AN-NUUR
Na.161 Rabiul Thani 1419, Agosti 7-13, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma yake 

Na Mussa Ally Morogoro 

"NOTHING happens in politics which is not planned". Franklin Roosevelt, Rais wa zamani wa Marekani aliwahi kutoa kauli hiyo akimaanisha kwamba hakuna jambo lolote linaloweza kutokea katika uwanja wa siasa ambalo halikupangwa. 

Na mimi naungana na mwanasiasa huyo wa zamani wa Taifa hilo ambalo hivi sasa limejipachika upolisi wa dunia kiubabeubabe. 

Dhulma na ukandamizaji kwa Waislamu bila shaka ni vitu vilivyopangwa. 

Padri Collins anatoa ushahidi wa hilo katika maagizo yake kwa padri Heinzman amtaarifu Papa kwamba kanisa limekubali kujitolea tiketi kwa Bw. Julius Nyerere ya kwenda na kurudi Amerika. 

Naye Dr. Sivalon anaongezea kwa kusema kwamba ushindi mwingine "kukua kwa uhusiano kati ya viongozi wa Kanisa na wa Serikali na chama. Hali ambayo imefanya matendo, msimamo na uamuzi wa viongozi wa serikali ufanane mara kwa mara na mafundisho na mwelekeo wa Kanisa." 

Aidha, historia ya harakati za kanisa wakati wa Ukoloni inatupa ushahidi mwingine wa wazi kabisa na hasa tukirejea ‘Proceeding of CMS 1880-81 ambapo Church Missionary Society ilijipa kazi maalumu ya kuiokoa dunia toka kwenye giza, Uislamu na ujinga. 

Na dhulma hiyo ya kanisa ikaanza kuelekezwa katika nyanja ya elimu walizingatia umuhimu wake, kama Bwana Hamidou kama mmoja wa waandishi washuhuri wa vitabu anavyosema: ‘Elimu ikiwa na nguvu madhubuti zaidi ya mizinga, inafanya utekaji wa kudumu. Wakati mizinga inalazimisha mwili kutii, shule (elimu) inaziroga fikra. 

Na kwa nini Waislamu wahujumiwe kitaaluma? Zaidi ya umuhimu nilioutaja hapo juu vile vile taaluma sahihi itahofiwa kuwakomboa Waislamu toka katika utumwa wa aina zote, na kukifanya kitabu chao (Qur’an) kuwa mwongozo wao. 

Mmoja wa watu walioiona "hatari hiyo" ya Waislamu kuongozwa na kitabu chao, ni Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Sir Winston Churchill aliweka wazi kwamba, "So long as the Muslims will have this book (Qur’an) no body will rule them. But time will tell." 

Yaani iwapo Waislamu watashikamana na kitabu hiki (Qur’an) hakuna yeyote atakayeweza kuwatawala. Hata hivyo (lakini) wakati utatoa majibu. 

Tukiachana na khabari hiyo na turejee barua ya viongozi wa Elimu wa Manispaa ya Morogoro kwenda kwa walimu wakuu wa shule zote za msingi ndani ya Manispaa hiyo, kuwataka waorodheshe wanafunzi wote Wakatoliki wa darasa la saba mwaka 1998. 

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa makala hii siku chache zilizopita umegundua kuwa, zoezi hilo tayari limekwishafanyika, miongoni mwa shule hizo ni pamoja na shule za msingi Mafiga, Msamvu, Misufini, SabaSaba, Kihonda na Kigurunyembe. 

Baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule hizo, ambao hawakutaka kutaja majina yao wametibitisha ama kuiona barua hiyo katika shule zao au kutekelezwa kwa zoezi hilo rasmi. 

Katika baadhi ya shule wanafunzi wa madhehebu na dini nyingine waliondolewa wasiwasi juu ya jambo hili kwa kuambiwa kuwa "vijana hao wa Kikatoliki wana mtihani wao ndiyo maana wanaorodheshwa!? 

Kiuhakika zoezi hilo linatutia wasiwasi hasa tukizingatia sera za kanisa hilo hususan katika nyanja ya elimu, na historia yake nchini hapa kama tulivyotaja kwa uchache hapo juu. 

Ingawa juhudi za kuwapata viongozi wa elimu Mansipaa na wale wa kanisa Katoliki dayosisi ya Morogoro zinaendelea, lakini siyo siri kuwa barua hiyo ya viongozi hao ina agenda kubwa nyuma yake ambayo bado ni kitendawili. 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI  

Waislamu hawatokubali kusingiziwa mambo 
Na Mwandishi wetu 

Serikali ya Sudan yadhamiria kuleta amani ya kudumu 
Na Mwandishi Wetu 

Mwalimu alaumiwa kuwashawishi watoto waingie ulokole 
Na Badru Kimwaga 

Wanawake Arusha watakiwa kutafuta elimu 
Na Habiba Swedi, Arusha 

Tamsa Tanga yapata viongozi wapya 
Na Masoud Mohamed 

Mjue Dr. Abuu Ameena Philips: Mwanaharakati aliyewasilimisha askari 3000 wa Amerika 

Duniani kwa ufupi 

Barua ya Ofisa Elimu ina agenda nyuma yake 
Na Mussa Ally Morogoro 

Nabii Isa Mwana wa Maryamu ni Yesu huyo huyo!! 

Kuanzishwa ‘Islamic Club’ ni ajenda ya siri inayoweza kuhatarisha amani Tanzania 

Agenda ya siri 
Na. Hassan Kimangale 

Hatua ya Rais kutengua uteuzi wa Parole ni ya kizalendo 
Na J. R. Msuya 

Serikali iwahurumie raia wake 
Na BADRU KIMWAGA  

Wanawake  Waislamu  Wilayani Masasi waanzisha Jumuiya 
Na Yousouf  S. Kayungilo, Masasi 

Kuhifadhika kwa mwanamke ni kuhifadhika kwa jamii 
Na Zuhra Tajiri 

Waislamu  wekezeni kwenye kheri -Mwinyi 
Na Mwandishi Wetu, Tanga 

Biashara ya ufuska yavamia Z’bar Polisi uchwara’ wanufaika 
Na Rajab Rajab 

Asimamishwa uongozi kwa kutoa fat’wa ya Hitma 
Na Nadhiru Ishengoma Wetu , Kahama 

Aqswa waazimia kufuata Qur’an na Sunna 
Na Mwandishi Wetu 

Mafunzo ya Quran  

Barua za wasomaji  

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)  

Masomo  

Chakula na Lishe  
  

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita