|
|
| Kuchomwa
nyumba za wananchi; serikali yasema:
Wanauza viwanja
ndani ya Msitu
TAARIFA ya serikali ambayo ilitolewa hata kabla ya wananchi wa Nzasa kuchomewa nyumba zao imeeleza kwamba wananchi hao wamevamia na kuingia ndani kabisa ya eneo la hifadhi ya msitu. Wananchi hao imedai taarifa hiyo kwamba mbali ya kujenga nyumba, wanachoma mkaa, kupasua mbao, kung’oa maboya (Beacon) za mpaka wa eneo hilo la hifadhi na hata kuuza viwanja na mashamba. Taarifa hiyo ya serikali ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Capt. J. C. Yamungu baada ya wananchi wa Nzasa kupeleka malalamiko yao kwa Kamati ya Msaada wa Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Awali, baada ya wananchi hao kuamriwa kuhama, waliomba msaada kupitia vyombo vya sheria. Kamati ya Msaada wa Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ililifikisha suala hili katika Wizara husika (Wizara ya Maliasili na Utalii). Wizara hiyo iliiarifu Kamati hiyo kwamba wananchi hao wasingeondolewa kwani vijiji vyao viko nje ya mipaka ya hifadhi ya msitu. Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Yusuf Makamba aliripotiwa na vyombo vya habari Julai 25, 1998 akitoa tishio kwamba wananchi hao watahamishwa bila kujali habari za mahakama. Agosti 1, 1998 Mkuu wa Wilaya Capt. Yamungu alitoa ilani ya kuwataka wananchi hao waondoke. Kufuatia ilani hiyo, wananchi wa Nzasa walikwenda kutaka msaada katika vyombo vya sheria. Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kwamba Jumanne Oktoba 6, 1998, wajumbe wa Kamati ya Msaada wa sheria walikwenda kuonana na Mkuu wa Wilaya Capt. Yamungu ambapo aliwaonyesha ramani inayoonyesha eneo lililovamiwa na wananchi. Hata hivyo, wajumbe hao hawakuweza kuandamana na Mkuu huyo wa Wilaya kwenda kushuhudia eneo linalodaiwa kwamba wananchi wamevamia mpaka ndani kabisa ya Msitu. Kilichofuatia baada ya hapo ni zoezi la uchomaji moto nyumba za wananchi hao. Zoezi ambalo limeteketeza nyumba na akiba ya chakula. |
YALIYOMO
TAHARIRI
Waislamu wasisitiza: Nyumba ya Waziri
Mkuu ni ya Waislamu
Kuchomwa nyumba za wananchi
Maoni Yetu:
Nguruwe marufuku Kinondoni – Tume
Watanzania waanzisha Baraza la Waislamu
Marekani
Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie
mauaji ya Mwembechai
‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’
Makala ya Kimataifa
Afghanistan washindi dhidi
ya uvamizi karne zote
MAKALA:
Tujikwamue na janga la utwaghuti
MAONI:
MAKALA:
Tufuate Uislamu kwa vitendo
na siyo kwa maneno -2
Tusihalalishe mauaji ya
raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’
Historia ya sayansi na tiba
Msiwageuze watoto ombaomba
MAKALA YA JAMII:
Sensa ya majaribio: Wananchi watofautiana
na serikali
Uislamu ulivyoingia Zanzibar -3 Mwembechai wageuka Hame,
Bado walindwa na polisi
Waislamu Moro waendelea kusaidia
wagonjwa
Mjadala wa Katiba ya Shirikisho
kuzinduliwa Dar Jumapili
Walimu wa dini Tanga wapokea
Baiskeli
Mafundisho ya Quran
Chakula na Lishe
|