AN-NUUR
Na.154 Safar 1419, Juni 19-25, 1998
 
Home 

Links 

Islam Tanzania 

Matoleo ya nyuma 
 
 

Kutoa talaka ovyo ovyo ni kuchupa mipaka ya Allah - Ust. Khamis Salim 

Na Mwandishi Wetu, Mtwara 

WAISLAMU wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kutoa talaka ovyo inayojengeka haraka haraka katika jamii ya Waislamu. 

Akihutubia katika Msikiti wa Ijumaa wa Noor Chikongola hivi karibuni, Ustadh Khamis alikemea vikali mtindo huo ambao jamii kama itaendelea kukaa kimya kuna hatari ukazoeleka. 

Akinukuu aya kadhaa ndani ya Qur'an zilizomo katika Surat Twalaq alisema kuwa, kweli takala ni halali, lakini inayomuudhi Allah (sw) na vile vile ina masharti, taratibu na misingi ya kufuata kabla mume hajamuacha mkewe. 

Akinukuu Hadithi za Mtume (saw) na kulinganisha na visa vinavyohusiana na takala vilivyojitokeza wakati wa Mtume na Makhalifa wake, alisema kuwa, imekuwa ni tofauti sana na wakati huu. 

Aliwaomba sana Maimamu na viongozi wa ngazi zote na taasisi zilizo na majukumu katika jamii yetu kuyakemea kwa nguvu zote maovu haya na kuwataka Waislamu kujishughulisha kwa wingi darasa za jioni popote zilipo na kuwauliza wataalamu wa dini hii mara mtu apatwapo na mushkeli juu ya mambo yake ya ndoa. 

Mwandishi wa habari hizi alizungumza na baadhi ya wazee wa mji wa Mtwara na wasomi aliobahatika kukutana nao kwa ujumla, walionesha sura za kuhuzunikia suala hili, baadhi yao walisema kuwa mengi yamesababishwa na mazingira ya mikoa ya Kusini hasa umaskini na kudumaa kwa elimu zote. Walisema watu wengi na hasa vijana wanajishughulisha mno namna ya kujinasua kimaisha. 

Wengi wamempongeza Ustadh Khamis Salim kwa uzindushi wake muafaka. 
 
 
 

Uislamu ni mfumo wa maisha - Mbukuzi 

Na Said Shariff 

IMAM wa Masjid Mujahiduun, Sheikh Juma Mbukuzi amesema Uislamu haukamiliki kwa kuswali tu, bali swala ni taasisi ya maandalizi katika kuuendea Uislamu katika kila kipengele cha maisha ya kila siku. 

Sheikh Mbukuzi ameyasema haya aliopokuwa akizungumza na Waislmu baada ya swala ya Ijumaa Juni 12, `98. 

Akifafanua kauli hiyo, Sheikh Mbukuzi amesema, Uislamu ni mfumo kamili wa maisha wenye manufaa kwa watu. 

Amesema pamoja na swala, kufunga Ramadhani Uislamu unahusika na jukumu la kuiendesha jamii kisiasa, kiuchumi kwa kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu (s.w.) na kila nyanja ya maisha. 

Alinukuu Hadithi ya Mtume (s.a.w.) isemayo, `pindi Uislamu utakapofuatwa sawa sawa, katika jamii hakutakuwa na ombaomba mitaani., hii ni kwa sababu taasisi ya zaka itachukua nafasi yake na kufanyakazi yake. 

Kinyume cha hivyo, Sheikh Mbukuzi amesema mifumo isiyokuwa ya Kiislamu ni janga katika jamii kwa sababu watu wenye nafasi huwakamua maskini wasio na uwezo hata wa kulipia ada za shule kwa ajili ya watoto wao wanaosoma. Ambapo katika Uislamu maskini ni mtu ambaye kwanza lazima asaidiwe. 

Kwa hali hiyo, Sheikh Mbukuzi amesema Waislamu wanajukumu la kufanya juhudi kuifikia hali hiyo na kuiokoa jamii kutokana na madhara ya mifumo ya kikafiri. 

Wakati huo huo, Sheikh Mbukuzi ametoa pongezi kwa akina mama wa Kiislamu waliojitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano wa wanawake wa Kiislamu uliofanyika Juni 7, `98 Sinza Masjid Nuur, Jijini. Amewataka wanawake hao wawe wanawake wema wa Kiislamu wa kweli kweli kwa sababu wao ni kiungo muhimu katika kujenga maadili mema katika jamii na wawe mfano bora kwa akina mama wengine. 
 
 

 
 

YALIYOMO
 
 
TAHARIRI  

Maoni yetu: 
Kama hodari wa kuhoji Tuhoji pia Tume ya Majeshi ya Vita 

Waraka wa Abu Aziz  

Unafiki si suala la wakati fulani  
  
Wakatoliki wawili wasilimu 

Ashitakiwa baada kusilimu 

Historia ya harakati za ukombozi wa Kashmir 

Sheikh wa Wilaya Same ahimiza Waislamu kushiriki tamasha 

Sheikh awataka wanawake wajistiri 

Madrasat Al-Hujuun washerehekea mwaka mpya 
 
Kutoa talaka ovyo ovyo ni kuchupa mipaka ya Allah - Ust. Khamis Salim 

Uislamu ni mfumo wa maisha - Mbukuzi 

Pole ya Mwinjilisti Kusupa ni kejeli 
 

 

 
 Maoni yoyote kuhusu ukarasa huu yapelekwe kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
An-nuur Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita