AN-NUUR
NNa.161 Rabiul Thani 1419, Agosti 7-13, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Mafundisho ya Qur’an

Ayatul Qursiyyuu 

Al-Baqarah Aya ya 255 

Allah hakuna Mola ila Yeye, ndiye Mwenye uhai wa maisha, Msimamia kila jambo; kusinzia hakumshiki wala kulala; ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini. Na ni nani huyo awezaye kuombea mbele Yake bila ya idhini Yake? Anayajua yaliyo mbele yao (viumbe) na yaliyo nyuma yao; wala hawalijui lolote katika elimu Yake ila kwa alipendalo. Enzi Yake imeenea mbinguni na ardhini wala kuvilinda hivyo hakumshindi; na Yeye ndiye aliye juu na ndiye Mkuu. 

Aya hii ambayo inaitwa kama Ayaatul-Kursy inayotowa maarifa kamili juu ya Allah, Sheikh Abdullah Saleh Farsi anaielezea kwa maneno yafuatayo:- 

Aya tukufu kabisa. Anahimizwa kila Mwislamu kuyaweka maana ya Aya hii mbele ya macho yake daima - ili asimwona Mwaddim wala Muakhkhir ila Mwenyewe tu Mwenyezi Mungu Subhanahuu Wataala. Na mahala pengi katika Hadithi za Mtume amehimizwa mtu kuisoma, kama (a) baada ya kutoa salamu katika sala (b) kabla ya kulala (c) anapotoka nje (d) anapoingia ndani (e) anapokuwa na khofu ya kuogopa vinavyoonekana na visivyoonekana. 

Pamoja na kuwa wanadamu wamekuwa mara kwa mara na kwa kipindi chote cha historia ya binadamu wakiwaabudu waungu wengine kinyume na Yeye Mwenyezi Mungu, bado ukweli wa mambo unathibitisha kuwa mwenye haki ya kuabudiwa ni Yeye Pekee. Kwani Yeye Pekee ndiye mwenye sifa zote za anayestahili ibada ikiwemo ile ya uhai wa milele tofauti na miungu inayobuniwa na binadamu ambayo yote huwa na mwanzo na mwisho wake kutegemea na ubunifu wa hao wanadamu wenyewe. Waungu wote wanaobuniwa na kupewa hadhi ya ibada wanaeleweka mwanzo wao na wengine mwisho wao. Jambo hili ni sawa kwa dini zinazoitakidiwa zina wafuasi wengi kama vile dini ya Kihindi (Hiduism), Kirusi au zile za wafuasi wachache wanaoabudu miti na mzimu ya mababu au hirizi na makaburi ya "watukufu" na "masharifu". 

Nabii Ibrahim (a.s.) kwa kuelewa sifa hiyo ya Allah aliwaambia watu wake kama ifuatavyo:- 

Na namna hii tulimuonesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi, 

Na ili awe miongoni mwa wenye yakini... 

Na usiku ulipomwingilia akaona nyota, alinena: "Nyota hii ni Mola wangu." Ilipotua alisema: "Sipendi wale wanaopotea....."Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayoyashirikisha. Mimi nimeuelekeza uso wangu kwa Yule aliyeziumba mbingu na ardhi...." (6:75-79). 

Aya hiyo (Kursyi) inaendelea kuwadhihirishia wanadamu sifa za Allah tofauti na waungu wao wengine. Waungu wa kibinadamu au wanyama wamekuwa wakisifika na sifa ya kuchoka pamoja na kuhitaji mapumziko ama kwa kupumzika tu au kulala. Hii ni sifa ya Mungu wa Biblia (anayeabudiwa na Mayahudi na Wakristo) kama tunavyosoma: 

Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibariki siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. (Mwanzo 2:2-3). 

Kwa kuwa Mungu wa Biblia ana sifa hiyo, tunasoma mfano mwingine anaopigiwa Mungu tena ndani ya kitabu cha Zaburi: 

Ndipo Bwana alipoamka kama aliyelala usingizi, kama shujaa apigaye kelele sababu ya mvinyo; (Zaburi 78:65). 

Kwa kweli sifa hii haimstahiki Mwenyezi Mungu (s.w.) kama tunavyofahamishwa zaidi ndani ya Qur’an: 

Na tumeziumba mbingu na ardhi na vilivyomo kati yao katika nyakati sita wala hayakutugusa machofu. (Qura’an 50"38). 

Allah anathibitisha zaidi kuwa ni haki yake ufalme wa mbingu na ardhi na kwa maana hiyo hata kama kuna kiumbe au kitu ambacho kinajipa au kinapewa sifa ya uungu basi kiumbe au kitu hicho ni sehemu ndogo tu ya millki hiyo ya Allah. Aidha ni kujidanganya kufikiria kuwa kiumbe hicho au kitu kuwa ni mshindani wa Allah wakati hana uwezo hata wa kudhibiti upumuaji wake au tumbo lake linapompinduka. 

