AN-NUUR
Gazeti la Kiislamu la kila wiki - Tanzania
Toleo
la Internet
|
|
|
Zikiwa
zimesalia siku 26 kupiga kura:
Wafumwa
wakigawa shahada za kuibia kura
JUZI kundi la wana CCM na watendaji wa serikali mjini Mwanza, walivamiwa wakidaiwa kugawa shahada za kuibia kura.
Mkasa huo ulitokea katika eneo la mlango mmoja kata ya Mbugani baada ya vyama vya CUF, NCCR na TLP kuvamia ofisi ya Mtendaji Kata na kuwakuta Mwanasheria wa Manispaa ya Mwanza, Katibu Mtendaji, Mwandishi Msaidizi wa wapiga kura na Mgombea wa CCM Mzee Ngofilo, wakiwa wamekamatia shahada na vitabu vya shahada kadhaa visivyotumika.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, mbali ya shahada hizo, "ambush" hiyo ilikuta vitabu vya shahada vilivyojazwa majina hewa kimoja kikiwa na nambari 163/d/31/354 na vingine vikiwa vimejazwa namba bila kuwa na majina. Endelea...
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |
Gazeti hili huchapishwa na Islamic Propagation Centre, Box 55105, Dar es Salaam