AN-NUUR  Na.174 Rajab 1419, Novemba 6 - 12, 1998 
 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
Macho ya shutuma
Na Abu Halima Sa Changwa

KUNA suala linalonishinda kuelewa. Shangazi yangu Fatuma haendi kuuza chakula. Nilipomwuliza, kwa nini, akaniambia ameacha kwa sababu chakula chake humwagwa. Nilipomwuliza, na nani? Akaniambia "na SERIKALI". 

Siku nyingine, nikamuliza mama, mbona siku hizi hatuendi Ubungo kwa Anko. Akaniambia, nyumba ya Anko imevunjwa. Nikamuuliza, na nani? Akaniambia, "na SERIKALI". 

Halafu. Nikaamuliza baba, lini tutaenda Nzasa kwa babu ? Akaniambia, nyumba ya babu yako imechomwa moto. Nikamuuliza na nani ? Akaniambia, "na SERIKALI". 

Nikamuuliza mama, mbona siku hizi tunakula mara moja tu, na baba haleti vile vyakula vizuri vizuri, na baba amekuwa mkali kama nini. Mama akaniambia, baba yako kapunguzwa kazi na hajalipwa pesa zake. Nikamuuliza na nani? Akasema "na SERIKALI". 

Nikamuuliza kaka Sudi kwa nini hakuninunulia nguo za sikukuu kama alivyoahidi. Akaniambia walimu hawajapewa hela zao miezi mitatu. Nikamuuliza wanatakiwa wapewe na nani ? Akaniambia, "na SERIKALI". 

Nikamuuliza kaka Hashimu, mbona siku hizi hatuendi kuswali Mwembechai ? Akaniambia, Waislamu wanaogopa kuvamiwa na kupigwa mabomu, na sisi hatuwezi kwenda. Nikamuuliza mvamizi huyo ni nani ? Akaniambia, "ni SERIKALI". 

Nikashangaa hata kaka Athumani naye hapeleki tena karanga zake na pipi Mwenge. Naye pia aliniambia kibanda chake kimevunjwa na huyo huyo SERIKALI. Kha! 

Ninachoshangaa ni kwamba, huyu SERIKALI, hata kama ni jitu kubwa, hakuna mtu anayeweza kupambana nalo ? Rais wetu hawaambii polisi wamsake huyo SERIKALI? 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
TAHARIRI  
Tuacheni na njaa yetu msituongezee silaha 

Serikali yakumbushwa kujiunga OIC 
Na Mwandishi wetu 

Polisi walizingira nyumba yangu usiku wa manane - Sheikh Mbukuzi 

Wafungwa waomba Futari na Vikoi 

Macho ya shutuma 
Na Abu Halima Sa Changwa 

Hoja pofu 
Na Abu Halima Sa Changwa 

Tafuteni ufalme wa kisiasa 

Ubaguzi katika mfumo wa elimu nchini: Chuo Kikuu chasikia kilio cha wanawake 

'Vichupi' vya nini Kimiti? 
Na. Said Rajab 

Mjadala wa Katiba na haki za Waislamu 
Na Masoud Mohammed Mbogo 

Mdahalo kati ya Waislamu na Wakristo- 3 
Na Nandenga wa Mkomidachi 

Waliochukuliwa utumwa Uarabuni 
Na Hassan Omar 

Madrasatul Maamury Islamiya 

Teknologia: Jifunze Kuunganisha Kompyuta (4) 
Na Hassan Omar 

Kuweni wabunifu muinue taaluma - Wito 

TVZ na kipindi cha 'Wasemavyo' 

Kesi ya Waislamu Mwembechai: Mashahidi washindwa  

Wanyimwa fursa ya kuswali Ijumaa Mwanza 

Shule ya Bakwata yafungiwa Tanga 

Mafunzo ya Qur'an  
Shetani anawaogopesha wenye mali kutoa 

Barua za wasomaji  

Masomo ya dini ya Kiislam  

Chakula na lishe 

Mashairi 

Matangazo 
 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita