AN-NUUR
Na.154 Safar 1419, Juni 19-25, 1998
 
Home 

Links 

Islam Tanzania 

Matoleo ya nyuma 
 
 

TAHARIR 

Ukawamu gani huu! 

Mwenyezi Mungu anatuambia katika Qur'an kwamba wanaume ni Walinzi (Qawamuna) au wasimamizi wa wanawake. 

Marais na Wafalme katika nchi huteuwa watu katika nyadhifa mbalimbali ili kutekeleza kazi na majukumu ya kiserikali. 

Wanaume hawa Waislamu hawateuliwi na Rais wa Taifa kubwa wala Mfalme mwenye utajiri na nguvu kubwa za kijeshi. Wanateuliwa na Mungu Muumba wa Wafalme na Marais kwamba wawe walinzi wa wanawake. 

Lakini mabinti, wake na akina mama wanalalamika na kumshitakia Mwenyezi Mungu kwamba Qawamuna" hawa wamebakia kuvaa kanzu safi na kujitia manukato tasbihi mkononi huku akina mama hao wakivuliwa nguo na kudhalilishwa! 

Wengine hodari wa kutoa mawaidha, kudarasisha na mahiri wa kunukuu aya na hadith. Lakini akina mama wanalalamika kwamba umahiri wao huo hauna tija yoyote kwao. Wanahoji "Qawamuna"gani asiyestuka mkewe akivuliwa nguo! Qawamu gani asiyestuka binti yake akidhalilishwa! Tunawashukuru akina mama kwa ujasiri wao kwamba pamoja na mateso waliyopewa na kutishwa hawakuhofu wala kunyamaza. Hii inatupa faraja kwamba tunapata Waalimu wazuri katika jamii yetu ya Waislamu. 

Hata hivyo tungependa kuwakumbusha akina mama wasisahau kwamba bado wako Waislamu wengine ndani, wengine bado majeraha kupona na tunao bado akina Chuki Athumani. 

Tuwasaidie na kuwafariji ndugu na jamaa za wale ambao bado wako ndani. Tuwasaidia gharama za matibabu ambao bado wanauguza majeraha. Na tusikose kuwajulia hali waliopo bado hospitalini. 
 
 

 
 

YALIYOMO
 

TAHARIRI  

Maoni yetu: 
Kama hodari wa kuhoji Tuhoji pia Tume ya Majeshi ya Vita 

Waraka wa Abu Aziz  

Unafiki si suala la wakati fulani  
  
Wakatoliki wawili wasilimu 

Ashitakiwa baada kusilimu 

Historia ya harakati za ukombozi wa Kashmir 

Sheikh wa Wilaya Same ahimiza Waislamu kushiriki tamasha 

Sheikh awataka wanawake wajistiri 

Madrasat Al-Hujuun washerehekea mwaka mpya 
 
Kutoa talaka ovyo ovyo ni kuchupa mipaka ya Allah - Ust. Khamis Salim 

Uislamu ni mfumo wa maisha - Mbukuzi 

Pole ya Mwinjilisti Kusupa ni kejeli 

 

 
 Maoni yoyote kuhusu ukarasa huu yapelekwe kwa: islamtz@wowmail.com
 
An-nuur Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita