AN-NUUR
Gazeti la Kiislamu la kila wiki - Tanzania
Toleo la Internet

Toleo la Ijumaa    Toleo la Jumanne

Mbunge wa CCM aishambulia CUF

MBUNGE wa CCM jimbo la Handeni mashariki, mheshimiwa Dk. Abdallah Kigoda amedaiwa kusema sera ya CUF ya jino la jino inahatarisha amani na utulivu nchini.

Dk. Kigoda ambaye pia ni waziri wa Nishati amedai kuwa CUF imeamua kuwa na sera hiyo kwa kuwa imefilisika kisiasa.

Aliyasema hayo alipokuwa akizindua Tawi la wakereketwa wa CCM Kwamngumi mjini Handeni hivi karibuni.

Aidha waziri huyo wa Nishati alimponda mgombea wa kiti cha Urais wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba kuwa chama chake hakina sera ila ni udanganyifu. Endelea...

Kufuatia ziara ya Rais Mkapa:
Wakereketwa wa CCM wafadhaika Mwanza

BAADHI ya wakereketwa wa CCM wamedai ziara ya Rais Mkapa imewavunja nguvu mbele ya wapinzani.

Wamesema, walitaraji mapokezi, shamra shamra na hotuba ambapo zingepiku zile za chama cha CUF.

"Japo hakuwa amekuja kichama ametukata makali. Hatuna kauli tena mbele ya hawa ngangari", amesema Bw. Joseph wa mjini Mwanza. Endelea..


USIKOSE!!
Kitabu kipya cha Kompyuta kwa Kiswahili
Bonyeza hapa kwa maelezo zaidi

Soma NASAHA, Gazeti jipya kwenye mtandao...

To search in An-nuur:
Write a word or words in the space provided then press "Search". 



Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook

Gazeti hili huchapishwa na Islamic Propagation Centre, Box 55105, Dar es Salaam