AN-NUUR 
Na.183 Ramadhan 1419, Januari 8 - 14, 1998 
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita
 
MASHAMBULIZI YA MAREKANI NCHINI IRAQ 

Dhuluma ya Marekani dhidi ya Waislamu 

Yafuatayo ni " Mazungumzo ya Ijumaa toka Masjidi Al-aqsa-Al.Quds" ambayo hutolewa na wanachama wa Hizb ut Tahrir. Mazungumzo hayo kwa e-mail: 
Info<penangle@ppencil. freeserve.co.uk >  

Mazungumzo haya pia yanaweza kusikilizwa katika lugha ya Kiarabu kupitia mtandao wa komputa ulimwenguni www.al-aqsa.org. Mazungumzo yafuatayo yalitolewa Ijumaa 25/12/98 na yalichukua muda wa dakika 11.  

Sifa njema zinamstahiki Allah. Tunaomba uongofu na ushindi toka Kwake (Allah) pekee, "Yule ambaye Allah amemuongoza basi huyo ameongoka barabara; Lakini yule ambaye Allah amemuacha apotee, wewe hutampatia mlinzi mwingine (zaidi ya Allah) wa kumuongoza katika Njia Iliyonyooka". 

Ninashahidia kuwa hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na kwamba Muhammad mja wake (Allah) na ni Mtume wake (Allah). 

Enyi Waislam, Katika Ijumaa ya kwanza ya Ramadhani mwaka huu, tunakukaribisheni mahali pa safari ya usiku (Istar) iliyofanywa na Mtume Muhammadi (s.a.w.). Tunakutoleeni salaam na tunamshukuru Allah kuwa ametuwezesha sisi sote kuushuhudia tena mwezi wa Ramadhani. Tunamuomba Allah atuwafikishe katika funga zetu wakati wa mwezi huu uliojaa baraka, na tunamuomba Allah atughufirie madhambi yetu yaliyopita na atuepushe mbali na moto wa Jahannam. 

Enyi Waislam, 

Leo tutazungumza kile ambacho kila mwislam kwa sasa anakizungumzia - matukio ya huko Iraq. Tutazungumzia ni kwanini Marekani imeipiga mabomu Iraq; kwanini Marikani imekoma; kwa nini ichague kufanya mashambulizi mwanzoni mwa Ramadhani; na iwapo Marekani itaipiga tena mabomu Irag au la. 

Hivi mpaka lini Mrekani itaendelea na ubabe wake, kiburi chake, kujifaharisha na uharibifu wake katika ardhi hii? 

Je, muda haujafika tu (kwa ulimwengu) kukomesha vitendo vyake [Merekani] ? Je muda haujafika wa kuing’oa Marekani toka katika ardhi yetu na kusimamisha, badala yake, dola ya haki - Dola ya Khalifa wa Kiislam? 

Enyi Waislam 

Marekani inataka kuendeleza "uhodhi" yake na utawala wake wa mabomu juu ya mataifa mengine yote. Inataka kuzuia njia na taratibu za nchi zingine ambazo zinajaribu kushirikiana na Iraq na kunufaika kutokana na biashara ya mafuta. Ikaamua kwamba kwa msaada wa makombora ya Tomahawak, 

makombora ya Cruise na mabomu ya B-52, yenyewe [Merekani] ndiyo itakuwa mla nyama!. 

Marekani ikaandaa aina zote za silaha na ikachagua mwanzo wa (mfungo ) Ramadhani kuanzisha mashambulizi yake - mudo mfupi sana baada ya Rais wake (Clinton) kurejea mikono mitupu toka Israel. Mji wa Baghdad ulipigwa mabomu, kama ulivyofanywa mji wa Al-Basra. Hao wanaoitwa watetezi wa haki za binaadam waliandika ujumbe katika makombora hayo kama vile " This is the American Present to the Muslims in Iraq on the occassion of Ramadhani" ( Tafsiri hii ni zawadi toka Marekani kwa Waislam wa Iraq kufuatia kuanza kwa mfungo wa Ramadhani). 

Zawadi hizo za ‘Uncle Sam’ zimepelekea wanawake na watoto kuunguzwa na kuuawa. Wamerekani hao walirusha makombola katika hospitali za mji wa Baghdad. Hivi watoto wachanga katika hospitali hizi walifanya uhalifu gani kiasi wao kustahili kuuawa namana hiyo? Ni namna gani vichanga hawa waliidhuru kiasi wao kustahili kuuawa pamoja na mama zao, wazazi wao na matabibu wao. 

Kwani hospitali hizi zilipata kutengeneza silaha za sunu? Kwani hospitali hizi ndizo zilizoishutumu Marekani au ndizo zilizomshutumu Bw. Butler (Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Ukaguzi wa Silaha za Iraq) kuwa ni ‘agent’ wa C.I.A. (Shirika la Kijasusi la Marekani)?. 

Kwa nini katika mwanzo wa Ramadhani ghala zza ngano zipigwe mabomu? Kwa nini ngano na mchele vilichomwe moto huko Iraq ? Nchi ya Iraq ambayo imetengwa! Iraq yenye NJAA! Je? Jii ndiyo haki kwa Merekani na Uingereza? 

Enyi Waislamu, 

Kwa nini kiwanda cha kusafisha mafuta huko Al-Basra kililipuliwa? Kwani hapo kuwandani kulikuwa na silaha za nyukilia au silaha za sumu au vifaa vya kutengenezea silaha? Ni katika namna gani kwamba Kiwanda hiki cha mafuta kiliiathiri Marekani? 

Enyi watu, 

Utawala wa Marekani ulitangaza kuwa lengo lake lilikuwa ni kuung’oa utawala wa Suddam Hussein. Lakini badala yake, makombora na mabomu yalitupwa juu a vichwa vya (raia) wenye njaa na wenye kuhitaji msaada. 

Marekani imeshindwa kukamilisha lengo lake la kuipiga mabomu Iraq. Haikuweza kuwakusanya washirika wake kama ilivyokuwa imepangwa. Marekani ilirusha angani makoratasi yenye kuwachochea wananchi wa Iraq kufanya uasi dhidi ya utawala wa Iraq kama hatua ya awali ya kuiangusha serikali ya Iraq. Lakini wananchi hawakuitika wito huo, badala yake, makundi kwa makundi ya Waislaam uliwengu mzima yaliungana kuipinga Marekani. Waliandamana kwa uchungu mkubwa wakipinga matashi ya Serikali za kidhalimu. Kisha hiyo Marekani ikadai eti inaheshimu utukufu wa mwezi wa Ramadhani. 

(Baada ya kutuma zawadi zake kwa Waislam wa Iraq). Hivyo[Merekani] ikasitisha upigaji mabomu ipate kutathimini upya hayo matukio. 

Hii ni moja ya sura katika sura kadhaa zinazokuja (tutakazowaletea) kati ya Marekani na Iraq. 

MWISHO 
 
 

Juu 
 

YALIYOMO 
 
 
Tahariri 
Onyesheni ushujaa wa Badri 

Daniel kuwatimua waumini Msikitini 

Waislamu Moshi: Wadai kulishwa nguruwe, vibudu 

Dondoo za Kisakolojia 
Na. Abu Halima Sachangwa 

Kona ya WachaMungu  

Jicho la Uzalendo 

Maulana Sayyid Jamal-Din Afghan 1214 - 1254 (1838-1897) - 2 

Vipi umoja wetu uwe hatari ? 

MASHAMBULIZI YA MAREKANI NCHINI IRAQ  

Marekani si rafiki mwema  

Tunahitaji UN ya Waislamu - 2  

Njia bora zitakazotusaidia kuwalea watoto 
Na Ust. Hashim Rusaganya, Mombasa 

Ijue Madrasatul-Qaadiriya Sokoni I Arusha. 
Na Habiba Swedi, Arusha 

Tutafute kwanza ufalme wa Allah (s.w.) 
Na Mwapwani Mohammed 

Sheikh Kisiwa atunuku zawadi 

Chuo cha Kilimo Ukiriguru kupata Msikiti mpya  
Na Mwandishi Wetu, Mwanza  

Huduma za maji Kondoa haziridhishi 
Na Abu Zuberi, Kondoa  

Mnyororo wa imani 
Na Sheikh Bernard P. Nyangasa 

Je, Yesu alibatizwa? 
Na Muhibu Said  

Kufuatia Waislamu kuritadishwa Merela Morogoro: Masheikh wa mjini watupiwa lawama  

Abiria walaani kumwagiwa pombe Kondoa 

Sheikh Bafadhil ateuliwa kudhamini waandishi wa habari Morogoro 
Na Mussa Ally, Morogoro 

Sayansi na Teknolojia 
[Tatizo la mwaka 2000] 

Masomo ya Dini ya Kiislamu 

Barua za Wasomaji 

Chakula na lishe 
[Mlo wa siku ya Idd] 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtanzania.org
 
Home Links Islam Tanzania Matoleo yaliyopita