kujali kanuni za Baraza la Umoja wa Mataifa na Baraza lake la Usalama; ndio demokrasia na sheria! Marekani imekuwa ikishinikiza kuadhibiwa kwa Iraq na Libya kwa kile ilichodai nchi hizo kupuuza maamuzi ya Baraza la Usalama. Je, kwakujichukulia mamlaka kinyume na taratibu za Baraza la Usalama ndio Marekani imeliheshimu Baraza hilo! Je; kwa Marekani kulishinikiza Baraza la Usalama lisipeleke tume ya uchunguzi Sudan kuchunguza madai yake kwamba kiwanda ilichoshambulia kinatengeneza silaha za sumu, ndio demokrasia na sheria! Sheria gani inategemea ushahidi wa upande mmoja! Sheria gani ambapo mtuhumu anakuwa ndiye shahidi, hakimu na mnyongaji! Marekani inaituhumu Sudan, Marekani hiyo hiyo imesema inaushahidi kisha yenyewe inatoa hukumu na kutoa adhabu! Akitetea tendo hilo la kuipiga mabomu Sudan na Afghanistan msemaji wa upande wa sheria wa Marekani amesema kwamba hata mwaka 1986 Reagan aliipiga Libya baada ya bomu kulipuka katika disco huko Ujerumani ambapo wanajeshi kadhaa wa Marekani waliuliwa. Hata hivyo msemaji huyo hakueleza kwamba Reagan alipiga Libya kwa kuituhumu na kusema kwamba ina ushahidi (kama inavyosema kwa Sudan leo) kwamba Libya ndiyo iliyolipua bomu katika ukumbi huo wa Disco. Ambapo baadae iligundulika kwamba Libya haikuhusika.Ubalakala na ubabe wa aina hii hauwezi kutatua matatizo ya ugaidi, na ukosefu wa amani duniani. Kwa upande mwingine kama jambo ni ovu basi litakuwa ni ovu kama litafanywa na mkubwa au mdogo, masikini au tajiri, mtu binafsi au nchi. Na ni muhimu na ndio uadilifu wenyewe kwamba wahalifu wote wakemewe; vinginevyo utakuwa ni unafiki kukemea kosa linapofanywa na mnyonge na kufumba macho kosa hilo hilo linapofanywa na mwenye nguvu. Dawa ya ugaidi si kufanya ugaidi ndani ya ugaidi. |
TAHARIRI: Dawa ya ugaidi si kufanya ugaidi ndani ya ugaidi Bakwata yalaani ubabe wa Marekani
Wanakijiji wawapiga Polisi
Olesiva
Waislamu washinda kesi Same
Wasafiri ATC wadai ndege ya Jeddah
inahujumiwa
Mahojiano kati ya CNN na Bwana Usama bin Ladin Historia ya damu za mashujaa Afghanistan Msikiti wa Wagoma Kigoma wapata
viongozi wapya
Muhadhara wanguruma Masjid
Hijaz
Waislamu waitumie Misikiti
ipasavyo
Mpango wa kudhibiti uzazi utawaangamiza
wengi
Hoja za kutofautisha Yesu na Issa
ni udhaifu, ni uzushi mtupu! - 3
Wanawake wa Kiislamu washiriki
maonyesho ya kilimo
Wanawake wa Kiislamu washauriwa
kupigania haki zao
Africa Muslims Agency: Inavyohudumia
jamii
Kitengo cha Zakkah chasafirisha wanafunzi
Kupinga kifo cha Yesu ni kumpinga
Mungu?
Zanzibar na biashara ya utumwa
Marekani ishitakiwe
MAPENDEKEZO YA KATIBA YA SHIRIKISHO LA TANZANIA - 3
|
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtanzania.org