AN-NUUR 
Na.170 Jamadul Akhir 1419, Oktoba 9 - 15, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
 
TAHARIRI
Tutaendelea kudhalilishwa mpaka lini ?

QUR’AN Tukufu inatuambia kwamba: "Atakayeua mtu bila ya yeye kuua mtu, au kufanya fisadi katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote " (5:32). 

Maantiki ya kauli hii ya Qur’an ni kwamba akiuliwa japo mtu mmoja, mtu huyo ni sawa na binadamu mwingine yeyote; sio paka. Binadamu ambaye uhai na utu wake unapaswa kulindwa na kuheshimiwa sawa na binadamu mwingine yeyote. 

Binadamu ana hadhi yake na haki zake zinazoandamana na hadhi hiyo. Mwisho hata kama mtu anahukumiwa kifo kwa hukumu ya mahakama, haiwi kifo hicho iwe ni kuanza kumkata sikio, pua, kumtoboa jicho n.k., hadi afe. Zipo njia za kiungwana zinazokubalika duniani kote kutekeleza adhabu hiyo. 

Serikali imewachomea nyumba wananchi wa Nzasa kwa madai kwamba wamevamia na kuweka makazi ndani ya eneo la hifadhi ya msitu. 

Yawezekana wengi wa wananchi hao bado wapo nje wakiwa hawana makazi wala chakula. Lakini tatizo hivi sasa si lao, ni sisi. Ni kweli wao wataendelea kuteseka, lakini tatizo ni je, sisi tunafanya nini. Kudhalilishwa kwa mwananchi mmoja ni sawa na kudhalilishwa mwananchi mwingine yeyote. Hakudhalilishwa yule kwa vile yeye ni nusu mtu. Ni binadamu kama mimi au wewe. Tofauti kama ipo ni kwamba yeye kadhalilishwa leo, kesho yaweza kuwa zamu yako. 

Ikiwa ilikuwa kwa yule mama Kanda ya Ziwa aliyevuliwa nguo akawekwa pilipili puani na sehemu zake za siri. Juzi ikawa zamu ya akina mama wa Mwembechai kudhalilishwa. 

Waliuliwa wananchi huko Kilombero. Wale walikuwa wananchi sawa na wananchi wengine. Inawezekana kwamba wengine wakidhani ni wale si sisi. Juzi ikawa Mwembechai. 

Ubungo walivurumishwa bila fidia wala kupewa viwanja vingine, ikadhaniwa ni wale si sisi. Leo ni zamu ya Wana-Nzasa, hatujui kesho ni wapi. 

Matukio haya na jinsi yanavyopokewa na wananchi hapana shaka ni ishara mbaya ya huko tuendako. 

Iwapo tutaona ni sawa tu, kila mmoja anapita na zake huku mwenzao pembeni akikabwa na kibaka kuporwa saa yake; basi tujue hakitapita kitambo, vibaka hata wakiwa wachache kiasi gani utadhani wao wamekuwa wengi kuliko raia wazuri. 

Sote hatutakuwa na salama, tutatamani tuhame mji na tukose pa kukimbilia. 
 
Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
TAHARIRI 
Tutaendelea kudhalilishwa mpaka lini ? 

Waislamu wasisitiza: Nyumba ya Waziri Mkuu ni ya Waislamu 
Na Mwandishi Wetu 

Kuchomwa nyumba za wananchi 
Na Mwandishi wetu 

Maoni Yetu: 
Maisha ya Mtanzania yanapokosa thamani 

Nguruwe marufuku Kinondoni – Tume 
Na Kassim Juma 

Watanzania waanzisha Baraza la Waislamu Marekani 
Na Mwandishi Wetu 

Wanawake Hai wamtaka Rais azungumzie mauaji ya Mwembechai 
Na Mwandishi Wetu 

‘Serikali haiwezi kuzuia rushwa’ 
Na Kassim Msuya 

Makala ya Kimataifa 
Nani gaidi: Slobodan Milosovic au Usama bin Laden 
Na Mwandishi Wetu 

Afghanistan washindi dhidi ya uvamizi karne zote 
Na Faiza bint Abubaka 

MAKALA: 
Demokrasia ya rushwa ! 
Na Mwapwani Mohamed 

Tujikwamue na janga la utwaghuti 
Na I. Kikong’ona 

MAONI: 
Nini Jihad na nani Mujahidina ? 

MAKALA: 
Marekani ni magaidi wa haki za binadamu 
Na MUSSA ALLY 

Tufuate Uislamu kwa vitendo na siyo kwa maneno -2 
Mwandishi: Maalim Ali Bassaleh 

Tusihalalishe mauaji ya raia kwa kisingizio cha ‘wananchi wenye hasira’ 
Na Mwandishi Wetu 

Historia ya sayansi na tiba 
Na Dk. Amur A.A. 

Msiwageuze watoto ombaomba 
Na H.E. Omar 

MAKALA YA JAMII: 
Profesa Malise Kaisi acha uzushi dhidi ya Mtume Muhammad 

Sensa ya majaribio: Wananchi watofautiana na serikali 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Uislamu ulivyoingia Zanzibar -3 

Mwembechai wageuka Hame, Bado walindwa na polisi 
Na Badru Kimwaga 

Waislamu Moro waendelea kusaidia wagonjwa 
Na Rajab Rajab - Morogoro 

Mjadala wa Katiba ya Shirikisho kuzinduliwa Dar Jumapili 
Na Mohamed Othman 

Walimu wa dini Tanga wapokea Baiskeli 
Na Abu Said 

Mafundisho ya Quran 
Kutoa katika njia ya Allah: Al-Baqarah aya  264 

Barua za wasomaji 

Masomo ya dini ya Kiislam 

Chakula na Lishe 
Vitu vinavyoweza kuwemo katika vyakula 

 
 

 

 

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita