Na Mwandishi Wetu, Mwanza
CHUO cha Biblia cha Kanisa la Inland Church kilichopo Katunguru Sengerema bado kimefungwa. Aidha, inasemekana kuwa baadhi ya wanafunzi wamefukuzwa na wengine kuhamishiwa Vyuo vingine.
Mapema mwezi uliopiga mtafaruku mkubwa ulizuka Chuoni, wanafunzi wa chuo hicho cha Biblia walipohoji tofauti mbalimbali za ibada za Kikristo pamoja na mambo mengine.
Kiu ya wanafunzi hao kuhusu mas'ala mbalimbali ya dini hiyo ilichochewa na yale waliyoyasikia kwenye muhadhara wa AL MALLID tawi la Mwanza.
Kufuatia sakata hiyo Jamhuri iliwafungulia mashitaka wahadhiri hao. Kesi hiyo ambayo inaendeshwa na Hakimu Bw. E. Raphael inawahusisha wahadhiri Athumani, Hussein, Twalib Abdallah, Rashid Shaaban na Issa Rajab.
Kesi hiyo No. 83/99 itatajwa tena Juni 22, mwaka huu.
Juhudi za gazeti hili kupata maelezo kamili juu ya mashitaka rasmi yaliyowasilishwa mahakamani dhidi ya wahadhiri hao hazikuweza kufanikiwa.
--
|