|
|
|
KWA kipindi kirefu Uyoga (Mushrooms) ulijulikana kama kiumbe sawa na mimea. Hata hivyo, uchunguzi wa kisasa wa sayansi umebaini kuwa uyoga ni tofauti kabisa na mimea (plants). Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa uyoga una baadhi ya sifa ambazo ni sawa na zile za mimea na pia una baadhi ya sifa ambazo ni sawa na zile za wanyama (animals). Kutokana na utata huo, wanasayansi wa sasa wameuweka uyoga na "ndugu" zake katika kundi lao ambalo ni "Kingdom Myceteae". Kwa asili, uyoga huota katika ardhi, miti iliyooza na katika takataka mbalimbali. Kwa mujibu wa teknolojia ya kisasa, uyoga unazalishwa bila ya kutumia udongo. Kinachohitajika ni kitu kama mabaki ya mimea ambayo huitwa "Substrate" na hali ya hewa yenye kuruhusu ukuaji wa uyoga. Si makusudio ya makala hii kuelezea namna ya kilimo cha uyoga kinavyoweza kufanyika. Uyoga umeanza kutumika kama chakula (mboga) miaka zaidi ya elfu mbili iliyopita. Lakini kuna baadhi ya aina za uyoga ambazo zina sumu na hivyo zinaweza kumuatihri mlaji. Uyoga kama mlo una thamani kubwa katika mwili wa mwanaadamu. Thamani ya kwanza ni kuwa, uyoga unaupa mwili virutubisho (nutrients). Na thamani ya pili, uyoga una upa mwili ‘dawa’ ambayo inasaidia kuponya baadhi ya maradhi (mfano saratani) na pia unatoa dawa (interferon) ambayo inaupa mwili kinga ya magonjwa yanayosababishwa na virusi ( lakini siyo ukimwi). Virutubisho vinavyopatikana katika uyoga ni kama vile protini, madini, vitamini, maji na kabohaidreti. Uyoga una protini kiasi cha asilimia 8.1 - 43.0 kutegemea na aina ya uyoga na mahali (substrate, hali ya hewa n.k.) ulipoota au ulipozalishwa. Vile vile uyoga ni chanzo kizuri sana cha vitamini ya kundi B. Kwa mfano Thiamine (B1), Riboflavin (B2), Nicotinic acid, Pantothenic acid na kiasi kidogo cha vitamini B12. Pia uyoga una vitamini C (Ascobic acid) na vitamini K. Vitamini A, D, na E pia zinapatikana katika uyoga, lakini kwa kiasi kidogo sana. Madini mbalimbali pia zinapatikana katika uyoga. Mfano wa madini hizo ni Potassium, Sodium, Phosphorus, Culcium, Magnesium, Iron (chuma) na Copper (shaba). Uyoga vile vile una kiasi cha asilimia 3 - 28 ya Kabohaidreti (sukari, glycogen, nyuzi nyuzi, n.k.). Zaidi ya hayo, uyoga una kiasi fulani cha maji. Tukizingatia thamani kubwa tunayoweza kuipata kutokana na mlo wa uyoga,
nawahimiza wananchi kuongeza uzalishaji wa uyoga na pia ninawaomba waongeze
utumiaji wa uyoga kama mlo.
|
YALIYOMO
Tahariri Baada ya futari nzuri: Tuwatupie macho wenye njaa Rais Mkapa kuwa mgeni rasmi Baraza la Idd Waumini, Masheikh Arusha wasutana kwa futari ya Mrema Dondoo za saikolojia
MSADAT yazidi kutia moyo Tanga MAFUNZO KUHUSU FUNGA YA RAMADHANI Michezo isiyoruhusiwa katika Uislamu Ustadh Farid: Kijana aliyejitolea kuwapa Da'awa watalii Hakuna Magharibi wala Mashariki:
Uislamu ni ubinaadamu
Ijue madrasati Mar-wa ya Dodoma
mjini
Ijue Madrasat Jadidul Fiqhyyat
- Tabata Kimanga
Madrasat Hidayatul Muumini Mwadui Washindi wa mashindano ya Hadithi za Mtume (s.a.w.) wapatikana Madrasa Shafii Ujiji Kigoma yaonyesha umahiri wake Waanzisha mifuko kusaidia wagonjwa Dodoma Waislamu Kondoa waomba msaada kumalizia Msikiti Mnyororo wa imani-2
Kutoka magazeti ya zamani:
Jengo la Waislamu Moshi lageuzwa
Kanisa la Walokole
Masjid Nurania yaswaliwa
Ijumaa
Jabal Hira kutoa mafunzo
ya Kompyuta Morogoro
Sayansi na Teknolojia
Chakula na lishe
|