Kutoka hapo Aya hiyo ikaelekea kwenye nadharia nzima ya uombezi mbele ya Allah siku ya hukumku. Waislamu na wasio Waislamu wanafahamishwa hapa kuwa hakuna Mtume, walii, sharifu, mtakatifu, Malaika na mtu/kitu ambaye atathubutu kusema chochote pasipo na idhini ya Allah. Hebu tupate picha zaidi ya hali ya uombezi itakavyokuwa katika Suratu Taha wakati Allah aliposema: 

Siku hiyo watamfuata muitaji asiye na upotofu. Na zitanyenyekea sauti kwa Allah Mwingi wa rehema na hutasikia ila mchakato tu wa miguu. 

Siku hiyo hautafaa uombezi (wa yeyote) ila wa yule atakayemruhusu Allah Mwingi wa rehema na kuiridhi kauli yake. (20:108-109). 

Kwa lugha nyengine aya hizi zinatuambia kuwa Muislamu wa kweli ambaye amefahamu aya hizi na ujumbe wake siku zote atajitahidi kumridhisha Allah kwa nia safi, kauli na vitendo anavyovikubali ili iwapo itabidi aidhinishiwe kupata uombezi lakini katu hatafanya mambo ya kimaajabu ajabu kisha akataraji kupata uombezi. 

Jambo la kumalizia na la kushangaza zaidi ni vipi wanadamu hawa wakajihalalisha uombezi huo huko Akhera wakati hawajui hata lini watafariki; sikwambii wataishia wapi baada ya kufufuliwa. Alilotudhihirishia Allah ni hilo la kututaka tufanya mema ili atufikishe kwa rehema Zake kupata mafanikio huko Akhera na kwa wale ambao watakuwa wamepungukiwa kidogo pamoja na jitihada yao ndio wanufaike na uombezi. Mtu kufanya maovu na kufa ndani ya maovu hayo na kisha kutaraji uombezi wa yoyote ni kujitangazia uwezo wa elimu ambayo hanayo. 

Ufalme wa Allah (Enzi) umeenea kote katika maumbile Yake mbinguni na ardhini na popote ambapo mtu atahisi hapajatajwa na aya hii. Ulinzi wa kweli na wa hakika ni wa Allah na siyo wa hirizi au vitu vinavyolingana na hivyo. Akitakacho Yeye ndicho kinachokuwa hata mtu akiwa hataki na ana uwezo wowote wa kibinadamu (kijeshi au kifedha), na asichokitaka; hicho hakiwi hata wanadamu wote wakilazimisha kuwa lazima kiwe. Ni kwa sababu ya imani hii tunayofunzwa na aya hii ndiyo Mtume (s.a.w.) akatutaka tuisome aya hii huku tukiamini katika sehemu tofauti. 

 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI  

Waislamu hawatokubali kusingiziwa mambo 
Na Mwandishi wetu 

Serikali ya Sudan yadhamiria kuleta amani ya kudumu 
Na Mwandishi Wetu 

Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto waingie ulokole 
Na Badru Kimwaga 

Wanawake Arusha watakiwa kutafuta elimu 
Na Habiba Swedi, Arusha 

Tamsa Tanga yapata viongozi wapya 
Na Masoud Mohamed 

Mjue Dr. Abuu Ameena Philips: Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika 

Duniani kwa ufupi 

Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma yake 
Na Mussa Ally Morogoro 

Nabii Isa Mwana wa Maryamu ni Yesu huyo huyo!! 

Kuanzishwa ‘Islamic Club’ ni ajenda ya siri inayoweza kuhatarisha amani Tanzania 

Agenda ya siri 
Na. Hassan Kimangale 

Hatua ya Rais kutengua uteuzi wa Parole ni ya kizalendo 
Na J. R. Msuya 

Serikali iwahurumie raia wake 
Na BADRU KIMWAGA  

Wanawake  Waislamu  Wilayani Masasi waanzisha Jumuiya 
Na Yousouf  S. Kayungilo, Masasi 

Kuhifadhika kwa mwanamke ni kuhifadhika kwa jamii 
Na Zuhra Tajiri 

Waislamu  wekezeni kwenye kheri -Mwinyi 
Na Mwandishi Wetu, Tanga 

Biashara ya ufuska yavamia Z’bar Polisi uchwara’ wanufaika 
Na Rajab Rajab 

Asimamishwa uongozi kwa kutoa fat’wa ya Hitma 
Na Nadhiru Ishengoma Wetu , Kahama 

Aqswa waazimia kufuata Qur’an na Sunna 
Na Mwandishi Wetu 

Mafunzo ya Quran  

Barua za wasomaji  

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)  

Masomo  

Chakula na Lishe  
  

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita