AN-NUUR
Na.159 Rabi' Awal 1419, Julai 24 - 30, 1998
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya Z'bar 

Na Mwandishi Wetu 

Wabunge kutoka Zanzibar wameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani kuwafichua vigogo na watu wazito katika jamii wanashiriki katika biashara ya madawa ya kulevya kuliko kuhangaika na vijana wa mtaani, huku wanaowapa madawa hayo wakiachwa. 

Aidha, Wabunge hao wametahadharisha juu ya uwezekano wa kuwepo kile walichokiita ‘Italian Mafia’ ambacho ni chanzo cha uhalifu wa kupangwa. 

Akiongea Bungeni hivi karibuni, Mbunge wa Jimbo la Mlandege Mhe. Fatma Said Ali alisema kwamba, hivi sasa biashara ya madawa ya kulevya imeshamiri sana Zanzibar na vijana wameharibika. 

Akaongeza kusema kwamba shughuli hii ya kuuza na kutumia madawa hayo hufanyika wazi katika maeneo ambayo yamebatizwa na kuitwa Argentina, Uruguay, Peru n.k. Aidha Mbunge huyo akasema katika maeneo ya Vikokotoni shughuli hizo ni maarufu. 

Katika hali hiyo ya kushamiri biashara hiyo na kufanyika kwa wazi kiasi hicho Mhe. Fatma Saidi Ali aliitaka Serikali iwabane vijana hao waeleze nani anawapa madawa hayo. 

Hoja ya Mhe. Mbunge Fatma ni kwamba vijana hao kwa hali zao hawana uwezo wa kupata fedha za kusafiri nje na kuyaleta madawa hayo ambayo huuzwa kwa fedha nyingi. 

Baadhi ya Wabunge wakiitahadharisha serikali kwamba pamoja na kuwa Utalii umekuwa ukiingizia serikali ya Zanzibar mapato lakini ipo haja ya kuangalia aina ya watalii wanaoingia Zanzibar. Mheshimiwa Hashul Nassor Ali alionya kwamba ipo hatari kuharibikiwa kama tahadhari haitachukuliwa. 

Akisherehesha nukta yake akinukuu maneno ya tahadhari ya Cris Maris kama yalivyoandikwa katika jarida la "Living Africa" la Shirika la Ndege la Aliance. Sehemu ya tahadhari hiyo, inazungumzia, "Rumours about the Presence of the Italian Mafia activities on the Island and some coastal parts are refugees of Western hippies and travellers escaping from the World." 

Kwa nukuu hiyo Mhe. Hashul aliitaka serikali kwamba pamoja na mapesa inayopata lakini ichukue tahadhari kubwa. 

Juu 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI 

Maoni yetu: Umakini wa Wabunge unatia wasiwasi 

AGIZO LA MANISPAA KUPEWA MAJINA YA WANAFUNZI WA KIKATOLIKI 
Na Mwandishi wetu, Morogoro 

Madai ya Ali Ameir kuhusu Chuki yakanushwa 
Na Mwandishi wetu 

AN-NUUR  kwenye Internet 

Mwanamuziki Nyota CAT STEVENS asimulia alivyosilimu 

Watakiwa kuacha kuwatuma watoto mitaani 
Na. Kassim Juma 

Kijana wa Kibarbaig aliyejitolea kupigania dini yake 
Na. Ali Njuki 
 
MAKALA: Zanzibar na tamasha la filamu
Na Said Mzee

'Waislamu wenye sisa kali'
Na. Ustaadh A. S. Fundi 

MAKALA: Maisha ya ndoa kwa Muislamu - 2
Ustaadh Khamis Suleyman Nassoro, Usangi, Mwanga - Kilimanjaro

Pongezi hizi za nini?

Mjibuni Mwinjilisti Kusupa msitukane 
Na Paskal Msemakweli

BARUA YA WAZI KWA WABUNGE

Vigogo wahusishwa na madawa ya kulevya Z'bar
Na Mwandishi Wetu

Da’awa Handeni yashika kasi
Na Ibn Muhammad

Kongamano la vijana wa Kiislamu Masjid Nuur Dar
Na Mwandishi Wetu

Mafunzo ya Quran 

Barua za wasomaji 

Mashairi - uzawa wa Mtume (S.A.W)

Habari za Madrasa 

Masomo 

Chakula na Lishe 
 

 

 
 Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu:
Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita