|
|
| Wafungwa
waomba Futari na Vikoi
WAKATI mwezi wa Ramadhani ukikaribia wafungwa wa gereza la Karanga mjini Moshi wamewaomba Waislamu wawasaidie futari, vitabu vya dini na vikoi vya kuswalia ili nao watekeleze wajibu wao kidini. Wamesema kwamba kutokana na ufinyu wa fedha za serikali hawapati sukari na futari kwa ujumla na mchele kwa ajili ya daku. Kwa hiyo wamewaomba Waislamu wenye moyo wa kusaidia wawasiliane na uongozi wa gereza ili kujua taratibu za kufikisha misaada yao. Katika risala yao kwa Sheikh wa Wilaya ya Moshi, wafungwa wa gereza kuu la Karanga wamesema kwamba wanapata ugumu katika kusimamisha swala kutokana na sare wanazovaa, hivyo wakaomba wapelekewe vikoi. Aidha, wameomba wasaidiwe masahafu tafsiri ya Kiswahili na watembelewe mara kwa mara kupewa ujumbe wa Allah. |
YALIYOMO
TAHARIRI Tuacheni na njaa yetu msituongezee silaha Serikali
yakumbushwa kujiunga OIC
Polisi walizingira nyumba yangu usiku wa manane - Sheikh Mbukuzi Wafungwa waomba Futari na Vikoi Macho
ya shutuma
Hoja
pofu
Ubaguzi katika mfumo wa elimu nchini: Chuo Kikuu chasikia kilio cha wanawake 'Vichupi'
vya nini Kimiti?
Mjadala
wa Katiba na haki za Waislamu
Mdahalo
kati ya Waislamu na Wakristo- 3
Waliochukuliwa
utumwa Uarabuni
Teknologia:
Jifunze Kuunganisha Kompyuta (4)
Kuweni wabunifu muinue taaluma - Wito TVZ na kipindi cha 'Wasemavyo' Kesi ya Waislamu Mwembechai: Mashahidi washindwa Wanyimwa fursa ya kuswali Ijumaa Mwanza Shule ya Bakwata yafungiwa Tanga Mafunzo
ya Qur'an
|