|
|
|
KUNA watu ambao wana kawaida ya kutoa hoja pofu dhidi ya jambo walisilolipenda au wasilolijua undani wake. Hoja pofu ni hoja inayotolewa kwa kuangalia upande mmoja tu wa jambo bila ya kuzingatia upande mwingine. Watu wenye hoja pofu huona weusi (ubaya) wa jambo bila ya kuona weupe (au uzuri) wake. Angalia taswira iliyoambatanishwa hapa. Unaona viduara vitatu vyeusi vilivyokatwa. Je, unaona taswira yoyote nyingine zaidi ya viduara ? Kwa wengi ni vigumu kuona kitu kingine. Hebu weka fikra yako katikati ya viduara hivyo na utagundua kuwa mchoraji ametaka uone umbo la pembetatu nyeupe iliyochomekwa katikati ya viduara vitatu. Umeiona ? Mfano mzuri wa watu wanaoona weusi wa kitu bila ya kuona weupe wake ni wale wanayoishangaa amri ya Mungu, ya kuwataka wezi kuwakata mikono. Watu hawa hukurupuka na kudai kuwa Uislamu ni dini ya kikatili isiyo na upendo wala huruma. Hii ni hoja pofu. Ni kweli kwamba kumkata mwizi mkono sio tendo zuri, lakini kuiba nako sio kuzuri, na ni kwa sababu hii ndio maana wale wanaoitwa "wananchi wenye hasira" huwaua watuhumiwa wa wizi kwa kuwabonda na kuwachoma moto. Sheria ya kukata mkono haitekelezwi mpaka tuhuma iwe ya kweli, na kuna kiwango cha wizi kinachoruhusu sheria hii itekelezwe, sio kama hii ya kuwaoka vibaka wa mikufu mitaani na kuwahifadhi wa ‘benki’ na mamilioni ya fedha za umma kwa kesi zisizokuwa na mwisho mpaka zinasahaulika na watuhumiwa kuonekana wakiendelea ‘kupeta’ na ‘kutanua’. Nenda kaone mambo yalivyo kule ambako sheria ya kukata mkono imesimama. Kitakachokushangaza ni kwamba hutakutana na mtu mwenye kigutu hata mmoja, kwa sababu hakuna mwenye hata fikra ya kunyoosha mkono wake kuchukua cha mwenzie au cha umma. Uislamu unaihurumia jamii nzima, na sio mwizi mmoja mmoja. Izingatiwe pia kwamba hoja dhidi ya Uislamu si hoja dhidi ya Waislamu, bali ni hoja dhidi ya mwenye ulimwengu wake na viumbe wake, yaani Mwenyezi Mungu, ambaye anasema: "Je, anayejua ya kwamba yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako ni haki (akayafuata) ni kama aliyekuwa kipofu ? Wenye akili ndio wanaozingatia". (Qur’an 13:19) |
YALIYOMO
TAHARIRI Tuacheni na njaa yetu msituongezee silaha Serikali
yakumbushwa kujiunga OIC
Polisi walizingira nyumba yangu usiku wa manane - Sheikh Mbukuzi Wafungwa waomba Futari na Vikoi Macho
ya shutuma
Hoja
pofu
Ubaguzi katika mfumo wa elimu nchini: Chuo Kikuu chasikia kilio cha wanawake 'Vichupi'
vya nini Kimiti?
Mjadala
wa Katiba na haki za Waislamu
Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 3
Waliochukuliwa
utumwa Uarabuni
Teknologia:
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (4)
Kuweni wabunifu muinue taaluma - Wito TVZ na kipindi cha 'Wasemavyo' Kesi ya Waislamu Mwembechai: Mashahidi washindwa Wanyimwa fursa ya kuswali Ijumaa Mwanza Shule ya Bakwata yafungiwa Tanga Mafunzo
ya Qur'an
|